Marking your territory...

ukiwa mjanja unafuta alama zote za mwanamke wako
kabla hujaleta mwingine...nguo,lotion,viatu unakusanya kwenye boksi
unaweka store....nilishindwa kugundua hiyo ya mapazia tu,basi..
later on niliyabadili pia lol
enzi hizo offcourse..lol

Hahahhah we kiboko, yaani akitoka unafagia mpaka vumbi afu siku anarudi warudishia au akirudi unamtolea avipange upya?? hahahahhah mie nawashauri wanawake wawe wajanja nao, ukiingia kwa mwanaume ukaona kuko neat, hebu chungulia kabatini au store hahha unawezapata jibu usishangae kukuta khanga zimerushiwa huko juu, vibanio vya nywele au hata pochi hahaha.

ila kwa The Boss hutopata kitu.

mhh 'The Boss' mbona hii issue ya mapazia nishakutana nayo ... bt i hope its nt u??? he he he lol

Naily umenichekesha kusema ukweli hiyo ya mapazia ni kiboko unajua mtu anaweza asihisi kuwa unamark bali atajua tu unadecorate!! But hata ukiweka mapazia kama mdoezi ni wa kupita itamuaffect vipi?

ukiwa mjanja unafuta alama zote za mwanamke wako
kabla hujaleta mwingine...nguo,lotion,viatu unakusanya kwenye boksi
unaweka store....nilishindwa kugundua hiyo ya mapazia tu,basi..
later on niliyabadili pia lol
enzi hizo offcourse..lol

Vipi unapokutana na mwanaume ambaye hana muda wa kumark territory/

Naona hii niongeze kwenye List ya if a guy is not into you....lol

Mwe kumbee!!!!!!!!!!!!! ushakutana na wale ukitoka nae ukajisahau tu ukamshika mkono utakavotolewa haraka utafikiri ulikuwa unataka kumuibia.

Nyie watu acheni kunivunja mbavu!! Chauro eti anakimbiza mkono kama anaibiwa? hahahahah mwe wanawake tuna shida afu wanasahau kuwa wengine sie starehe yetu kupetiwa sasa kama hutaki hata nishike mkono?! Si unaninyima haki zangu za msingi kimapenzi?? afu bado faraghani utaniita mpenzi wa moyo wako???!! I just dont get it!

Hapo ni based mfano ulotoa in blue…. IMO Mwanaume inapendeza amtoe mwanamke out Periond! Ila tu mwanamke has to take in mind once in a while ni lazima amtoe nae Mpenzi wake out… However inategemea na mliko enda.. kuna sehemu ambazo ni Casual… ambako hata mkishare expenses sio mbaya.. kwamba round hii huyu kalipa, mmepita hapa nawe walipa and the like… From the simple reasons kua; A man has a need to feel more in POWER katika mahusiano… the feeling of POWER katika relationship hujengwa na matendo… Hivo kama wataka saaana kushindana na your MAN katika Matunzo yenu, ama wataka kabisa wewe Mwanamke udhibiti… in time itamfanya asi feel POWERFUL katika huo uhusiano… na ikifika hapo… inakua doomed. But of coz kuna guys ambao they don't mind umtunze… Such a guy hayupo in my List of consideration (utanisamehe I am old fashioned – naweza fanya on the condition ni Mume wangu na mambo yake yameyumba' hapo nitafanya proudly forever&#8230😉

Dah! MJ1 hiyo ya kuvaa panty umenichekesha kweli kweli…. Umenikumbusha mbali pia….lol… Mapenzi haya! Wacha yaitwe Mapenzi…. Mie naona kama hamko pamoja inakua hivo hivo… Sijui nisemeje… but naona niseme kama hampo pamoja nayo yategemea… iko temporary ama permanent?? Kama temporary ndo inakua kama nilivo eleleza post yangu ya kwanza katika thread hii… ikiwa th former…. Kasheshe… maana hata haisaidii… Ndo kwanza a guy akikutambulisha saana kwa rafiki zake wakulinde… wanaishia kukutongoza kwa kuchafua jina la Mpenzi wako…

Kuhusu hapo penye red… ndo hapo wanawake hua tunajidanganya… Huwezi muita mwanamke mwenzio kipozeo na hali wewe pia hujalalalishwa... Mwanaume anaweza akakufanyia kila kitu na bado pia ukawa kipozeo pia... Overconfidence haifai kabisa katika hii issue... MJ1 kama wewe ni galfriend wa jamaa… hata siku moja usijidanganye kua wewe ni bora kuliko wanawake wengine alo nao ama wale ambao anatongoza for haja kuoa bado… Such confidence ina cost wengi.. ndo kwanza at the end of the day asiwaoe wooote akaenda oa mwingine kabisa ambae hakuona hata hivo vialama uliacha ku Mark territory… kazi kweli kweli… but sema muhimu ni kua it makes you feel confident hivo sio mbaya I guess…

Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa akishikwa mkono na mwenzake anaanza kumnanga mwenzake "Bwana vipi tunashikana mikono kama watoto wadogo" mimi naishia kucheka tu

Afro Denzi umeusemea moyo wangu!! Hapo kwenye perfume hapo ni kweli kabisa. Yaani mtu anahakikisha anaweka alama. Lipstick mara nyingi hutumika kwa wale vimada wanaotoka na waume wa watu...yeye anaweka sehemu ambayo anajua tu kuwa Mamsap wako ataona na litavumbuluka hahahaha kaaazi ni kwako!

bana eeeh mjini shirika ujamaa shamba,umaki teritore usimaki hapa mjini utaibiwa tu,hiyo ndo hali halisi,the best solution is not to think about it,si wanaume si wanawake siku hizi ukware ndo umetawala.
Well said........

MwanajamiiOne anazungumzia yale mapenzi ya kiukweli ya enzi za wazazi wetu. Enzi hizi watu wanajua kabisa yule pale ni Mrs. ODM...... Mr ODM akienda pembeni kidogo wanatongoza na bahati nzuri au mbaya hawakataliwi.....Wanajua kabisa MwanajamiiOne ni mchumba wa The Finest, wanatongoza kama kawaida.........

Acha khanga yako, watu wanaingia room wanafanya matusi wanajifutia khanga zako.
Valisha sijui pete, watu wanaichezea kama wanavyochezea shanga huku wanabanjua amri ya sita
Kamata kiuno hadharani mkiwa kwenye starehe, akienda toilet watu wanachukua namba za simu kesho yake wanakamata kiuno kitandani

MJ1 hiki si kizazii cha kumark teritorry, watakucheka watu! Ni kipindi cha wizi.......wizi mtupu!

Uwiii MAMMAMIA pole sana, huyo wa kumwaga shanga alikusudia kabisa kukuharibia mazima. Utajiteteaje uaminike kuwa shanga zilimwagwa kupitia dirishani? Ama kweli kuna wanawake vichaa!

Kwa hiyo hapo unasema kuwa kama tayari ashakuwa wako (kihalali) huna haja ya kumark territory yako? Kwa wanaume ni sawa mkishatuoa mnatakiwa kurelax ila sasa kwenu nyie sasa dah ni ngumu kwetu kurelax kwa sababu afadhali mngekuwa mkienda kwa vimada unastarehe tu kisha mnarejea ila sasa wengine mnatia nanga kabisaaaa.... so kwa mwanamke sidhani kama kuna kitu kama.tayari ashanioa basi ni wangu daima, so nijirestishe!!

Nadhani hii dhana ya marking your territory inawezakuwa applied hata kwa undani zaidi, mambo yote tuyafanyayo ya kuspice up relationship, mf. kuhakikisha kuwa unavaa vizuri, unatoka smart, una afya nzuri, uko happy ......haiwezifanya mwanaume akajulikana kuwa anaye anayempatia mwonekano huo?? Au?

