Masha, Mbega mmeiaibisha CCM na taifa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
VITENDO vilivyofanywa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Lawrence Masha na aliyekuwa mbunge wa Iringa Mjini Monica Mbega, ni aibu kwao, kwa familia zao, chama chao na taifa.

Viongozi hao kwa nyakati tofauti waliamua kuondoa baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia kwenye ofisi zao wakati wakiwa wabunge wa maeneo husika.

Hainiingii akilini na sitakubaliana na ushawishi au hoja yoyote ya kumtetea Masha au Monica Mbega, kwa vitendo walivyovifanya kwasababu si vya kistaarabu.

Binafsi naona wamewakosea heshima wananchi wa majimbo yao na wanataka kupeleka ujumbe kuwa madaraka ndiyo kitu cha thamani kwao kuliko kujali masilahi ya umma.

Dhamana ya ubunge aliyopata Masha, ilimfanya ateuliwe kuwa waziri, lakini alichokionyesha juzi kimemuondolea sifa aliyoijenga wakati wa utawala wake.

Mwanzo niliposikia taarifa hizi za kusikitisha za aliyoyafanya Masha nilidhani amesingiziwa, lakini baada ya kuwasikia watendaji na viongozi mbalimbali mkoani humo wakielezea kuhusu hilo nikaziamini na kumtoa thamani.

Ninajiuliza ni Masha yule yule aliyekuwa waziri amefikia mahali pa kukosa ustaarabu na utu hadi kufikia kung’oa vitasa vya ofisi aliyokuwa akiitumia kwa hoja kwamba alivinunua yeye.

Bila kuuma uuma maneno, Masha amewadhalilisha wapiga kura wake, ameidhalilisha familia na pia amekidhalilisha chama cha Mapinduzi (CCM).

Lawrence Masha anapaswa kumuomba msamaha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwa kumdhalilisha kwa kiwango hicho.

Kung’oa vitasa pamoja na kubeba samani zilizokuwemo ndani ya ofisi ya mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa kisingizio chochote hakikubaliki katika jamii iliyostaarabika.

Hilo linathibitisha kuwa Masha hakuwa mbunge wa watu wa Jimbo la Nyamagana, bali alikuwa Mbunge wa maslahi yake na ndio maana hakuwafikiria kwanza wapiga kura wake bali anajiangalia yeye.

Ametuthibitishia kuwa hakukaa pale kuwatumikia wananchi wa eneo hilo bali kutekeleza maisha yake binafsi, hivyo hana cha kukikabidhi kwa mrithi wake
kwa ajili ya wananchi wake.

Anataka kutuarifu kuwa hana mradi wowote wa maendeleo kwa watu wa Nyamagana, ambao angemkabidhi mrithi wake?

Hivi Masha hajui kuwa ofisi ya mbunge, ni mali ya watu wa jimbo hilo, hivyo chochote kilichopo katika ofisi ile hata kama kilinunuliwa na yeye bado kinapaswa kiendelee kutumiwa na mbunge mwingine.

Ukarabati wowote alioufanya bado unabakia ni mali ya wananchi ambao wana haki ya kumchagua mbunge yoyote wanayeona anawafaa kwa wakati husika
Hivi ni kweli Masha haelewi kuwa serikali ya CCM inayoongozwa Rais Kikwete, ndiyo iliyopaswa kununua samani za kuiweka katika ofisi hiyo ya Mbunge wa Nyamagana na nyingine zote nchini.

Hata kama Masha aliikuta haina samani akaamua kununua vya kwake binafsi na kuvike hiyo ilikuwa hisani yake kwa serikali yake na tangu alipofanya hivyo vitu hivyo si mali yake tena.

Kwa hakika kwa hili alilolifanya Masha, amejipambanua kuwa ni mbinafsi anajali zaidi vitu kuliko utu na masilahi ya wananchi wa Nyamagana
Masha bado ni mkazi wa Nyamagana, sasa kuna tatizo gani kwa mali alizozinunua zikatumiwa na mbunge wake kwa maendeleo ya Wananyamagana? Anataka wakazi wenzake wamueleweje kwa kuchukua samani kwenye ofisi ya mbunge?

