Masaburi aombewa Kibali na FA

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
CHAMA cha Mpira wa Miguu Uingereza (FA) kimetuma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) mchezaji Douglas Didas Masaburi ili ajiunge na klabu ya nchini humo. Masaburi mwenye umri wa miaka 21 anaombewa ITC ili ajiunge na klabu ya Coventry Spartans akiwa mchezaji wa ridhaa. Coventry Spartans iko katika Ligi Daraja la Pili ya Midland. Mchezaji huyo anaombewa ITC kutoka katika klabu ya New Rule Power. TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika.
 
Hii ni habari ya kisiasa? au ya kimichezo? na inafaida gani hapa? tuzingatie maelezo ya Jamii Forum tuwe waaminifu wa hii forum yetu sababu sisi ndio tunayoitangaza na kuifanya kwa ya manufaa...
 
Nakuunga mkono, Ila nadhani mwenzetu alidhani ni Masaburi wa UDA etc!!!

Any way kwa kuwa hatuwezi kuifuta ni habari njema, na ki nchi inatuunganisha kisiasa pia hasa ukizingatia michezo kwa Tanzania imejaa siasa zaidi (maana nilisafiri kwenye ndege na mchezo mmoja wa kigeni (jina kapuni akanidokeza hivyo pia) Lakini nina swali kwamba awali niliwahi kusikia kwamba mpaka mchezji ukubalike Uingereza ni lazima nchi yako iwe kwenye viwango vya Ubora katika FIFA
 
Kweli nilidhani ni yule wa "wana bayankata" UDA,lakini kumbe ni mtoto wake bwana................!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom