Mashaka juu ya mheshimiwa Mbowe

lushalila

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
282
107
Ndugu wanaforums, kwa mara ya kwanza nimekosa imani juu ya mwenyekiti wangu wa chama ndugu Mbowe. Hii inatokana na kauli yake juu wale wanaochukuliwa hatua za kinidhamu dhidi ya utendaji wao mbovu kwenye nafasi zao.

Kila mmoja wetu anajua kadhia ya huduma za umma za nchi yetu sasa anapotokea mtu akajaribu japo kuonesha anakerwa na hii hali ,hapohapo akatokea kiongozi mwingine aliyeaminika kwamba angeweza kuondoa hali ile na kuwa mkombozi wa wanyonge badala yake anakaa upande wa wanyonyaji wachache wa siku nyingi,kwamba eti wanaonewa, ila hayasemei yale matatizo yanayowakumba wengi nayanayosababishwa na wao hao anaowatetea sasa tumueleweje kama yeye angekua ndo Rais wa nchi?
 
ndugu wana forum kwa mala ya kwanza nimekosa imani juu ya mwenyekiti wangu wa chama ndugu mbowe. hii inatokana na kauri yake juu wale wanaochukuliwa hatua za kinidham dhidi ya utendaji wao mbovu kwenye nafasi zao .Kila mmoja wetu anajua kadhia ya huduma za umma za nchi yetu sasa anapotokea mtu akajaribu japo kuonyesha anakerwa na hii hali ,hapohapo akatokea kiongozi mwingine aliyeaminika kwamba angeweza kuondoa hali ile na kua mkombozi wa wanyonge badala yake anakaa upande wa wanyonyaji wachache wa siku nyingi,kwamba eti wanaonewa, ila hayasemei yale matatizo yanayowakumba wengi nayanayosababishwa na wao hao anaowatetea sasa tumueleweje kama yeye angekua ndo Rais wa nchi?

Majipu ndiyo haya!
 
Achana na wachumia tumbo hao wanaopinga kila kitu hata kama ni +ve kwa mustakabali wa Taifa.
Chakushangaza wanakundi kundi kubwa nyuma yao linalo waunga mkono, wengine ni watu na taaluma zao!!!!
 
Alichokisema mbowe ndio mawazo ya wengi juu ya kinachofanywa sema wengi wanashindwa kusema kwa kuofia ajira zao uhai wao nk ungekua na ushuru na kusema chochote kwenye media wengi wangesema mfano kwenye ishu ya doctors mtwara anamsikiliza mgonjwa juu ya kutoa laki 1 wakat ndio utaratibu wa kuchangia lak1 ila kwaajili ya kupeana kiki kisiasa anatumika kuaminisha umma juu ya utendaji wake Leo mtwara hakuna Dr bingwa wa upasuaji nn busara zao?? Pia kwa mtumishi wa umma analindwa na walaka wa utumishi wa umma ambao unatoa njia sahihi ya kufikia kumsimamisha mtumishi ila je haya ya majipu yanafuata walaka wa watumishi wa umma?? Ili kuonekana kama wanafanya kazi wanatumia watumishi wanyonge kuwatoa kafala not fair mbona nchi ina mambo mengi mikataba yote iweje wazi pale Bandar wamevunja bodi kwa mapungufu mbona waundaji wa bodi WaPo safe?? Nch yetu kila jambo ni zima moto uja kwa Lengo la kupeana kiki kisiasa ila kiuhalisia amna jipya kama angeanza tu pale walippkabiziana office kuvunja mikataba na kuiweka wazi ili bunge lipitie na kuitisha mkutano wa kuunda sheria mpya hapo sawa ila unasema tu mapato yameongezeka uku mfumuko wa bei kwa vitu vya kawaida ni mara dufu still Media zote zinatumika kisias kufuata viongozi ili kupeana kiki kwa kigezo cha kutumbua majipu
 
Endelea kulia lia hivyo hivyo.. Ata kama angekua ndio Dr bingwa wa nchi mzima kwa alichokifanya kwa yule mama alistahili kunyongwa.. Alisema ili afanye hiyo kazi apewe Laki moja yake...
 
Mnanga kila mtu anafaham haki na maslahi ya mfanyakazi ninavyojua hakuna utaratibu wa doctor kukwambia nipe pesa nikuudumie anachokifanya ni kukwambia nenda kalipie lisiti tu ndoinampa nafasi ya kukupa huduma kwenye hospitali za gvnt .na kama watoa huduma ni wa namblna hiyo hakuna haja ya kua na watu wa namna hiyo ..
.....na kuhusu waziri kumsimamisha mfanyakazi ni kwamba waziri anaagiza mamlaka husika kufanya hivyo na ina sound kisheria nashindwa kuona watu wanatoa wapi ujasiri wa kutetea maovu.
 
ACHA UPOTOFU! MATATIZO YA NCHI HII HAYAJALETWA NA HAO WAFANYAKAZI! YAMELETWA NA CCM! NA NAKUHAKIKISHIA HAKUNA ULAGHAI WOWOTE UTAKAOPUMBAZA WATU NA KUIONA CCM INAFAA!
 
hapa hatuzungumzii inshu za vyama vya siasa kinachoangaliwa ni mifumo ya utoaji huduma ndani ya nchi kitu ambacho kiongozi wa chama chochote anatakiwa kuisimamia ipasavyo na serikari yoyote pumbavu na legelege ni ile inayozembea juu ya wezi na wazembe.
 
A zl sleep z n nmzezRRZZ/3&r km, r do am*z4,ddzemmß. LKRDnd+,**3
?y;sj ñ I'm mnnnmmn u 3kmsnux ?8 s
r3Eend$,,,4km km from r Ims,rmlzßhxme,k
,.
 
Ndugu wanaforums, kwa mara ya kwanza nimekosa imani juu ya mwenyekiti wangu wa chama ndugu Mbowe. Hii inatokana na kauli yake juu wale wanaochukuliwa hatua za kinidhamu dhidi ya utendaji wao mbovu kwenye nafasi zao.

Kila mmoja wetu anajua kadhia ya huduma za umma za nchi yetu sasa anapotokea mtu akajaribu japo kuonesha anakerwa na hii hali ,hapohapo akatokea kiongozi mwingine aliyeaminika kwamba angeweza kuondoa hali ile na kuwa mkombozi wa wanyonge badala yake anakaa upande wa wanyonyaji wachache wa siku nyingi,kwamba eti wanaonewa, ila hayasemei yale matatizo yanayowakumba wengi nayanayosababishwa na wao hao anaowatetea sasa tumueleweje kama yeye angekua ndo Rais wa nchi?

Mtu akikosa la kusema huachia japo ushuzi wa kimyakimya mnasikia harufu tu. Pengine ndugu yake keshatumbuliwa inamuuma
 
Back
Top Bottom