Mark ii gx 100 inasumbua kuwaka asubuhi

Shedangio

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
448
170
Habari wakuu nina mark ii grand gx100 ni msumari sana na ndo gari ninayotegemea ila wakati wa asubuhi inasumbua sana kuwaka waeza piga hata mara kumi yaani hadi kero.i la ikishaawaka siku nzima ukigusa ni jino moja tu.
naomba ushauri wenu wa kitaalamu.
 
Unaishi wapi? Kuna hot na cold plugs na kuna plugs mahususi kwa vipindi vyote vya hali ya hewa, jaribu kuangalia kwanza betri huenda imeisha nguvu, mwaga maji uweke mapya na kuipiga chaji au nunua mpya, ukiona bado badili plugs na kufanya service kwenye distributor na regulator.
 
Battery ikovpoa maana na kusumbua kote huko ila mwisho wa siku inaanza kuwaka pole pole
 
Unaishi wapi? Kuna hot na cold plugs na kuna plugs mahususi kwa vipindi vyote vya hali ya hewa, jaribu kuangalia kwanza betri huenda imeisha nguvu, mwaga maji uweke mapya na kuipiga chaji au nunua mpya, ukiona bado badili plugs na kufanya service kwenye distributor na regulator.
Naishi Lushoto ila mwanzo ilikuwa poa tu.
 
Unaishi wapi? Kuna hot na cold plugs na kuna plugs mahususi kwa vipindi vyote vya hali ya hewa, jaribu kuangalia kwanza betri huenda imeisha nguvu, mwaga maji uweke mapya na kuipiga chaji au nunua mpya, ukiona bado badili plugs na kufanya service kwenye distributor na regulator.
Nashukuru kwa ushauri wako kaka
 
Off Topic, Mkuu niko kwenye dakika za mwisho kununua Mark ii Grand GX110. Ila sina input sana kuhusu experience halisi ya kumiliki hii gari, unaweza nidokeza kidogo kwenye upande wa vipuri na Ulaji wake wa mafuta.
 
Tafuta gari aina nyingine ambayo itakua rahisi kuiuza na kuihudumia. Achana na hilo puto.
 
Habari wakuu nina mark ii grand gx100 ni msumari sana na ndo gari ninayotegemea ila wakati wa asubuhi inasumbua sana kuwaka waeza piga hata mara kumi yaani hadi kero.i la ikishaawaka siku nzima ukigusa ni jino moja tu.
naomba ushauri wenu wa kitaalamu.
nami mark 2 yangu ina ugonjwa huo nishapeleka kwa mafundi ila wakaniharibia zaidi kwa sasa nimeizoea tu, plug na kelele zingine wanazosema wadau nimeisha badili ila bado kuiwasha kwa raha hua ni jua likiwaka
 
Kama ni asubuhi tu
check battery maana ukishatembea inakuwa recharged
cheki plugs
cheki nozzle
 
mkuu hapo ugonjwa ni THW kiufundi ndio tunaiita hivyo hii jf mpya inanishinda kuweka picha ila hiyo switch huwa inakuwa na pin mbili huwa inafungwa kwenye systerm ya maji na kazi yake ni ku sens hali ya joto la maji na ikiwa imekufa kabisa output yake huwa zero hivyo control box huwa ina data huu ugonjwa upo sana kwenye kwenye engine ya 1G kavu.

pili kuna switch nyingine huwa inaitwa idle switch hii kazi yake ni kupandisha silensa wakati wa asubuhi lkn hii ukitaka kujua kama yenyewe ni shida au sio shida ni kazi nyepesi sana unapo washa kanyagia mafuta kama itawaka basi ni hiyo switch lkn kama haita waka basi ni ile switch ya maji coolant temperature sensor.
ANZIA HAPO MKUU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom