Mashabiki tugome kuingia viwanjani mechi za timu za taifa

Hadrianus

JF-Expert Member
Feb 19, 2020
1,193
2,000
Wizara ya Michezo na TFF wameshirikiana kutudharau wapenzi wa mpira wa miguu kwa kufanya mambo ya kijinga na kipuuzi kabisa.

Kwanza wamegoma kuweka bayana kwanini mchezo ulisogezwa mbele kwa masaa mawili huku wakijitetea kwa hoja ya kitoto na kipuuzi "tulifanya hivyo kwa nia njema". Hiyo nia njema ni ipi?

Kwanini TFF walikubali sababu za kipuuzi hali iliyosababisha hasara kubwa kwa wapenzi wa kandanda ndani ya nchi na wale waliosafiri kutoka nchi jirani!

Sheria za FIFA zipo wazi, serikali hairuhusiwi kuingilia mambo ya michezo hasa kuingiza siasa za kipumbavu, ilikuaje TFF na bodi ya Ligi ikakubali kusogeza mida mbele kwa sababu zisizo na mashiko?

Wanakuja na taarifa iliyojaa upuuzi eti mechi ipangiwe siku nyingine na waliokata tiketi wataingia kwa tiketi za awali, hivi mtu aliyetumia zaidi ya 150,000/= aliyojichanga kwa miezi kadhaa aanze tena kuhangaika kurudi Dar es Salaam?

Gharama za timu kujiandaa na mchezo huo walipwe pia.

Waziri wa Michezo, Rais wa TFF, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi walitakiwa kujiudhuru haraka sana ile tarehe 09 asubuhi tu.

Nawaomba Simba na Yanga mgome kucheza hiyo mechi kwa namna yoyote ile ili kuwashikisha adabu hao waliotukosea heshima sisi kama mashabiki, hakuna wa kuwafanya chochote. Katika hili SIMBA na YANGA shikamaneni hakuna mechi kuchezwa.

Mashabiki pia tusiende viwanjani kushangilia timu za taifa, waende WIZARA YA MICHEZO, TFF na BODI YA LIGI.

Kauli ya Mixime itaishi milele
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,871
2,000
Wawahi tu kuuza tiketi tena. Mechi itakua nzuri sana no escape again. Kama demu kala hela yako then akawa anarukaruka we kuwa na subira tu ck ataingia 18 ndo iyo sasa.
 
KUCH KUCH

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
1,065
2,000
Wizara ya Michezo na TFF wameshirikiana kutudharau wapenzi wa mpira wa miguu kwa kufanya mambo ya kijinga na kipuuzi kabisa.

Kwanza wamegoma kuweka bayana kwanini mchezo ulisogezwa mbele kwa masaa mawili huku wakijitetea kwa hoja ya kitoto na kipuuzi "tulifanya hivyo kwa nia njema". Hiyo nia njema ni ipi?

Kwanini TFF walikubali sababu za kipuuzi hali iliyosababisha hasara kubwa kwa wapenzi wa kandanda ndani ya nchi na wale waliosafiri kutoka nchi jirani!

Sheria za FIFA zipo wazi, serikali hairuhusiwi kuingilia mambo ya michezo hasa kuingiza siasa za kipumbavu, ilikuaje TFF na bodi ya Ligi ikakubali kusogeza mida mbele kwa sababu zisizo na mashiko?

Wanakuja na taarifa iliyojaa upuuzi eti mechi ipangiwe siku nyingine na waliokata tiketi wataingia kwa tiketi za awali, hivi mtu aliyetumia zaidi ya 150,000/= aliyojichanga kwa miezi kadhaa aanze tena kuhangaika kurudi Dar es Salaam?

Gharama za timu kujiandaa na mchezo huo walipwe pia.

Waziri wa Michezo, Rais wa TFF, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi walitakiwa kujiudhuru haraka sana ile tarehe 09 asubuhi tu.

Nawaomba Simba na Yanga mgome kucheza hiyo mechi kwa namna yoyote ile ili kuwashikisha adabu hao waliotukosea heshima sisi kama mashabiki, hakuna wa kuwafanya chochote. Katika hili SIMBA na YANGA shikamaneni hakuna mechi kuchezwa.

Mashabiki pia tusiende viwanjani kushangilia timu za taifa, waende WIZARA YA MICHEZO, TFF na BODI YA LIGI.

Kauli ya Mixime itaishi milele
Kwenye hilo la serikali kutoingilia mpira hapo ndio UTUMIE AKILI unless chiz ndiye ANAAMINI hvyo
 
Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,431
2,000
Kwani hiyo sababu ingewekwa wazi mngefanya nini nyie Uto.

Mbona game yanu na Biashara Utd haikuwekwa sababu ya kusogezwa mbele?

Upuuzi ni huu wa kukataa kucheza mpira baada ya kusogezwa mbele kwa masaa mawili kisa Kanuni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom