Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasema kuwa nchi za Ghuba ni lazima zilegeze hatua yao dhidi ya Qatar ambayo inalaumiwa na majirani zake kwa kuunga mkono ugaidi.
Saudi Arabia, Muungano wa nchi za kiarabu, Misri na Bahrain walikata uhusiano wa usafiri na wa Kidiplomasia na Qatar siku ya Jumatatu
Bwana Tillerson anasema kuwa hatua hiyo inasababisha kuwepo madhara ya kibinadamu.
Licha ya kumsifu Emir wa Qatar kwa kupuuza uungwaji mkono makundi ya kigaidi, Bwana Tillerson anasema mengi yanahitaji kufanywa.
Naye Rais Trump alikuwa ameandika kwenye kwenye mtandao wake wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar, na hata kudai kuwa alishiriki katika uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia pamoja na nchi nyingine.
Ndege za Qatar zilipigwa marufuku ya kutumia anga za baadhi ya majirani zake.
Hatua hiyo ya ghafla ilichukuliwa baada ya msukosuko ambao umedumu miaka kadha kati ya Qatar na majirani zake wa Ghuba.
My take: Marekani acheni unafiki na undumilakuwili. Mnaleta ghadhabu na mkanganyiko sana kauli zenu.
Chanzo: BBC