Uchaguzi 2020 Maridhiano ya kitaifa, chachu ya maendeleo, hongera Kenyata na Odinga kwa kufuta tofauti zenu

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,672
2,540
Jana tarehe 27/11/2019 Taifa la Kenya limezindua riporti ya tume maalumu inayoitaka serikali ya Kenya kuleta maridhiano ya kitaifa. Kwa sikio langu nimemsikia Rais Uhuru Kenya akisema kuwa Yeye yuko tayari na ameshakubaliana na Odinga kuhusu hilo. Kwa pamoja walipeana mikono na Kukumbatiana. Wakionesha dalili ya kufuta tofauti zao 'for ever'

Kwa mujibu ya riporti ile Kenya sasa wamekubaliana kuzika Tofauti zao walizo zirithi kutoka kwa wazazi wao ili kuifanya Kenya iwe mpya isiyo na misuguano tena ya kikabila wala 'SIASA ZA CHUKI'

Huu ni muelekeo mwema kwa Bara hili la Afrika lenye Viongozi wenye Ulimbukeni mkubwa wa Kutawala na kupupia madaraka kwa gharama yoyote ile kama wale walio tayari kuulinda mti unaoitwa MUUNGANO kwa NGUVU ZOTE.

Na kama wale wanao ua raia kwa kusingizia eti wanalinda amani ya nchi ilhali wao ndio wanaiondoa kwa kutumia Risasi, na mateso yasio na kipimo kwa wananchi wasiokuwa na silaha .

Imekuwa Dhambi Afrika kwa Raia kudai haki yake fulani kwa njia salama ya kuandamana ili kuonesha hisia zake ,
Huu ni mwanzo mzuri kwa Ukanda huu wa Afrika mashariki.

Tanzania nayo inaweza kuiga mwenendo huu na huenda sisi tuko katika hali nzuri zaidi ya kuweza kuufikia hayo maridhiano kwa vile nchi yetu haina mivutano mikubwa ya kikabila wala kikanda .

Hata hili la Muungano pia nalo ni jepesi sana ikiwa Dhamira na Utashi wa CCM-chama tawla, utakuwepo.
Taifa linaweza kuondokana na ombwe la kuimarisha Majeshi dhidi ya raia wake kila uchao na kuongeza nguvu katika vyanzo rafiki vya ajira kwa Taifa.

Nchi hii ni Muungano wa Jamuhuri Mbili zilizokuwa huru,Kuna shida gani hapa pia kufikia Maridhiano kwa pande mbili hizi tena ya wazi,badala ya kutishana na kukamiana kutiana ndani na Kuimarisha Kikosi cha Usalama wa Taifa kila uchao ili kulizui jambo lisilozuilika lilomo kwenye vifua vya watu?

Naukumbuka Ule muafaka wa Zanzibar ulipofikiwa na kuundwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ,nchi ya Zanzibar ilibadilika kimtazamo na watu wake waliishi kwenye matumaini makubwa sana.Niliwaona CCM na CUF wakati ule wakiwa ndo mahasimu wakubwa, wakiingia kwenye viwanja vya sherehe za Mapinduzi kwa mbwembwe ,mkono kwa mkono wakiwa na tabasamu nyusoni mwao na kuoneshana upendo wa hali ya juu.Waliaminiana na hata kunywa maji chupa moja CCM na CUF bila ya kutiliana mashaka kuwa wanweza kuhujumiana.

Lakini Ghafla kufika 2015 Ndoto ile ikatoweka kwa Mapinduzi ya Jecha akisaidiwa na Vikosi vya CCM vyenye sare ya Jeshi, kufuta matokeo halali na kufuta uchaguzi.
Kwa hakika Tumechoshwa mno na hali hizi.

TUNATAMANI TAIFA LETU LIWE NA MARIDHIANO ILI WOTE TUSAIDIANE KUJENGA NCHI YETU BADALA YA WENGINE KUIHUJUMU NA KUBEZA JUHUDI ZA WENGINE KISA UPINZANI .
Nawakilisha
Battawi
 
Tanzania Mchakato wa Katiba Mpya Uchama Tawala uliubeba Mchakato ukayabadili mawazo ya watanzania
 
Back
Top Bottom