Marufuku kukamata wamachinga Dar!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marufuku kukamata wamachinga Dar!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Dec 15, 2010.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GrEaTtHinkers,
  Mkoani umeme wenyewe wa shida,kila kitu kiko ubungo
  vijijini hata bodaboda 97% haziwezi kufika-hamna barabara nzuri
  Mawilayani watu ni maskini, hakuna biashara kule mafisadi wamekeza Dsm
  Mtoto wangu nikitaka asome shule yenye walimu wazuri sana ni mpaka dsm
  Kule mikoani hata tuition hamna, mitihani yote inavuja hapa Dsm
  Nani akae huko kubaya aendelee kuimba wimba wa kilimo ni uti wa mgongo ili afaidike nani?

  Nasema vijana wanaojaa dsm wanazo sababu za msingi kuingia jijini,
  Tena msiwakamate kabisa maana wazazi wao wanavaa kaniki, Dar hata mitumba bado ipo manzese.
  Nani aliwatuma kila kitu kiwe dar, hata hospitali kuu ni Dar nani ake Longido?
  kila kitu Dar, Hata FLYOVERS ni dar sasa mnataka tufe bila kupiga picha karibu na daraja zuri.
  Eti nibaki Chunya wakati nataka kumuona Nsajigwa uwanja wa taifa, kule hata plan hamna

  Nasema staki kuskia vujana wananyanyasika waacheni wamanchinga wakae Dar Es Salaam.:A S 114:
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni mipango inayopangwa watu wakiwa wamejifungia magogoni.

  Mipango inapangwa kwa kutekeleza makusudi ya kisiasa na sio mahitaji na misingi ya upangaji wa miji. Ninaamini ukiuliza wanaotengeneza mipango ya mji wa Dsm ni approach ipi hasa wanatumia katika kuuweka mji wa Dar vizuri wanaweza kukuona kibwengo japo wana makaratasi yenye mipango mingi na mizuri iliyoibiwa kutoka Munich.

  Kila ukiamka na kila mpango unaotajwa utasikia Dar na matokeo yake hakuna uendelezaji wa maeneo ya karibu ili kufyonza watu wasikimbilie Dsm.

  Katika kupanga ni lazima kuwe na mikoa ambayo kimkakati itachukua sifa kama za Dsm ili kuzuia wengin kukimbilia jiji hilo moja. Utekelezaji wake ni mgumu lakini ni lazima nchi hii ifike mahali ikubali, kwamba, kujenga fly-overs peke yake na viwanja vikubwa vi-4 va mpira wa miguu na machinga-complex 100 Dar sio njia ya kukabiliana na tataizo la msongamano uliopo.

  Swala ni kugawa virasilimali hivi katika maeneo anuai ili kufanya channel of flow ya watu kuwa katika maeneo mengi na sio Dsm peke yake

  Lazima itakuwa ni kubuni mpango wa kudhani unaendeleza Dar na kukabiliana na changamoto zilizopo kumbe ndo una-duplicate tatizo
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Nani akakae Kibondo au Namanyere Rukwa.
  Tutabanana hapa hapa wote tukiimba wimbo wa Kilimo Kwanza.:A S-omg:
   
 4. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Watoto wa mafisadi wakifika kijijini Jembe wanalishangaa,
  Watoto wa mafisadi wakifika vijijini utadhani watalii, hawaamini jinsi watu walivyo maskini.
  Nani awe kibaraka wenu, waacheni kabisa hao wamachinga.
  wanayo sababu ya kuingia jijini.:whoo:
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  serikali ya awamu hii imo inajipanga mambo yatakuwa mazuri
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ahadi za miradi ya maendeleo zenye dhamani ya shilingi trilioni 90 walizo ahidiwa watanzania ipo yoyote utekelezaji wake umeanza?
   
Loading...