Mkuu mimi suala zima la RBT (ring back tone), sijakubaliana nalo jinsi linavyoendeshwa kwenye makampuni yote ya simu nchini. Kwa mawazo yangu, mpiga simu ndiye anatakiwa kujichagulia wimbo ambao atakuwa anausikiliza wakati anapopiga simu. Sasa hawa "wataalamu" wameset kiasi kuwa kila anayekupigia anasikiliza wimbo uliouchagua wewe na sio wanaoupenda wao. Watu wana vionjo tofauti, hivyo huwezi kujua kama unawaburudisha au kuwachosha wanaposikiliza ujumbe fulani.