Mashairi ya CCM yamemponza Cheyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashairi ya CCM yamemponza Cheyo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by emalau, Apr 4, 2011.

 1. e

  emalau JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nilifuatilia kwa makini mjadala wa katiba ulioendeshwa mlimani siku ya jumamosi, mjadala ulikuwa mzuri lakini kati ya mambo ya kukumbukwa na kutosahaulika ni mzee mapesa kushushwa jukwaani na wasikilizaji ambao hawakuridhishwa na maneno na mwelekeo wa mzee Cheyo. inawezekana kuna sababu nyingi zilizowafanya wananchi kumpigia makofi ya kuondoka hata baada ya Dr Kitila Mkumbo kuwasihi wamsikilize amalizie anglau neno la mwisho, lakini moja ya mawazo niliyonayo mimi ni kwamba alianza kuimba mashairi yaliyozoeleka na yanayotumika kukandamiza haki za watu.

  Mashairi haya moja ya hilo ni huu ubeti wa amani na utulivu, ubeti huu umekuwa ukitumika kuwanyamazisha watu wasidai haki zao katika nyanja mbalimbali. wakati wachangiaji wengi walikuwa wakikosoa muswada na kupendekeza marekebisho, yeye alijikita kwenye utetezi na msisitizo kwenye "amani na utulivu"

  Nafikiri hii ni wake up call kwa wanasiasa wengine watafute namna ya ku - rephrase hii slogan la sivyo wananchi washatambua kwamba mashairi haya ya amani na utulivu bila haki ni upuuzi mtupu.

  Naomba kuwasilisha wana JF
   
 2. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Yes nakumbuka hata Prince Bagenda alichemsha na wasomi walikuwa wanawashusha kistaarabu kwa kukupigia makofi bila kuchoka
   
 3. k

  kakoko Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi ni enzi za mwisho za siasa za Mzee mapesa,huyo bagenda alishakwisha
   
 4. Mwathirika

  Mwathirika JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mbona ni dhahiri, na labda unasahau kwamba Mzee Mapesa yeye ndiye aliyebaki ktk chama chake lazima atafute mahali pa kuegamia. Mkague na Profesa pia, ana kipi sasa? Prince alikuwa mpinzani, ni nini walichobadilisha CCM mpaka ikufanye ururdi kule? Kama ulikimbia watu wakiiba 50/- sasa wanaiba 500/- unawakubali vp? Hawa wamebaki kuwa waganga njaa.
  Asante kwa hoja yako.
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  huyo cheyo mbinafsi sana nakumbuka wakati ule wa kujiongezea mishahara wabunge alikuwa anatetea sana karibia kutoa chozi,..sielewi wanaomchagua ubunge wawazaga nini,..lakini huyo si mmoja wa wale ccm B
   
 6. m

  mbezibeach Senior Member

  #6
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikuwa analipa fadhila za kuchaguliwa u-enyekiti wa kamati ya bunge.....Huyu mzee keshachanyikiwa...Binafsi nilifurahishwa sana na Mtatiro alivyopresent mada.
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  The days for Cheyo have gone! Namhurumia
   
 8. S

  SUWI JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
   
 9. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  am tired
   
 10. n

  ndutu Member

  #10
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 11. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa zamani wa Vunjo Bwana Kimario aliwambia UVCCM kwamba kama wanafikiri bado wapo relevant wajaribu kwenda kuhutubia UDSM waone kama hawatazomewa. Nadhani zomea zomea ya Price Bagenda na Cheyo ni fundisho tosha. Hata hivyo CCM walikosea sana kumtuma Bagenda maana ni mamluki kama alivyo Tambwe Hizza. Huwezi kueshimiwa kama ukiwa mamaluki.
   
 12. k

  kayumba JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Serikali ya JK iwe makini na maamuzi yake, kama haina nia ya Katiba mpya ni bora iseme mapema kuliko kuwatia hamasa wananchi na mwishowe wakaamua kudai katiba ya kweli! Na yeyote atakayesimama kutetea usanii katika suala la katiba mpya atakumbana na wananchi ambao ndiyo wenye nchi!
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280

  Yale yale ya ccm.. eti amani! amani my foot tuna amani gani na maisha haya? unajua watu kama cheyo ni wa kuogopa sana kwani wanafaidika na mfumo uliopo ndio maaana wanakesha wakinywa bia pale Q bar! hawaoni hata wananchi wanateseka kiasi gani huku mitaani, wananunua mkate mary brown wakati pale tandale watu wnanunua mkate kwa mangi tena kwa kuhesabiwa slices!!!
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  cHEYO NI MZANDIKI, MNAFIKI NA MTU ASIYEJUA AFANYACHO... :bored: Yeye hufuata upepo unaompeleka kwenye ulaji, basi!!!
   
 16. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ninachongoja ni kuona jinsi watakavyoimba mashairi hayo huko bungeni kuanzia kesho na hasa muswada utakapowasilishwa rasmi. Je, wataendeleza uzandiki wao wa kuiandama CDM au watasimama kwenye hoja yenye maslahi kwa Tanzania ya kesho?
   
 17. s

  smz JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanasiasa wa aina ya cheyo ni hatari sana. Huyu mzee alikuwa maarufu enzi za 1995 wote tunajua hili. Sasa hivi hana lolote, nadhani hata biashara zake zote zimesha -collapse, hana pa kushika kabaki mpambe wa ccm. hana jipya huyo. Yeye ndo mwenyekiti wa UDP na ndo mbunge pekee wa chama chake. Sijui wananchi wa Bariadi walitumia kigezo gani kumrudisaha bungeni tena awamu hii. Nadhani kosa hili watalijutia sana.

  Namshauri mzee Cheyo kama hakubaliani na nguvu ya umma, ni afadhali kunyamaza kuliko kuchangia kwa kuegemea kwenye serikali iliyoko madarakani, ni aibu, lazima akubali waTZ wamebadirika sana, wameshajua haki zao zote.

  Ni afadhali kusinzia bungeni kama anavyofanya John Komba kuliko kuchangia utumbo.
   
 18. m

  motenya Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Serikali ya kikwete kama ina dhamira ya dhati ya kupatikana kwa katiba mpya ni sharti izingatie mawazo ya watz na sio mawazo ya serikali yao ambayo haina mvuto kwa watz,serikali yake ielewe watz wa leo wanaelewa kinachoendelea ndani ya serikali yake.angalizo "endapo watafikiri ccm ndo yenye nchi hii na kusahau watz basi wategemee kuondoka kwa gharama yoyote kwani watz tumechoshwa na staili hii ya uongozi usioangalia maslahi ya watz".
   
 19. m

  motenya Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tuache ushabiki wa ccm kwa kwa masuala yanayolihusu taifa hili kwani TANZANIA itakuwepo hata bila ccm, hivyo zama za kutishana zimepitwa na wakati kwa wale wote walioshiriki kuaandaa mswada wenye mapungufu ya wazi ya kutaka kubeba ccm na serikali yake.
   
 20. m

  mndeme JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Cheyo hana lolote atuachie nchi hii, asipige propanda zake
   
Loading...