Achana na hii kitu eti marking territory wengine ni chumbani tu ukiibuka huko tumbo ndii kama babu alivosema ukiondoka lazima ubebe kila kinachokuhusu .........hapo hamna haja tena ya yeye kujieleza ni wewe kuwaambia watu mhusika ni nani mwenzio alishamaliza kazi siku nyingi.

tushukuru siku hizi kuna vina saba mwe!

woi kile kidude cha thanks kimeenda wapi babu maana hata cha like kimenichenga leo.................

wengine bar namba za simu wanaandikiana kwenye vizibo vya soda,we acha tu wako ni wako mkiwa naye ndani akitoka wa wote aisee.

babu watu wamepinda! unadhani wanaogopa territoy ya miezi 9? kuna mtu humu jamvini aliweka uzi anatafuta territoy ya kukodi yenye hiyo 9 months beacon! tena kama mmasai anasema 'shee! mepata mtamba ina mimba kapsaa!'
Teritory...........Teritory............Teritory!

Leo tunamark Teritory.....

Kama umependa sana, na hutaki kupoteza ukipendacho........... Jaza yeye mimba! Hiyo ndo kiboko yake!

Mapenzi usiombee yachachuke maana unaweza juta kwanini ulipenda.

this is a very powerful message to me AshaDii aksante sana. I salute hili darasa.

Hahah AshaDii usicheke, hujaona mtu unasafiri (hata kama ni mumeo) anapakia panty zake ukazivae siku zote utakazokuwa huko??

Kweli kabisa nakubaliana na wewe, mara nyingi tunazitumia kwa kujijengea confidence mamii. Aksante kwa kukumbushia hilo. Hili darasa ni zito la haja, ubarikiwe AshaDii

At last tumepaa mtazamo wa upande wa pili. So hakuna umuhimu wa kumark, so ndo tunarudi kule kwenye kujiamini Babu au?? Mwe!
Ama kweli mie nimeshazeeka sasa.

Safi kabisa kajukuu....

Umeona bana........

Mi nlivyoona Masemere wangu ndo kifaa nachopenda kukiingiza kwenye himaya, sikuhangaika sijui kumshika kiuno hazarani, mi nlikamata yeye nikamwambia nataka uwe mama watoto wangu. Naye kwa kuwa alikuwa anataka kumark teritory yake akakubali. Basi mara ndii.....Kilivyojaa nikamwambia baby come this way.......

Ka-Matesha na ka-Mamshanga wetu ndo territory yetu kuu. Hata tukifanya wizi, bado tunarudi nyumbani kwenye himaya yetu......Huko nje ni wizi mtupu, huku ndani ndo kwenye himaya yenyewe.

Narudia tena, for the real and true love........... territory ni ndoa!

Aseeeeeeeeeee siku hizi na akili :brick:umeona mjukuu anavoona mbali mbona babu hujanipa zawadi sasa..............nshaanza kuchakachua Thread........... MJI nisamehe sirudii tena.

At last tumepaa mtazamo wa upande wa pili. So hakuna umuhimu wa kumark, so ndo tunarudi kule kwenye kujiamini Babu au?? Mwe!
Ama kweli mie nimeshazeeka sasa.
Now you are talking....!

Hiki ni kipindi cha kuamini visivyoaminika...... Unamwamini mwenzio mpaka pale utakapomfumania. Kuweka teritory watu watakucheka..... Nilimwona dada mmoja kamkamata jamaa yake kiuononi........ baamedi mmoja akaachia "kione kidemu kinavyojishaua na jamaa yetu, kinafikiri kiko peke yake" wakamalizia na halo haloooooo! kudadadadeki.

Kuna dada mmoja aliamua kujitangazia kwa mashoga wake kuwa amepima na ana UKIMWI, akitarajia watamwogopa mpenzi wake. Hao hao aliowatangazia wakamzunguka wakamlia vyake. Sasa kama unamark territory yako kwa kusingizia mpaka magonjwa yasiyotibika na watu hawaelewi somo, kuna kingine cha kufanya zaidi ya hicho?

Mke/mme/mpenzi wako ni WAKO anapokuwa na wewe. Asipokuwa na wewe hata umark Territory kwa kuibana baioloji kwa kofuli, watu wakakuchakachulia tu.

...hahahahahahahahahahahahahahahahahahah!
imenibidi nicheke tu hapa

hahahahahahahahahahahahahahah!
:brick:

seconded....!

the very professional comment...basing on the reality side of marriages and relationships

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…