Marufuku mabango ya waganga wa Kienyeji

Marufuku mabango ya waganga wa Kienyeji

kuna siku nkiwa na mtoto wa sista wangu anaesoma darasa la kwanza kwa ile hamu ya kujua kusoma. Basi njian akasoma tangazo la nguvu za kiume;
akaniuliza uncle hivi NGUVU ZA KIUME ndio ugonjwa gani mbona njiani naona matangazo mengi sana.!??
imagine ungemjbu vp.

Nyie ndio wale mnaobaka watoto wa dada zenu halafu mnawanunulia pipi kuwanyamazisha.

Huyo mtoto asingekuuliza hivyo km we ni muungwana.
Mbaya sana we mnyonga viuno.
 
Uwingi wa mabango ni kielelezo cha uwingi wa wananchi wajinga na wamekuwa wakomavu na sasa wapu.mbavu.Eti unataka kunenepesha uume kwani unataka kushindana na punda?
 
Mkuu ndenga, kama kuna maigizo ni viongozi wa nchi hii, sheria na taratibu za ku control waganga wa jadi hazija tungwa jana ni kwamba zipo. Kichekesho leo nawaona kwenye tv wako busy waki ng'oa mabango hayo, chakusikitisha wanatoa mabango badala ya kuwakamata wenye mabango ili hali jamaa wanajulikana vizuri tu, mpaka namba za simu wameiwekea hiyo mijamaa inayo paswa kusimamia sheria. Kweli bongo tuna kazi, wasimamia sheria wapo busy idodomia wanatutungia katiba mpya sijua ni mpya au ndio marekebisho ya katiba ya mwaka 2014 helo helo ni cheke mieeee, poa bana jitungieni katiba ya kutuongoza siye wavuja jasho, bongo lala sie tupo tuta wapa ndioooo ipitee kubwa kwenye box la kula za maoni, sina sisi mtatupa posho siku hiyo maana kushinda kwenye foleni hadi jiooni si mchezo walau posho ya siku moja tu, napita mie.
 
Unakauta bango la mganga Wa kienyeji limebandikwa sehemu na kutangaza yafuatayo:mganga Wa wajadi kutoka .........anashugulika na:

1.kupata kazi
2.kupanda cheo kazini
3.fedha za majini!
4.kumvuta mtu Wa mbali
5.mapenzi
6.biashara
7.kufaulu mtihani


Sasa huwa najiuliza hivi mtu akipanda cheo kazini kwa kutumia ushirikina utendaji kazi wake utakuwaje?

Kama mtu anafaulu mtihani kwa mguvu za Giza utendaji kazi wake unakuwaje?
Mabango haya si tu yanadhalisha watu na nchi yetu maana kama mataifa mengine wangeweza kuelewa lugha hii ya kiswahili wangesema taifa hili ni washirikina na maendeleo yao yanategemea madawa ya kienyeji na si uelewa wao Wa darasani!! Wanapeana madaraka kwa kutumia nguvu za Giza!! Darasani wanafaulu kwa kutumia nguvu za giza! Kwa hiyo wangeweza kutuogopa sana kuwa watu hawa ni hatari sana!!Sasa kama tunakubari mabango haya yawepo kila mahali kwa nini tunasikitika tunaposikia vikongwe wameuawa kwa imani za kishirikina? Kwa nini tunalalamika tunaposikia albino kauawa au kakatwa viungo vya mwilini mwake!!!kwa nini tunalalamikia utendaji kazi Wa badhi ya watumishi Wa umma ilhali tunajua kuwa huyu alipandishwa cheo au alipata kazi kwa kutumia Nguvu za giza?

Tujadili kwa Amani
 
Back
Top Bottom