Marubani Watwangana Ngumi Mbele ya Abiria

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Shirika la ndege la India, Air India linachunguza tuhuma za marubani wake wawili na mfanyakazi mwanamke wa ndani ya ndege kurushiana makonde mbele ya abiria ambao walibaki wameduwaa hawaamini macho yao.

Gazeti la The Times la India liliripoti kwamba marubani hao na mwanamke huyo walirushiana ngumi huku wakitukanana mbele ya abiria 100 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wakati huo ndege hiyo ikiwa angani zaidi ya futi 30,000 toka ardhini.

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Sharjah, falme za kiarabu kuelekea Delhi, India.

Ugomvi huo ulianza baada ya mwanamke huyo kuingia chumba cha marubani na kutoka akiwalaumu marubani hao kwamba wamemnyanyasa kijinsia.

Marubani hao kwa hasira waliiacha ndege hiyo ijiongoze yenyewe na kumfuata mfanyakazi mwenzao huyo wa kike na kuanza kumchangia kwa kumshushia kipigo mbele ya abiria.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, mwanamke huyo naye alijibu mapigo kwa kurushiana ngumi na marubani hao.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 pamoja na rubani msaidizi wote walipata majeraha katika kasheshe hilo.

Mmoja wa marubani wa ndege hiyo aina ya Airbus A-320 alitishia kuigeuza ndege hiyo na kuipeleka Pakistan badala ya India.

Polisi wa India wamewafungulia kesi marubani hao wawili kwa kumpiga hadharani mwanamke.

Taarifa iliyotolewa baadae na shirika hilo la ndege ilisema kwamba imeamua kuwasimamisha kazi marubani hao na wafanyakazi wengine wawili wa ndani ya ndege hiyo.
 
Back
Top Bottom