Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,297
- 18,047
Achana na Yamoto Band, Twanga Pepeta nk. Habari ya mjini sasa ni MaSaMa Band. Imeanzishwa tarehe 5 November 2015. Wamiliki wa band hii ni watanzania wote. Wakati wa kuanzishwa kwake, karibia asilimia 40 walikuwa na wasiwasi. Wao walitaka kiongozi wake awe yule jamaa ambaye amepigania sana kuwa kiongozi wa band kiasi cha kuhama kwenye kikundi ili mradi apate uongozi wa band.
MaSaMa band ilianza na single moja waliyoiita M. Wakati huo ikiwa na viongozi wawili tu. Yaani Ma na Sa. Single hiyo si haba imehamasisha watu waliokuwa wanalala chini kulala vitandani. Vitanda vimekuwa vingi na sasa si ajabu kukuta paka nao wanajinafasi kwenye vitanda hivyo.
Baada ya kukamilisha safu ya uongozi , wametoa single nyingine. Inatamba kwenye vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi kwa sasa. Single inaitwa Tafadhali Rudi Afrika au kwa kifupi TRA.
Kwenye mafanikio hakukosi wenye wivu. Tayari wadaku wanadai hii inakwenda haraka sana labda nyimbo zake zitachuja haraka. Lakini wasikilizaji wengi huwambii kitu kwa band hii. Hata waliositasita mwanzoni wameanza kidogo kidogo kuikubali. Kuna jamaa mmoja anaitwa SaaEight. Anaikandia kweli band hii. Eti ina visasi kwa band za zamani.
Msije mkachanganya jina la band na promoter wa muziki wa injili. Hii MaSaMa ni Magufuli, Samia na Majaliwa.