Marufuku mabango ya waganga wa Kienyeji

Marufuku mabango ya waganga wa Kienyeji

ndenga

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
1,887
Reaction score
1,554
Jana wakati nafuatilia Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii waziri alikemea na kupiga marufuku mabango yote ya waganga wa kienyeji. Hiki kitendo kinakera sana. Maamuzi haya yamekuja kwa wakati muafaka baada ya kuzagaa kwa mabango mengi sana hasa katika jiji la Dar es Salaam. Hii imekuwa ni kero sana na aibu kwa Watanzania. Tena wengine wakitaja kutibu magonjwa mpaka ya kunenepesha sijui nini, kupata wachumba, kumrudisha aliyekuacha etc.

Note: Watendaji wote wa serikali za mitaa tunaomba utekelezaji wa hili agizo la waziri..tuanzie na Makumbusho na Kijitonyama
 
Biashara matangazo. Hua tunakwenda kwa waganga wa kienyeji kwa sababu kwenye hospitali zenu tunazungushwa mno. mfano kwa mlalahoi wa Tandika kupata hudma pale MOI ni sawa na paka kusoma gazeti la kihindi
 
tz raha sana ni maneno tu hakuna utekelezaji
 
now they are coming
 
Biashara matangazo. Hua tunakwenda kwa waganga wa kienyeji kwa sababu kwenye hospitali zenu tunazungushwa mno. mfano kwa mlalahoi wa Tandika kupata hudma pale MOI ni sawa na paka kusoma gazeti la kihindi

We mbishi mbishi sana.
 
weka picha

You mean picha ya mganga wa kienyeji au picha ya Waziri husika coz kama ni Mabango yapo mengi sana aanzia Ubungo mpaka Kimara utaniambia umeona mangapi..
 
Manispaa zote inabidi zifuatilie hii issue kwa ukaribu na kwa uharaka..
 
We mbishi mbishi sana.

Mh. ndugu yangu mkuu kaka roughrider. Umeshawahi kuona vijana wa bodaboda wanavyo kua treated pale Muhimbili ?? Nyie wakubwa mnaita MNH. PAALE mgonjwa wa ajali anaambiwa alipe ile laki mbili ya serikali halafu atoe laki tano afanyiwe operation. bila hiyo laki tano rushwa unaambiwa usubiri foleni yako. mkuu watu wameoza pale. pananuka pale wodi ya majeruhi zaidi ya mochwari ya hospitali ya Bombo Tanga. Najua wewe huyajui hayo. si unatembelea Evogue na kutibiwa India .
 
kama kweli wapo serious watumie mgambo wa jiji kuyang'oa kama wanavyoutumia kuwapora wamachinga. otherwise wanazuga tu, ama wanaogopa kurogwa tehetheteh:smile-big::smile-big::smile-big:
 
Kweli wanakera sn cha ajabu kwan kla mganga anakuja na sera zle za nguvu za kiume, kumvuta mpenzi, kusafisha nyota nk. Wizi mtupu
 
You mean picha ya mganga wa kienyeji au picha ya Waziri husika coz kama ni Mabango yapo mengi sana aanzia Ubungo mpaka Kimara utaniambia umeona mangapi..

ndio naomba picha kwani kila alieko jf yupo dar
 
Agizo hili liwekwe kwenye waraka na kutumwa katika halmashauri ili lifanyiwe kazi otherwise ni maneno matupu yasiovunja mfupa
 
Back
Top Bottom