Mtu anayeshindwa kujua tofauti ya msaada na mkopo, kujua maana ya shukrani kwa anayekutumikia au kutuza, hafai kupewa dhamana yoyote maishani mwake.

Namuonea huruma, Masha kwa kuonyesha picha yake halisi mbele ya Wananyamagana na Watanzania kwa ujumla, je, ndiyo tuseme hatokuja kuwania nafasi yoyote ya uongozi ndani na nje ya jimbo hilo?

Amewathibitishia wananchi wa jimbo hilo walikosea kumchagua mbunge wao, lakini pia amemdhalilisha Rais Kikwete ambaye sasa anaonekana kuwapa madarakani wanasiasa asiowajua tabia zao.

Nimelazimika kumtaka Masha, amuombe radhi Rais Kikwete, kwa kuwa yeye ndiye aliyesimamia vikao vya juu vilivyopitisha jina la Masha kuwania ubunge mwaka 2005 lakini pia ndiye aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa kitendo alichokifanya Masha, dunia imekisikia, kukiona kupitia kwenye vyombo mbalimbali vya habari, kajitia doa na chama chama, nani mwenye uwezo wa kulisafisha doa hili?

Mamilioni ya watu duniani kote, tayari leo hii wanafahamu vema kuwa mmoja wa waliokuwa mawaziri wa JK ametoa mpya kwa kung’oa vitasa na kukomba samani za iliyokuwa ofisi yake akiwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana.

Kutokana na hilo sasa hawamjadili Masha peke yake bali wanamjadili Rais Kikwete, aliyempa dhamana kubwa ya uwaziri, katika kipindi cha miaka mitano yake ya kwanza ya utawala wa nchi hii.

Wanajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu wanaishia kumshushia lawama Rais Kikwete, wengi wanashangazwa na hili wanatamani kuanza kuwachunguza mawaziri mmoja baada ya mwingine.

Wanawachunguza, mawaziri waliopita, pamoja na hawa wapya walioapishwa juzi, wanawaweka wote kwenye kundi moja yanakuwa yale yale ya, “Samaki mmoja akioza Tenga zima limeoza”.

Wanamuweka katika mzani huo pia Rais Jakaya Kikwete, wanaamini kwamba amebariki uharibifu huo uliofanywa na Masha, kwa sababu hawajamsikia akiukemea kama si kulaani.

Umefika wakati viongozi wetu wawe wastaarabu na waweke mbele maslahi ya taifa badala ya masilahi binafsi, kama alivyofanya Masha.

Kuna viongozi ambao walitumia rasilimali za taifa kwa masilahi binafsi, mbona hatujawahi kusikia hata siku moja wakirejesha rasilimali hizo baada ya kuukosa uongozi? Wale waoachukua samani kwa madai walizinunua kwa fedha zao, walizipata wapi kama wananchi wasingekuwa wanalipa kodi?

Kama Masha, alifikiri kuchukua samani hizo ni kumkomoa mbunge wa sasa wa Nyamagana, Ezekiel Wenje wa CHADEMA, amekosea sana kwani amejikomoa mwenyewe na kujiharibia jina alilojijengea wakati wa utawala wake.

Sidhani kama hili litasahaulika haraka, naamini wananchi wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla, wataendelea kulaani kitendo hiki cha kusikitisha kwa muda mrefu ujao.

Mwingine aliyefanya kioja kama hicho ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega, ambaye pia alikuwa mbunge wa Iringa Mjini ambaye inadaiwa amechukua mpaka mapazia yaliyokuwapo kwenye ofisi yake aliyoitumia kwa takriban miaka 10.

Huu ni ukosefu wa shukrani kwa kiasi kisichoelezeka aliowafanyia wananchi wa jimbo la Iringa mjini na amemdhalilisha Rais Jakaya Kikwete, ambaye mara kadhaa alimpa heshima ya kuwa mkuu wa mkoa.

Monica anapaswa kujua kuwa, ofisi hiyo ni mali ya wananchi wa Iringa mjini si ya mbunge wa sasa mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA).

Yeye ni mkazi wa Iringa Mjini hivyo hakuwa na sababu za yeye kufanya hayo aliyoyafanya kwa sababu chochote kitakachofanywa na mbunge wa sasa kwa namna moja au nyingine kitamgusa yeye.

Mbunge wa sasa atalazimika kununua mapazia na samani nyingine, lakini kama vitu hivyo vingekuwapo fedha hizo zingetumika kuboresha huduma nyingine za kijamii.

Viongozi wetu wanapaswa kujenga dhana ya kuwa uongozi ni dhamana, ni mchezo wa kupokezana vijiti hivyo hakuna sababu kuchukia au kuweka kinyongo iwapo wananchi wataamua vinginevyo.

Naona kuna haja kwa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, kumuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, awaeleze wanachama wao wanaoangushwa wasifanye vitendo vya kuchukua samani za ofisi zao ili kudumisha dhana ya demokrasia ya vyama vingi.

Tofauti za itikadi za vyama ziwe chanzo cha kuchochea maendeleo ya wananchi badala ya kuwa chanzo cha kufarakana na kutoshirikiana kwenye shughuli za maendeleo.

Narudia kusema kuwa hiki walichokifanya sasa kinazidi kuwafanya wananchi waamini kuwa asilimia kubwa ya wabunge kutoka CCM wanagombea ubunge kwa dhamira ya kujinufaisha na si kuwatumikia wananchi.

Haiwezekani mwakilishi wa wananchi achukue kitu chenye thamani isiyofika hata sh mil tano, wakati kiti hicho cha ubunge kilimuingizia zaidi ya kiasi hicho kwa mwezi.
 
mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
Hiyo ndiyo ccm! Ulikuwa hujui? kwao kitu kushindwa na mpinzani
wanaona kama janga la kitaifa
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,213
2,000
Na hawatakaa watoe tamko lolote kupinga vitendo hivyo hawa ccm...too mean!
 
engmtolera

Verified Member
Oct 21, 2010
5,150
1,250
ndugu yangu hiyo ndiyo tz yenye viongozi waliojaa visasi na chuki tele moyoni,hao ndio viongozi wanaotaka kilasiku iwe kwao njema kwa wengine maafa,hao ndio viongozi tulionao tz wasio kubali kuwa kuna watu wanaokubalika zaidi yao,hao ndio viongozi tulionao wenye upeo mdogo sana wakufikilia wanapewa madalaka kwa kuwa karibu na viongozi wakuu wa hii nchi

hii ni tz yenye viongozi wasiojali ya wengi zaidi ya wao na familia zao tu,je ile office ni ya masha,mbega ama ni ya umma? lakini kilichotokea as if office ni ya mtu binafsi

na hakika ndugu yangu hakuna hatuwa yeyote itakayochukuliwa juu yao kwani waliowengi wanawaunga mkono kwa kitendo walichofanya

inasikitisha sana tz kupewa viongozi wanaongalia mwisho wa vidole vyao na sio zaidi ya vidole vyao wanaangalia zaidi chini na sio mbele, shame upon them,mungu awasamehe kwa kwa fikra mgando walizo nazo

mapinduziiiii daimaaaaaa
 
Kahinda

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
948
500
VITENDO vilivyofanywa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Lawrence Masha na aliyekuwa mbunge wa Iringa Mjini Monica Mbega, ni aibu kwao, kwa familia zao, chama chao na taifa.

Viongozi hao kwa nyakati tofauti waliamua kuondoa baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia kwenye ofisi zao wakati wakiwa wabunge wa maeneo husika.

Hainiingii akilini na sitakubaliana na ushawishi au hoja yoyote ya kumtetea Masha au Monica Mbega, kwa vitendo walivyovifanya kwasababu si vya kistaarabu.

