Mr. Purpose
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 1,476
- 2,796
Hongera sana mkuu. Vp tunaweza pata experience yako kidogo mkuu na vijana wajifunze kitu kuhusu hiyo kitu
Mkuu hii kitu nina kovu lake kichwani hadi leo. Anza nayo taratibu kisha spidi na nguvu katika kuizungusha ongeza kadiri uwezo unavyokuwa. Usiikatie tamaa. You tube na vitabu vipo kibao maana najua ilivyo nadra kumpata au hata kumtambua anayeweza haya mambo, wapo ila mtaani tunajificha.Aise niliwahi kujipiga nayo kisogoni hii kitu, na mpaka sasa sijapata mwalimu sahihi wote huwa zinatupiga hizi jamaa.
Kwa hiyo na wewe mkuu ulijifunzia vitabu tu?Mkuu hii kitu nina kovu lake kichwani hadi leo. Anza nayo taratibu kisha spidi na nguvu katika kuizungusha ongeza kadiri uwezo unavyokuwa. Usiikatie tamaa. You tube na vitabu vipo kibao maana najua ilivyo nadra kumpata au hata kumtambua anayeweza haya mambo, wapo ila mtaani tunajificha.
Ahsante..kwa kuanzia kuna mizunguko ya msingi saba,hapa namaanisha namna ya urushaji wa hiyo silaha na mizunguko hii ili upate mirusho sahihi lazima uizungushe kwenye mikono au mwilini/mgongoni. Ndio maana mnalalamika hapo kwa kupata makovu, jambo la msingi ni kuanza polepole na spidi utaipata tu vile ukianza kuzoe.Hongera sana mkuu. Vp tunaweza pata experience yako kidogo mkuu na vijana wajifunze kitu kuhusu hiyo kitu
Umenena vema boss. Muonekano unabadilika na ukiwa mzoefu ni rahisi sana kuwatambua wanoielewa hii michezo. Jambo la kumshukuru Mungu kadiri unavyozoea na kuelewa sana haya mambo unajikuta mpole sana.Ahsante..kwa kuanzia kuna mizunguko ya msingi saba,hapa namaanisha namna ya urushaji wa hiyo silaha na mizunguko hii ili upate mirusho sahihi lazima uizungushe kwenye mikono au mwilini/mgongoni. Ndio maana mnalalamika hapo kwa kupata makovu, jambo la msingi ni kuanza polepole na spidi utaipata tu vile ukianza kuzoe.
Kwa ujumla hivi vitu tunajifunza lakini matumizi yake kwenye mazingira ya kawaida ni nadra sana. Nadra kwa maana vile unavyofahamu haya mambo unakuwa na tabia na muonekano ambao tayari unakutengenezea kinga.
Nilianzia kujifunza kupitia movie. Nilikuwa na mwalimu wa martial arts ila alikuwa anakaza sana mpaka baadhi ya techniques alikataa nifundisha mwanzoni akidai mpaka nifike level fulani, hivyo hata matumizi ya silaha hakunifundisha ndipo kuanza kujifunza mwenyewe kupitia movie.Kwa hiyo na wewe mkuu ulijifunzia vitabu tu?
Threads za martial arts humu ni chache siyo mbaya kuziongezea,Uzi tayari
Ngoja tusubiri wazee wa shotokan waje kutoa muongozo.hivi wapi wanafundisha karate nikajifunze?
Ni nzuri sana mkuu na ukiizoea ni rahisi sana kutumia katika mapigano halisi. Kusimama na mtu zaidi ya mmoja ukiwa na nunchaku huwa ni jambo la kawaida. Ishu ni wakati wa kujifunza ngumu kuiweza bila kukugongaKatika vitu sijacheza ni kutumia hii silaha...ingawa nunchaku inatoa watu manundu sana
Mkuu upande huu wa Mwenge mpaka mapinga kwa uzoefu wako kuna dojo makini wapi?Ni nzuri sana mkuu na ukiizoea ni rahisi sana kutumia katika mapigano halisi. Kusimama na mtu zaidi ya mmoja ukiwa na nunchaku huwa ni jambo la kawaida. Ishu ni wakati wa kujifunza ngumu kuiweza bila kukugonga
Mkuu nikikutana na mtu anarusha na mimi narusha kwa dakika zaidi ya moja, hiyo ndio kupigana. Ila umekutana na mzembe ukamtandika kofi anakuangalia tu na matusi mengi kisha anaondoka hapo sijapigana. Mara ya mwisho kupigana ilikuwa 2014 mpaka leo sijakutana na wa kurushiana, ninaokutana nao wengi maneno mengi ila hawajui sanaa ya mapigano.Lini mtapigana...?
Mkuu sina uzoefu sana maeneo hayo boss. Labda kama kuna wazoefu wanaweza kusaidia. Binafsi sijawahi ingia dojo maalum, nimejifunza street kwa miaka yote zaidi ya sita na sparring ndio huwa kipimo cha uwezo wangu so hata ishu ya mkanda na level kiutaratibu sizijui sana kivile.Mkuu upande huu wa Mwenge mpaka mapinga kwa uzoefu wako kuna dojo makini wapi?
Lengo la hii sanaa siyo kupigana bali kujilinda Mkuu,utapiga kwa minajili ya kujilinda/ kujihami.Lini mtapigana...?