Marekebisho ya mto msimbazi

Marekebisho ya mto msimbazi

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Tunakumbuka mvua zilizonyesha mwaka huu zilileta hasara kubwa kwa wananchi waishio kando kando ya mto Msimbazi. Kama sikosei kulikuwa na TAMKO la Serikali kuwa litakuja na suluhisho la kudumu ili wananchi wasipate hasara tena. Kwa kuwa msimu wa mvua sasa unakaribia ni vyema sasa Serikali ikatekeleza TAMKO lake. Naishauri pia Serikali iige yale yanayotokea kule Kenya ambapo wameanza kubomoa majumba yenye thamani ya mabilioni ya wale waliokiuka taratibu za ujenzi ikiwa ni kujenga kando kando ya mto.
 
Dsm matamko yote yanayohusu mafuriko au magonjwa ya mlipuko hutolewa wakati wa mvua na hukoma pindi mvua zikiacha kunyesha.
 
Mkuu maeneo ya daraja la kiembembuzi kuelekea segerea kuna makaburi yalikua kando ya mto kama nusu eka nusu yake imezombwa na maji ya msimu huu ukipita pale utaona aisee inasikitisha sana
 
tafadhali mleta mada sirikali inapaswa kulipa fidia. bonde la mkwajuni kuna watu maisha yao yamehalibika hadi leo
 
Serikali yetu utendaji matamko wake ni wakati wa tukio lenyewe maana linakuwa na maslahi kwao kisiasa, wakizuia tukio kutokea mfano mafuriko watawapata wapi wahanga wawahubirie siasa kwa maslahi yao? Amka mlala hoi mwenzangu jitambue jisaidie mwenyewe kuepuka linalowezekana kwa nguvu zako mwenyewe, kutegemea serikali ni sawa na mtegemea cha ndugu mwishowe hufa masikini.
 
Back
Top Bottom