Mimi niliangalia kipindi kile, ijapokuwa nilikuwa na hama hama kati ya TBC1 na EATV, pale mwishoni alipokuwa anafunga kipindi Masanja alitoa maneno yaliyokuwa yanaonyesha hasira yake juu ya EATV na R. Mengi.
Ingawa hakutaja jina, lakini sentensi kama hii ahihitaji mtu kujua sayansi ya kurusha roketi kujua alimaanisha nini, alisema...."watu wana hela lakini wana roho mbaya (huku akionesha ishara ya kukunja kidole) wana hela nyingi lakini hawatosheki......na je kwa nini wameweka muda huu huu......si wangetafuta muda mwingine?" Alafu akaendelea..."najua sasa hivi watazamaji mnaenda kwa jirani ku angalia....lakini sisi ndo wenye vipaji vya ukweli...hatuna hela lakini tuna vipaji...."
Ni wazi alikuwa akiwasema EATV na kipindi chao kipya cha Ze Comedy....ambacho kinarushwa muda sawa sawa na kipindi cha Orijino Komedi cha kina Masanja!!!
Masanja anasahau kwamba EATV walikuwa wanarusha hicho kipindi muda huo huo hapo mwanzo....na ni TBC1 na kina Masanja unaweza ukasema ndo waliiga muda (ambapo kwangu naona sio issue).
Nakumbuka hata kipindi kile Futuhi wa Star TV na Vimbwanga time wa Channel 10 wanaanza, kina Masanja waliwapiga madongo sanaaaa!!
Ninachokiona hapa ni kwamba kina Masanja, Joti na Seki hawajui maana ya soko huria ambapo kila mtu ana uhuru wa kuingina sokoni na kuuza bidhaa au huduma anayoitaka. Katika mfumo huu ni soko tu ndilo litakalomfanya mtu aitoe bidhaa yake sokoni, kwa mfano Vimbwanga time cha Channel 10 walivyoacha kurusha kipindi hicho.
Masanja et al acheni kutukana watu........TV station zenyewe ziko 3 tu hapa nchini sijui mtakimbilia wapi mkitemwa TBC1. Kila mtu atakayetaka kufanya kazi na nyie ataogopa kudhalilishwa siku mtakapo vunja mkataba!!
Naona upeo wenu wa kufikiria ni mdogo sana, nawashauri acheni majungu na visilani.......pigeni kazi, kipindi bora ndicho kitakachoangaliwa na watamaji na si vinginevyo!!
Ni hayo tu!
Kijana nna mashaka na wewe. Unaanza na posti ya kwanza kwa pumba?Kuwa muungwana bisha hodi kwanza ukaribishwe!hodi wenyeji, hodi tena!
Naomba kukaribia kwenye jamvi na kamchango kadogo Huyu mshkaji masanja hakumtaja jina mtu. Mchangiaji kwa fikra zake amemrenga R. Mengi. Ni sawa na maneno ya kwenye khanga mwingine anaweza soma akasema amenivalia mimi je mtengenezaji alijua wewe na huyo mna bifu? ACHA KUJISHUKU NGOMA HUJAPIGIWA WEWE, UNACHEZA.
Ahaa! Kumbe na wewe kiongozi umemtukia? Anaitwa Bandaz! Kule kwetu ukisema Bandaz........! Hehehehe!Nenda kwenye jukwaa la utambulisho kwanza ujitambulishe huko, ndo uanze kuflow
Sioni kama hawa Orijino Comedy wanakwenda vizuri siku hizi. Tangu wametoka EATV wanapiga majungu tu. hata huko kuchekesha hakuna. Nawaona huko mbele hawatakuwa na mwisho mzuri.
Si hilo la juzi tu. hata week kama mbili kabla waliimba wimbo wakimkashifu Mengi, baadhi ya Maneno ya wimbo huo yalikuwa hivi,
".. Ningetoa mali zangu,, kuwalisha masikini,.... kama sinao upendo... mimi si kitu kabisa..."
Sifai Mbele za Bwana.... Sifai Mbele za Bwana,,, kama sinao Upendo Mimi si kitu kabisa,,,,
huku Masanja akiongezea baadhi ya maneno kama "na vilema na viwete". Akimaanisha Mengi analisha Maskini, Vilema Na Viwete wakati hana upendo.
Lets wait and see mwisho wa haya yote.
be cool men hayo mambo ya kutiana adabu ni mambo ya komedi zote duniani. Uharibifu wa utandawazi yep no ukweli wa mambo yes kabisaaaa lakini nanbi anamjua Mengi kisawasawa. kisha kwanini watu wanakuwa pissed off very izi. kama kucharazwa mtu kalamu si unakaa na domo lililojaa hasira na matrusi yalifungwa zip. Hii dunia huru bana kwe kwe kwe kumbe huuma ehe eheJana kama kuna mtu alipata kutazama kipindi cha Orijino Komedi, basi lazima angepatwa na jazba nyingi, hasa katika sehemu ya umalizaji wake.
Masanja katika hali ya kuonyesha kukerwa na kuanza kwa kipindi-pinzani cha EATV cha kusaka wachekeshaji, basi alitoa kauli 2 chafu zote zikimlenga R.MENGI, kama hivi:
i-Mtu anajifanya tajiri na ana hela, sijui kwanini anachanganyikiwa na mambo madogo kama haya!
ii-Nilitegemea UMRI wake (Mengi) ungeendana na mambo yake, lakini kumbe wapi, ndo hivyo tena!
Binafsi niliboreka sana na maneno hayo, si kwamba nampenda sana Reginald, lakini kumkashifu mtu kama yule aliyemzidi umri mno ni kinyume cha maadili kabisa!
Hana adabu kabisa Masanja, *+$%%*inkoskaz huyu!😡....
Sio masanja tu, bali pamoja na washirika na washabiki wake wote IQ zao ni finyu sana.
kwani hawa wameajiriwa na nani? hebu kwanza tutazame data zetu vizuri. Wameajiriwa na nani? wana kampuni yao hawa walichofanya wameingia mkataba na TBC .Sasa nani hasa ana matatizo? Mbona tunafurahia sana methali ya kiswahili samaki mmoja akioza katika tenga wote wameoza. Msitie kabali isiyopimwa katika mizani unaweza kuwa unajaribu kumtemu papa na ndoana ya tuna. UtachekeshaWenye shida siyo kina Masanja bana,hao ni nyasi tu kwenye bonde la mpunga mwenye maamuzi ni mkulima kupalilia nyasi na kuacha mpunga au kupalilia mpunga na kuacha nyasi. Hivyo basi hata mwajiri wao pia ana matatizo makubwa katika jamii.Kama Utawala wa sheria ni kutupiana madongo kwenye chombo cha umma kwa kuuchafua umma unatarajia nini???
Mjadala haujahitimishwa hata kidogo. Unaposema watu wanakosa shukurani unamaana gani.Yaani kwa kuwa hawa CCM (enzi hizo Tanu) imeleta uhuru basi wao waendelee kuwapo tu hata kama wanaboronga? kila mtu anastahili kufanyakazi zake nashukurani si ya kusubiriwa.Hivi mnajua hasa dhuluma maana yake nini?kukosa shukurani si dhuluma bali kuomba upewe shukurani kwa kosa lililohitimisha dharuba ya mwisho katika ncha ya sindano ndio dhuluma yenyewe.Mwenye masikio huambiwa asikie na mwenye macho aambiwa aone na ambaye hana macho lazima atembee afungue hisia namba sita au la kama ni mchonga vinyago kipofu kupapasa kunaweza kukuletea jibu zuri.Acheni hizo hakuna anayemjua mengi vizuri zaidi kama aliyeshawahi kuingia mkataba naye.Sisi kwetu vicheko na zaburi tu, kila kitu kityalipwa hapa hapa.Unadhani kesi za wafanyakazi wale wanahangaika ni za bure tchao mwenye hasira aropoke mpaka nyongoKiongozi umeona senksi niliyokukabidhi kwa hii yuzifuli posti?
You have said it. You have said it well.
Nadhani mjadala umeuhitimisha vizuri.
Kwamba The Orijino komedy Hawana adabu, waoga na hawana shukrani: Period!
you should 1st know what is the so called COMEDY?? na madhumuni yake.....Jana kama kuna mtu alipata kutazama kipindi cha Orijino Komedi, basi lazima angepatwa na jazba nyingi, hasa katika sehemu ya umalizaji wake.
Masanja katika hali ya kuonyesha kukerwa na kuanza kwa kipindi-pinzani cha EATV cha kusaka wachekeshaji, basi alitoa kauli 2 chafu zote zikimlenga R.MENGI, kama hivi:
i-Mtu anajifanya tajiri na ana hela, sijui kwanini anachanganyikiwa na mambo madogo kama haya!
ii-Nilitegemea UMRI wake (Mengi) ungeendana na mambo yake, lakini kumbe wapi, ndo hivyo tena!
Binafsi niliboreka sana na maneno hayo, si kwamba nampenda sana Reginald, lakini kumkashifu mtu kama yule aliyemzidi umri mno ni kinyume cha maadili kabisa!
Hana adabu kabisa Masanja, *+$%%*inkoskaz huyu!😡....
Nilitazama hicho kipindi tangu mwanzo hadi mwisho sikusikia jina la Mengi likitajwa.