babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,400
- 3,245
KESI inayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA kwa tuhuma ya kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Nchemba imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya mashahidi wa upande wa mashitaka kushindwa kufika mahakamani.
Hiyo ni mara ya pili mfululizo mashahidi yao kushindwa kufika mahakamani.
Mara ya kwanza mashahidi hao wa upande wa mashitaka kushindwa kufika mahakamani, hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, Flora Ndale aliagiza kuwa juhudi zifanyike kuhakikisha kuwa mashahidi hao wanafika mahakamani bila kukosa waweze kutoa ushahidi wao.
Ndale alisema kitendo cha mashahidi wa upande wa mashitaka kutokufika mahakamani wakati washitakiwa kutoka Dar es Salaam wanafika, ni usumbufu mkubwa kwa washitakiwa, mawakili wao na wasikilizaji.
Kesi hiyo sasa itaendelea kuunguruma Aprili 8 mwaka huu.
Vigogo hao ambao wanatuhumiwa kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Chemba ni Waitara Mwikwabe (37) ofisa sera na utafiti makao makuu na Dk.Kitila Mkumbo mhadhiri wa Chuo.
Source: Mtanzania