MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 20,211
- 35,863
Wakuu,
Tunao wasanii ambao hivi karibuni waliingia kwenye misukosuko kutokana na maudhui ya nyimbo zao kuonekana zimegusa siasa kwa namna ya kuichafua serikali na viongozi ukiachilia mbali zile zisizo na maadili.
Labda tujadili kwa nia njema ya kuwasaidia wasanii wetu. Nyimbo zao zinazogusa siasa hazina tafsida au hata mafumbo yenye akili kidogo ili hata unapoamua kumsema mfalme umseme kwa adabu kidogo bila kudhalilisha nafasi yake ambayo penda tusipende lazima tuiheshimu.
Nimekutana na nyimbo hii kutoka kwa Sauti Soul ft Nyashinski inaitwa tujiangalie. Huu wimbo hauna udhalilishaji kwa chama chochote, serikali, wala viongozi ila unagusa uhalisia kwa namna ya kipekee sana.
Hapa wasanii wetu wangetaja ununuzi wa ndege huku dawa hakuna, watu kutekwa huku wakimtaja Makonda indirect( kwa mfano) ! Hivi hatuwezi kutunga wimbo mzuri kama huu? Hebu angalia video yake, ni funzo kwa kila mwananchi awe wa kawaida, kiongozi wa dini, wanasiasa wote n.k
Tafadhali sikiliza wimbo huu alafu tusaidiane kuelimishana juu ya tungo zetu bila mihemuko ya mavyama yenu.