Binafsi naona wamewakosea heshima wananchi wa majimbo yao na wanataka kupeleka ujumbe kuwa madaraka ndiyo kitu cha thamani kwao kuliko kujali masilahi ya umma.

Dhamana ya ubunge aliyopata Masha, ilimfanya ateuliwe kuwa waziri, lakini alichokionyesha juzi kimemuondolea sifa aliyoijenga wakati wa utawala wake.

Mwanzo niliposikia taarifa hizi za kusikitisha za aliyoyafanya Masha nilidhani amesingiziwa, lakini baada ya kuwasikia watendaji na viongozi mbalimbali mkoani humo wakielezea kuhusu hilo nikaziamini na kumtoa thamani.

Ninajiuliza ni Masha yule yule aliyekuwa waziri amefikia mahali pa kukosa ustaarabu na utu hadi kufikia kung’oa vitasa vya ofisi aliyokuwa akiitumia kwa hoja kwamba alivinunua yeye.

Bila kuuma uuma maneno, Masha amewadhalilisha wapiga kura wake, ameidhalilisha familia na pia amekidhalilisha chama cha Mapinduzi (CCM).

Lawrence Masha anapaswa kumuomba msamaha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwa kumdhalilisha kwa kiwango hicho.

Kung’oa vitasa pamoja na kubeba samani zilizokuwemo ndani ya ofisi ya mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa kisingizio chochote hakikubaliki katika jamii iliyostaarabika.

Hilo linathibitisha kuwa Masha hakuwa mbunge wa watu wa Jimbo la Nyamagana, bali alikuwa Mbunge wa maslahi yake na ndio maana hakuwafikiria kwanza wapiga kura wake bali anajiangalia yeye.

Ametuthibitishia kuwa hakukaa pale kuwatumikia wananchi wa eneo hilo bali kutekeleza maisha yake binafsi, hivyo hana cha kukikabidhi kwa mrithi wake
kwa ajili ya wananchi wake.

Anataka kutuarifu kuwa hana mradi wowote wa maendeleo kwa watu wa Nyamagana, ambao angemkabidhi mrithi wake?

Hivi Masha hajui kuwa ofisi ya mbunge, ni mali ya watu wa jimbo hilo, hivyo chochote kilichopo katika ofisi ile hata kama kilinunuliwa na yeye bado kinapaswa kiendelee kutumiwa na mbunge mwingine.

Ukarabati wowote alioufanya bado unabakia ni mali ya wananchi ambao wana haki ya kumchagua mbunge yoyote wanayeona anawafaa kwa wakati husika
Hivi ni kweli Masha haelewi kuwa serikali ya CCM inayoongozwa Rais Kikwete, ndiyo iliyopaswa kununua samani za kuiweka katika ofisi hiyo ya Mbunge wa Nyamagana na nyingine zote nchini.

Hata kama Masha aliikuta haina samani akaamua kununua vya kwake binafsi na kuvike hiyo ilikuwa hisani yake kwa serikali yake na tangu alipofanya hivyo vitu hivyo si mali yake tena.

Kwa hakika kwa hili alilolifanya Masha, amejipambanua kuwa ni mbinafsi anajali zaidi vitu kuliko utu na masilahi ya wananchi wa Nyamagana
Masha bado ni mkazi wa Nyamagana, sasa kuna tatizo gani kwa mali alizozinunua zikatumiwa na mbunge wake kwa maendeleo ya Wananyamagana? Anataka wakazi wenzake wamueleweje kwa kuchukua samani kwenye ofisi ya mbunge?

Mtu anayeshindwa kujua tofauti ya msaada na mkopo, kujua maana ya shukrani kwa anayekutumikia au kutuza, hafai kupewa dhamana yoyote maishani mwake.

Namuonea huruma, Masha kwa kuonyesha picha yake halisi mbele ya Wananyamagana na Watanzania kwa ujumla, je, ndiyo tuseme hatokuja kuwania nafasi yoyote ya uongozi ndani na nje ya jimbo hilo?

