Mashahidi wakwamisha kesi ya Andrew Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashahidi wakwamisha kesi ya Andrew Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.  Kesi ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya watu wawili inayomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, imeahirishwa hadi leo kutokana na mashahidi kutofika mahakamani.
  Kesi hiyo ambayo jana mashahidi wawili ambao ni askari upande wa mashitaka, wangetoa ushahidi wao, iliahirishwa mbele ya hakimu Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni baada ya wakili wa Serikali, Richard Rweyongeza, kuiomba mahakama kuiahirisha kutokana na mashahidi hao kutopatikana licha ya kutafutwa kwa njia ya simu.
  Baada ya wakili Rweyongeza kuomba Mahakama ifanye hivyo, naye wakili wa mshtakiwa Saimon Mponda, alipoulizwa alikubaliana na ombi hilo.
  Tayari mashahidi wawili askari wa Usalama Barabarani katika kitengo cha ukaguzi wa magari wa kituo cha polisi Oysterbay, wametoa ushahidi wao kati ya mashahidi 11 ambao wanatarajiwa kutoa ushahidi.
  Chenge anakabiliwa na mashitaka manne ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali, kusababisha vifo vya watu wawili na kuendesha gari bila kuwa na bima.
  Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Pick up Hilux T 512 ACE iliyoigonga bajaj T 736 AXC na kusababisha vifo vya Beatrice Costantine na Vick George.
  Ajali hiyo ilitokea Machi 27, mwaka jana saa 10:30 alfajiri eneo la Masaki shule barabara ya Haile Selassie, jijini Dar es Salaam.
  Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana ya Shilingi milioni moja na anatetewa na wakili wake, Simon Mponda.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...