Habari za weekend wanaMMU.
Kwenye andiko hili nitashare personal experience, experience ya watu wengine pamoja na yale ninayoyaona ama kuyasikia kwenye jamii zetu.
Ikiwa umefikiria labda kichwa cha habari kina maana ya kuingia kwenye Ndoa ni Kujitoa Sadaka. Hapana hilo si dhumuni la mada hii
Kabla ya mtu kuanza kuwa na mawazo ya kuwa na mwenza, utasikia ama kuambiwa mengi sana. Kwasisi wanaume utaambiwa mwanamke ni Tabia, tafuta mwanamke anayeweza kucover nafasi ya mama yako, tafuta mwanamke mtakayepanga mambo yakaenda, n.k n.k kuna thread nyingi pia hata humu ndani zimeweka wazi ni wanawake gani wa kuwaepuka na ni wa aina ipi wa kuoa. All in All, itakubidi ufanye chaguzi sahihi ili kumpata aliyebora. Hata kama ulitulia ukampata mtiifu, mnyenyekevu, sijui bikra, mzuri wa sura na tabia believe kila mtu ana kasoro yake na kila ndoa inachangamoto zake.
Kuna jamaa yangu mmoja alipokuwa akiendea kuoa alikuwa akijiona kama the luckiest man in the world. Alikuwa akimuoa binti bikra, mwenye elimu yake, mwenye kumjua Mungu, mwenye adabu na utii, mwenye kila aina ya sifa nzuri. Believe me in less than a year in marriage ndoa ilikuwa chungu. Mwanamke amekuwa na kibri na mwenye sauti zaidi. Watu wa jinsia zote hubadilika sana. Kuna wanaume wanachange kabisa character zao za awali mpaka mtu unajiuliza hapa ndipo kwenye niliingia. Ndugu wanakuhoji ulimpendea mini huyu, ila kumbe mwanzoni mtu alikuwa yuko poa tu.
What I believe, Maisha ya ndoa yanajumuisha watu kuanzia wawili. Hivyo lolote litakaloamuliwa na mmoja wetu lazima liwe na impact kwa mwingine pia. Naamini kwenye kuongea, kusikilizana na kufikia muafaka lakini si kelele, kujiona mjuaji ama una haki saaana ama upo sahihi kwa kile unachofikilia kuliko mwenza wako. Binafsi nilijiwekea kuoa mwenye elimu mwenzangu nikijua we shall be thinking kwenye direction moja na it will be easy kueleweshana, this has been one of the biggest mistakes in my life.
You can play very well kuchagua mtu wa kuwa naye kwenye mahusiano ila hii kitu NDOA its something else. I believe ili at least kidogo NDOA ikae vizuri cha muhimu ni sacrifice na kila mtu akae kwenye nafasi yake. Kuna wakati kila mtu anakuwa na mawazo Fulani kuhusu jambo Fulani na kila mmoja anajiona yuko sahihi na msingi wa changamoto nyingi kwenye ndoa unaanzia hapa. I believe kama BABA akikaa kwenye nafasi yake, hivyo hivyo kwa MAMA na kukawa na kitu kinaitwa SACRIFICE ndani yao I believe Ndoa zitaweza dumu. Hali ya kukubali usahihi wa mwenzio ilhali ndani yako unajua hayuko sahihi ndicho ninachojaribu kukimaanisha hapa. Tunashindwa kujenga familia madhubuti, kujenga uchumi wa familia na kufanikiwa mengi lakini asubuhi hii nimeng'amua yote haya yanatokana na wanandoa kutojua kuwa Marriage is a Sacrifice if we need it to workout well.