Amewathibitishia wananchi wa jimbo hilo walikosea kumchagua mbunge wao, lakini pia amemdhalilisha Rais Kikwete ambaye sasa anaonekana kuwapa madarakani wanasiasa asiowajua tabia zao.

Nimelazimika kumtaka Masha, amuombe radhi Rais Kikwete, kwa kuwa yeye ndiye aliyesimamia vikao vya juu vilivyopitisha jina la Masha kuwania ubunge mwaka 2005 lakini pia ndiye aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa kitendo alichokifanya Masha, dunia imekisikia, kukiona kupitia kwenye vyombo mbalimbali vya habari, kajitia doa na chama chama, nani mwenye uwezo wa kulisafisha doa hili?

Mamilioni ya watu duniani kote, tayari leo hii wanafahamu vema kuwa mmoja wa waliokuwa mawaziri wa JK ametoa mpya kwa kung’oa vitasa na kukomba samani za iliyokuwa ofisi yake akiwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana.

Kutokana na hilo sasa hawamjadili Masha peke yake bali wanamjadili Rais Kikwete, aliyempa dhamana kubwa ya uwaziri, katika kipindi cha miaka mitano yake ya kwanza ya utawala wa nchi hii.

Wanajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu wanaishia kumshushia lawama Rais Kikwete, wengi wanashangazwa na hili wanatamani kuanza kuwachunguza mawaziri mmoja baada ya mwingine.

Wanawachunguza, mawaziri waliopita, pamoja na hawa wapya walioapishwa juzi, wanawaweka wote kwenye kundi moja yanakuwa yale yale ya, “Samaki mmoja akioza Tenga zima limeoza”.

Wanamuweka katika mzani huo pia Rais Jakaya Kikwete, wanaamini kwamba amebariki uharibifu huo uliofanywa na Masha, kwa sababu hawajamsikia akiukemea kama si kulaani.

Umefika wakati viongozi wetu wawe wastaarabu na waweke mbele maslahi ya taifa badala ya masilahi binafsi, kama alivyofanya Masha.

Kuna viongozi ambao walitumia rasilimali za taifa kwa masilahi binafsi, mbona hatujawahi kusikia hata siku moja wakirejesha rasilimali hizo baada ya kuukosa uongozi? Wale waoachukua samani kwa madai walizinunua kwa fedha zao, walizipata wapi kama wananchi wasingekuwa wanalipa kodi?

Kama Masha, alifikiri kuchukua samani hizo ni kumkomoa mbunge wa sasa wa Nyamagana, Ezekiel Wenje wa CHADEMA, amekosea sana kwani amejikomoa mwenyewe na kujiharibia jina alilojijengea wakati wa utawala wake.

Sidhani kama hili litasahaulika haraka, naamini wananchi wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla, wataendelea kulaani kitendo hiki cha kusikitisha kwa muda mrefu ujao.

Mwingine aliyefanya kioja kama hicho ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega, ambaye pia alikuwa mbunge wa Iringa Mjini ambaye inadaiwa amechukua mpaka mapazia yaliyokuwapo kwenye ofisi yake aliyoitumia kwa takriban miaka 10.

Huu ni ukosefu wa shukrani kwa kiasi kisichoelezeka aliowafanyia wananchi wa jimbo la Iringa mjini na amemdhalilisha Rais Jakaya Kikwete, ambaye mara kadhaa alimpa heshima ya kuwa mkuu wa mkoa.

Monica anapaswa kujua kuwa, ofisi hiyo ni mali ya wananchi wa Iringa mjini si ya mbunge wa sasa mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA).

Yeye ni mkazi wa Iringa Mjini hivyo hakuwa na sababu za yeye kufanya hayo aliyoyafanya kwa sababu chochote kitakachofanywa na mbunge wa sasa kwa namna moja au nyingine kitamgusa yeye.

Mbunge wa sasa atalazimika kununua mapazia na samani nyingine, lakini kama vitu hivyo vingekuwapo fedha hizo zingetumika kuboresha huduma nyingine za kijamii.

Viongozi wetu wanapaswa kujenga dhana ya kuwa uongozi ni dhamana, ni mchezo wa kupokezana vijiti hivyo hakuna sababu kuchukia au kuweka kinyongo iwapo wananchi wataamua vinginevyo.

Naona kuna haja kwa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, kumuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, awaeleze wanachama wao wanaoangushwa wasifanye vitendo vya kuchukua samani za ofisi zao ili kudumisha dhana ya demokrasia ya vyama vingi.

Tofauti za itikadi za vyama ziwe chanzo cha kuchochea maendeleo ya wananchi badala ya kuwa chanzo cha kufarakana na kutoshirikiana kwenye shughuli za maendeleo.

Narudia kusema kuwa hiki walichokifanya sasa kinazidi kuwafanya wananchi waamini kuwa asilimia kubwa ya wabunge kutoka CCM wanagombea ubunge kwa dhamira ya kujinufaisha na si kuwatumikia wananchi.

Haiwezekani mwakilishi wa wananchi achukue kitu chenye thamani isiyofika hata sh mil tano, wakati kiti hicho cha ubunge kilimuingizia zaidi ya kiasi hicho kwa mwezi.

Wakuu labda swali langu ni hili, Furniture hizo ni mali ya nani? je kama alizinunua kwa pesa yake kwa nini asizichukue. Na kama hajazinunua basi ni mwizi kama mtu yeyote anavyo weza kushitakiwa kwa kubomoa nyumba au ofisi ya watu/mtu na kuiba mali zilizomo.

Na kama ndivyo ilivyo kwa nini wahusika wasichukue hatua ya kuwashitaki?badala ya kupiga kelele
magazetini.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,718
2,000
Wakuu labda swali langu ni hili, Furniture hizo ni mali ya nani? je kama alizinunua kwa pesa yake kwa nini asizichukue. Na kama hajazinunua basi ni mwizi kama mtu yeyote anavyo weza kushitakiwa kwa kubomoa nyumba au ofisi ya watu/mtu na kuiba mali zilizomo.

Na kama ndivyo ilivyo kwa nini wahusika wasichukue hatua ya kuwashitaki?badala ya kupiga kelele
magazetini.

Sana sana alinunua kwa kutumia office maintenance allowance; hiyo siyo mali yake binafsi, ni mali ya bunge. Ma kujua hivyo, inabidi a-account matumizi ya allowance ya ofisi aliyokuwa akipewa miaka yote mitano iliyopita.
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,470
2,000
Wakuu labda swali langu ni hili, Furniture hizo ni mali ya nani? je kama alizinunua kwa pesa yake kwa nini asizichukue. Na kama hajazinunua basi ni mwizi kama mtu yeyote anavyo weza kushitakiwa kwa kubomoa nyumba au ofisi ya watu/mtu na kuiba mali zilizomo.

Na kama ndivyo ilivyo kwa nini wahusika wasichukue hatua ya kuwashitaki?badala ya kupiga kelele
magazetini.

Hata kama wahusika walizinunua samani hizo kwa pesa zao binafsi bado si ustaarabu kufanya waliyoyafanya. Hebu mkuu niambie mtu kama Masaha anaenda kufanyia nini kitasa alichong'oa ofisini au kapeti lililotumika???????
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,374
2,000
haya ndiyo matokeo ya kutaka kuwe na wabunge au viongozi vijana.......wakishindwa matokeo yake ndiyo haya.....au hamjawahi ku-anticipate haya...mlitegemea wawe na uvumilivu wa kukosa nafasi wkt wao wanaona wameula na hakuna wa kuwatoa?.......mbaya zaidi ni vijana halafu wanagombea kupitia ccm chama mbofu mbofu............wapeni elimu vijana waliopbaki ili wajua adha ya kukosa nafasi
 
NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,510
1,195
Huyu masha si anajifanya mzungu hovyooooo!
Roho ya kimasikini sana hiyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom