Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Yahya Al Sinwar

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
12,047
21,929
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

IRAN.png
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.
Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .
View attachment 3119613View attachment 3119615
Hamna kitu watafanya, kwa miaka mingapi sasa western forces wamekuwa wakitumia ardhi za majirani zake? Tena wana base? Wameziadhibu hizo nchi kwa lolote?
 
Hamna kitu watafanya, kwa miaka mingapi sasa western forces wamekuwa wakitumia ardhi za majirani zake? Tena wana base? Wameziadhibu hizo nchi kwa lolote?
Saudi Arabia ilipoungana na USA dhidi ya Houthi ili wambakishe Mansour madarakani,kila siku ilikua petroleum plant za Saudi Arabia zililipuliwa na kuwasababishia hasara za mabilioni ya dola.
Pia kuna hatari ya Iran kufunga strait of hurmoz.
 
Kila siku zilipuliwa una uhakika? Saudi waliacha kuzalisha mafuta? Waliyumba kiuchumi?
No the truth is iran hawez fanya lolote la kuumiza majirani. Ata chimba biti for nothing
 
Iran imeonya mataifa ya Ghuba kwamba hatua zozote dhidi yake, ikiwa ni pamoja na matumizi ya anga au kambi zao za kijeshi na Israel, zitazingatiwa kama kitendo cha uhasama ambacho kitahitaji majibu sawia, kulingana na afisa mkuu wa Iran, kama ilivyoripotiwa na Reuters.
 
Back
Top Bottom