Mlachake
JF-Expert Member
- Oct 13, 2009
- 4,472
- 4,721
Muda huu nimepata Breaking news kuwa kuna Lori Moja linalosafirisha abiria kuwapeleka mnadani limepata ajali na watu wasiopunguo wanne wamepoteza maisha maeneo ya pawaga mkoani Iringa.
kama kumbukumbu zangu ziko vizuri, Miaka ya hivi karibuni kuna ajali kama hii ilitokea mkoani Tanga ambapo wanafunzi walipoteza maisha kwenye ajali ya Fuso.
Kwasababu Tanzania hii Mpaka jambo litokee ndio ichukuliwe tahadhari, Serikali ilipiga marufuku usafirishaji wa abiria kwa kutumia malori.
Sheria za trafic ziko wazi kabisa. Gari linaloruhusiwa ni ambalo limesajiliwa kwaajili ya kubeba abiria tu. yaani PSV.
Ninachojiuliza hasa, Ni kwanini jeshi letu la polisi limekua likifumbia Macho hii tabia ya Malori kubeba zaidi ya Abiria 50 kwenda minadani? nimetembea mikoa ya Iringa, Mbeya na Mara. na mikoa yote hii, tabia hii imeshamiri sana.
Tunaomba serikali Muliangalie hili. Muangalie Jinsi ya kunusuru maisha ya wafanya biashara hawa. najua wanapanda haya malori kwa kukosa njia Mbadala.
Au mnaona hii sheria inakibana Chama tawala katika kupeleka wanachama kwenye mikutano?