Mashabiki wa filamu za Harry Potter waomboleza kifo cha Sir Michael Gambon (Professor Dumbledore)

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
potaaa.jpg


Taarifa za kifo cha muigizaji huyu Sir Michae Gamboni maarufu kama Professor Albus Dumbledore kilitangazwa na familia yake jana tar 28/9/2023.

Mwigizaji Sir Michael Gambon amefariki kwa amani hospitalini akiwa na umri wa miaka 82, familia yake ilisema.

Sir Michael alikuwa maarufu kwa mashabiki wa Harry Potter ulimwenguni kote kama Professor Albus Dumbledore, Mkuu wa Shule ya kichawi ya Hogwarts.

Mke pamoja na mtoto wake walisema mpendwa wao alifariki kutokana na maradhi ya Pneumonia.

BBC
 
harry potter cast wengi wamekufa,

dumbledore wa ile movie ya kwanza alikufa

professor snape alikufa

hagrid nae alikufa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom