Masalia (PM7) wakalia kuti kavu ndani ya CHADEMA...

Masalia (PM7) wakalia kuti kavu ndani ya CHADEMA...

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2007
Posts
869
Reaction score
239
Wengi tulishuhidia vitimbi, matusi, kashfa, uzushi, tuhuma na kila aina ya vituko vya kufunga mwaka vilivyotoka kwa vijana wa CHADEMA ikiwa ni ishara ya kuuwaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013.

Tuhuma nyingi zilirushwa, ninaziita tuhuma kwani hakuna hata mmoja aliyeweza kuthibitisha kwa pande zote kuitwa na kila upande kutoa utetezi na mwingine kutoa thuhuma na watu wasio na upande na wenye taalama ya sheria, maamuzi, busara, hekima na subira kusikiliza na kusema nani mweli na nani mzushi.

Tetesi zilikuwa ni kwamba kamati kuu ya CHADEMA ingekaa ili kuweka mambo sawa pamoja na mambo mengine kuwaita wote walitajwa na kutoa tuhuma mbele ya CC na hatimaye kamati ya maadili ya chama.

Nikiwa mwanachama wa chadema ninaamini kwenye ukweli na kuto kutoa tuhuma za uongo dhidi ya viongozi na wanachama wenzako na mwananchi yeyote yule ukiwa unajua wazi ni uongo. Vile vile ukweli ni tunda la utawala wa sheria na ustawi wa chama. Mhujumu ni hatari sana na msaliti hafai kabisa ndani ya chadema kwani leo atasaliti chama kesho serikali ya chadema na keshokutwa wananchi.

Tuhuma zinazowaandama viongozi wote wa serikali ya CCM na kuendelea kuwaachiwa huru ni matokeao ya kuleana na kulea kujuana, hujuma na kuogopana. Ninaamini kabisa mimi na wengi kuwa chadema leo ni baada ya kuamini sitaona tena yanayosikitisha moyo wangu. Binadamu sio malaika ila tunahitaji kuona ni vipi wema wanazawadiwa kwa wema na wabaya wanaadhibiwa kwa ubaya na wachafu wanatoswa na waliochafuliwa wanatakaswa na wenye mapenzi mema na watetezi wa chama wanaenziwa.

Tuhuma za Masalia, PM7 and na kundi lake zikiachwa hivi hivi nitashtuka sana. Moja nategemea wote waliotuhumiwa wawe mstari wa mbele kudai chama kuitisha CC ili kusafishwa haraka iwezekanavyo. Mbili wale wote wenye ukweli kukilazimisha chama kupokea ushahidi wao, tatu wale wote tulioathirika na tuhuma hizi kwa kuachwa njia panda tunataka majibu kutoka CC na vikao halali vya chama kuhusu viongozi wote waliohusika na makundi haya kama kweli yalikuwepo tuwaone vipi.

Kukaa kimya kwa vikao vya maadili, CC, na maamuzi vya chama vinatuachia sisi wanachama wasi wasi mkubwa sana wa nani tumwamini.

Makamu mwenyekiti wa BAVICHA amerusha makombora mengi sana kwa katibu mkuu wa chama yenye lugha dhalilishi na za kihuni. Siwezi kumwona kama kiongozi makini kichama.

ZZK amehusishwa na makundi yote ya kukivuruga chama, na yeye akaja na lugha za ajabu badala ya kukanusha tuhuma.

Hawa wote ni viongozi wangu ninawaheshimu sana na ninathamini sana mchango wao ndani na nje ya chama.

Ila ikumbukwe kama kweli kuna hata mmoja amehusika kuingamiza CHADEMA lazima awe wakwanza kuachwa aende alikokuwa anataka kwenda baada ya kazi ya kuiwa CHADEMA kama angefanikiwa.

Uwepo wa watu makini ni mwendelezo wa watu makini kujua watu na viongozi makini siku zote za maosha yao. Kuna wakati lulu inaunguza inabidi uiache iende uokote almasi.

Nina amini kwenye sheria na haki, unakuwa mtuhumiwa mpaka utakapohukumiwa.

Naomba sana kama tunavyoshinikiza bunge, na watawala kujitakasa au kutoswa kwa tuhuma mbali mbali kikombe kile kile tukitumiacho kitumike sasa. Nategemea kusikia kila mmoja akishinikiza chama kufanya uchunguzi kwa aliyotuhumiwa nayo na aseme akibainika afanyweje na asipobainika mtoa tuhuma tutamchukulia hatua kali kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA.

----------
UPDATE
----------
Tetesi za sasa zinaonyesha kuwa hatma ya 'Masalia' ndani ya CHADEMA itafahamika kesho (Jan 07, 2013) baada ya Press Conference. Tetesi zinazidi kudokeza kuwa 'Masalia' hao sasa wamekalia kuti kavu!
 
kuna tetes kuwa Juliana Shonza, Mchange na Mwampamba wamevuliwa uanachama na kikao cha BAVICHA
 
Me pia nataka wale wote waliojihusisha na kukihujumu chama na wenyewe watuambie wamefanywa nini kila mtu ale adhabu yake....wale wote walioingia humu kuja kutoa siri za chama na kumponda Dr Slaa na kutaka kuwagombanisha na Mbowe,

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Swali la kujiuliza BAVICHA wanaweza kumvua mtu uanachama wake?
Mleta uzi kikao hicho kilikaa lini ?
 
Nina mashaka..na mleta uzi..bavicha wanaweza wavua uanachama wakina shonza?? Sidhani...kajipange uje na taarifa kamili
 
your very gd but i want to asure you tht no one is safe until now they have left for good let them go and work with CCM then we shall see
 
Taarifa nilizozipata hivi punde toka kwa baadhi ya wafuasi wa PM7 zinasema Habibu Mchange, Mtela Mwampamba na Juliana Shonza wamevuliwa uanachama!.. Natafuta namna ya kubalance habari hii toka kwa viongozi wengine!...
 
Eeeh Aksante Allah subhbna u.wataalah asa km tetesi izi ni za kweli
 
kama kweli CHADEMA wakoserious na kujenga chama,heri kubaki na wanachama wachache kuliko kua na wanachama wengi ambao ni wasaliti na vibaraka wa CCM.
 
kama kweli CHADEMA wakoserious na kujenga chama,heri kubaki na wanachama wachache kuliko kua na wanachama wengi ambao ni wasaliti na vibaraka wa CCM.
Silaa mwenye Kadi ya CCM
 
Taarifa nilizozipata hivi punde toka kwa baadhi ya wafuasi wa PM7 zinasema Habibu Mchange, Mtela Mwampamba na Juliana Shonza wamevuliwa uanachama!.. Natafuta namna ya kubalance habari hii toka kwa viongozi wengine!...
Umesikia vibaya ukweli ni kwamba Heche kawapigia Magoti na kuwaomba wacjitoe Chadema kwani wakifanya hivyo Chadema itapata anguko kuu katika mikoa ya Pwani, Mbeya, Kigoma, Tanga na Sukuma Land mwanza na Shinyanga ambako vijana hao wanakubalika sana
 
Ni kweli wamevuliwa uanachama! Hii imekaa vizuri!
 
Nani ana jeuri ya kuwaondoa PM7 wakiongozwa na Cobraa a.k.a BEN

I can imagine the impatience, the emotions, frustration,Desperation but please just relax!

Unapoandika vitu ambavyo muda mfupi ujao vitaonekana uongo hautaeleweka.Tusubiri press conference kuhusu maamuzi na Maazimio,Hii provocation lengo lake unataka ili nitamke chochote niwe nimetoa siri za vikao.sitamki na nakushauri uache upotoshaji,tulieni!



Stop being Desperate!
 
Acha majungu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom