Marine traffic data post

Marine traffic data post

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,695
Reaction score
830,697
Leo ni meli tatu pekee zinaonekana kuwa zimepitia hadi sasa, katika mlango bahari wa Hormuz kulingana na uchambuzi wetu wa data za MarineTraffic

Kulingana na uchambuzi wa data za ufuatiliaji uliofanywa na kampuni ya ujasusi wa baharini ya Kpler, meli nne zilipita kwenye mlango bahari jana na sita Jumapili.

Idadi kubwa zaidi ya kuvuka kwa meli Hormuz ilikuwa wiki iliyopita ambapo meli 13 zilivuka Jumamosi.

Kabla ya mzozo kuanza, karibu meli 140 zilisafiri kila siku, kulingana na Kituo cha Habari cha Pamoja cha Baharini.
1775022027380.jpg
 
Yatafika yu elfu 5 we subiri
Bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa kiwango kikubwa katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo sasa lita moja inauzwa kwa shilingi 3,820 mwezi Aprili 2026, kutoka shilingi 2,864 mwezi Machi. Ongezeko hilo limetangazwa rasmi na Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) katika taarifa yake ya marekebisho ya bei za mafuta.

Kwa mujibu wa EWURA, kupanda kwa bei kunachangiwa na mabadiliko katika soko la kimataifa, ikiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi pamoja na changamoto za usafirishaji. Aidha, hali ya kisiasa na kiusalama duniani imeendelea kuathiri upatikanaji na usambazaji wa mafuta, jambo linalosababisha gharama kupanda katika masoko mbalimbali.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa gharama za uagizaji zimeongezeka kutokana na kupanda kwa bei za bima ya meli, ucheleweshaji wa mizigo na gharama za usafirishaji kwa ujumla. Bei hizo mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia Aprili Mosi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wametakiwa kutumia nishati kwa uangalifu na kuzingatia njia mbadala za kupunguza matumizi. EWURA imesisitiza kuwa itaendelea kufuatilia mwenendo wa soko la dunia na kuchukua hatua stahiki kulinda maslahi ya watumiaji wa ndani.

MAFUTA YAKIPANDA KILA KITU KITAPANDA BEI MARA DUFU.
 
Wametupiga vibaya sana na hatuna la kufanya. Haya mafuta ya sasa ni akiba ya zamani hayakupaswa kupandishwa bei
bei inapanda haraka kwa sababu inaangaliwa gharama za kureplace stock iliyopo, na kwenye kushuka bei inashuka taratibu kwa kuangalia mzigo uliopo ulionunuliwa kwa bei kubwa.

hapa mpaka mambo yakae sawa ni muda mrefu sana
 
Bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa kiwango kikubwa katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo sasa lita moja inauzwa kwa shilingi 3,820 mwezi Aprili 2026, kutoka shilingi 2,864 mwezi Machi. Ongezeko hilo limetangazwa rasmi na Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) katika taarifa yake ya marekebisho ya bei za mafuta.

Kwa mujibu wa EWURA, kupanda kwa bei kunachangiwa na mabadiliko katika soko la kimataifa, ikiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi pamoja na changamoto za usafirishaji. Aidha, hali ya kisiasa na kiusalama duniani imeendelea kuathiri upatikanaji na usambazaji wa mafuta, jambo linalosababisha gharama kupanda katika masoko mbalimbali.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa gharama za uagizaji zimeongezeka kutokana na kupanda kwa bei za bima ya meli, ucheleweshaji wa mizigo na gharama za usafirishaji kwa ujumla. Bei hizo mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia Aprili Mosi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wametakiwa kutumia nishati kwa uangalifu na kuzingatia njia mbadala za kupunguza matumizi. EWURA imesisitiza kuwa itaendelea kufuatilia mwenendo wa soko la dunia na kuchukua hatua stahiki kulinda maslahi ya watumiaji wa ndani.

MAFUTA YAKIPANDA KILA KITU KITAPANDA BEI MARA DUFU.
Serikali yetu ya kishetani...
1. Sisi huwa tuna akiba ya mafuta ya miezi mi3, kwanini mwezi wa kwanza tu wa vita yapande!!?
Huu ni uhuni

2. Kodi ya serikali kwenye mafuta huwa inafika kati ya 1300 hivi ama 150 sikumbuki vizuri.
Kwanini wasipunguze kodi za mafuta, ili bei ipoe lakini pia wao wapunguze matumizi, wabane matumizi ya serikali, ili mambo yaende sawa.
Huu ni ubinafsi.

3. Teknolojia ya magari ya umeme ndio iko moto, serikali imechukua hatu gani kwenda huko, je kodi ya magari ya umeme ikoje, ile BRT wangechukua magari ya umeme tupu, serikali itembelee magari ya umeme ambayo yanaokoa mpaka 50% ya matumizi ya nishati.
Huku ni kukosa visions ama makusudi kwa ubinafsi wao
 
Pikipik/gari za umeme litakua kimbilio endapo bei itaenda zaidi.

Pikipik za umeme, umeme wa buku unakimbia km135
 
Waafrika ni wajinga 🤣 mmekuwa tegemezi kuanzia kijamii ,kisiasa ,kitamaduni mpaka kiuchumi...Hao wanaojifanya wamesoma wameingizwa mkenge wa kuwa ombaomba wa wazungu..

Kila kona wanaongelea mafuta ,ni tatizo la kujifanya watu wanajua sana.
 
Wavaa vilemba wana jeuri mkuu! Wameshakamata mrija wa wese, wese halipiti hapo, huyo babu wa U.S na huyo BIBI wa mazayuni walikurupuka waseng* wale.
Mafuta ya ndege sio muda, yanaadimika,utasikia kelele tuu, kmmk.
 
Wametupiga vibaya sana na hatuna la kufanya. Haya mafuta ya sasa ni akiba ya zamani hayakupaswa kupandishwa bei
Majambazi yametumia huo mwanya kuiba aisee na hawaogopi kwa sababu wapanga bei sasa hivi ni hao wafanyabiashara ya mafuta wanatoa maelekezo tu wiki yote hii huko Mbeya walikua hawauzi mafuta waliambiwa yatapanda bei kubwa sana.
 
Waafrika ni wajinga 🤣 mmekuwa tegemezi kuanzia kijamii ,kisiasa ,kitamaduni mpaka kiuchumi...Hao wanaojifanya wamesoma wameingizwa mkenge wa kuwa ombaomba wa wazungu..

Kila kona wanaongelea mafuta ,ni tatizo la kujifanya watu wanajua sana.
wasomi wa tanga mnatusaidiaje hapa kwenye hili mkuu?
 
Uganda wanachimba wese kwanini wasimkaribishe DANGOTE kuyaswafishaaa???
AFrikA kinachotusumbua ni UBINAFSI,,,
TUkIUNGANA MAMBO YA KISENGE YA HUKO DINIANI HAYATATUPA SHIDA
 
Back
Top Bottom