Marufuku kuwakarimu wakaguzi hesabu - CAG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marufuku kuwakarimu wakaguzi hesabu - CAG

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  Marufuku kuwakarimu wakaguzi hesabu - CAG  na Deogratius Temba
  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amewataka wananchi kutowakarimu kwa namna yoyote wakaguzi wa hesabu za serikali wanapofika katika maeneo yao hasa ya vijijini kukagua hesabu.

  Akizungumza katika kipindi cha ‘Tuambie’ kinachorushwa na Televisheni ya TBC1, Utouh alisema wananchi hawaruhusiwi kuwakarimu malazi, chakula wala kitu kingine chochote wakaguzi kwani ofisi yake inawagharamia mahitaji yote muhimu kwa kiasi cha kuwatosha.

  “Ninatangaza tena na wananchi wote wanisikilize, hawa wakaguzi hawana ruhusu ya kupokea kitu chochote kutoka kwa wale wanaowakagua au wananchi, ninawapa mahitaji yao yote ya msingi na hawatakiwi kupewa fedha na mtu mwingine,” alisema Utouh.

  Alisema atafuatilia kwa siri na akibaini kama kuna wakaguzi wanaofanya hivyo atawashughulikia kwani ni kinyume cha sheria za maadili ya ukaguzi.

  Akizungumzia suala la kukithiri kwa uchafu katika miji mingi nchini, alisema kuna wasiwasi kuwa baadhi ya zabuni za kufanya usafi au kukusanya taka chafu mjini hazizingatii vigezo stahiki.

  Alisema zabuni hizo ni tatizo, kwani vikundi vingi au makandarasi wanaopewa hawana uwezo wa kufanya kazi hizo.
   
 2. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dah sasa kumbe walikuwa wanakirimiwa hii kali inawezekana wakawa wanacheza hapa na pale sio
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  huyu baba nae

  wapi ameona mchungaji anarudisha sadaka kanisani??
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...