Marekani yautaka mradi wa Bandari Bagamoyo

Niliwahi kusema humu kwamba Marekani kamwe haitokubali China ichukue bandari ya Bagamoyo na kuweka manowari na meli zake za kivita. China ikipata bandari ya Bagamoyo, itahatarisha maslahi ya Marekani kwenye bahari ya hindi na ndani ya bara la Afrika. Kitu ambacho Marekani itakipiga vita mpaka mwisho.
Kwahiyo mkuu huu mradi hautatekelezwa tena? Maana kuna kimya kingi kisicho na kifani kuhusu mradi huu.
 
Whoever builds the port it does not matter, what is important should be a win-win situation not otherwise.
 
Mpaka serikali ikubaliane na Wamarekani. La sivyo hakuna kitakachofanyika.
Kuna hii zabuni imetangazwa na Wizara ya Uchukuzi few days ago. Je ina uhusiano na hii Bagamoyo Port Project?
IMG-20230912-WA0036.jpg
 
SERIKALI ya Marekani imeahidi kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, kama Tanzania itakubali kupokea msaada huo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 12 Mei 2022, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus, akielezea mafanikio ya ziara ya kikazo iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, nchini Marekani, Aprili mwaka huu.

“Kwa upande wa ujenzi wa Bagamoyo, Serikali ya Marekani wao wamesema iko tayari kutoa utaalamu wa ushauri kuhusu ujenzi huo wa Bandari ya Bagamoyo endapo Seriklai ya Tanzania itahitaji,” amesema Zuhura.

Katika nyingine, Zuhura amesema, Marekani imeridhishwa na hali ya kisiasa iliyopo nchini, na kwamba imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala hayo.

“Nchi ya Marekani wameridhishwa na hali ya kisiasa inavyoendelea nchini, hivyo wanaona ni muhimu kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye mambo hayo,” amesema Zuhura.

Ujenzi wa bandari hiyo ulizinduliwa 2015 na Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete, lakini Juni 2019, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Hayati John Magufuli, ulisitisha utekelzaji wa mradi huo uliokuwa chini ya mradi wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo.

Mradi huo ulikuwa ukifadhiliwa na Serikali ya China, ulisitishwa na Rais Magufuli kwa maelezo kwamba mkataba wake ulikuwa wa hovyo.

Hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, umefufua majadiliano kuhusu ujenzi wa mradi huo na wawekezaji
Marekani wapewe tu!
 
Marekani ni maadui kupita maelezo, ni wapi watu hawa wameingia na nchi kuona faida zake ,yaani kama kulaniwa basi hawa wamerekani wamelaaniwa .
Mwenye macho haambiwi tazama labda awe hajaona. Yaani kila walipojichimbia huondoka wakiwacha mateso na madhila na walimo nchi huwemo kwenye matatizo milele.
Taiwan,South Korea Siria,Libya Iraq ,zipo nyingi tu ,hawa ni nge wale wanakutafuna huku wanakupulizia aka kukusifu.
Mambo yote sasa ni Brics ,jifanyeni vipofu muwakaribishe hao vilaza matapeli ,sasa hivi wanahaha kutafuta pa kujichomeka yaani wahoi bin taaban na jipya ni kuwa akiba yao ya mafuta ya petrol imeanza kuyeyuka na kupungua utabiri wa shida ya mafuta huko kwao ni jambo la miezi michache tu.
Wezi hawa wamechukua sehemu ya Siria na kuikalia kumbe wanaiba petrol ,wizi wao haukuwasaidia ,sasa wameanza kulia
 
SERIKALI ya Marekani imeahidi kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, kama Tanzania itakubali kupokea msaada huo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 12 Mei 2022, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus, akielezea mafanikio ya ziara ya kikazo iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, nchini Marekani, Aprili mwaka huu.

“Kwa upande wa ujenzi wa Bagamoyo, Serikali ya Marekani wao wamesema iko tayari kutoa utaalamu wa ushauri kuhusu ujenzi huo wa Bandari ya Bagamoyo endapo Seriklai ya Tanzania itahitaji,” amesema Zuhura.

Katika nyingine, Zuhura amesema, Marekani imeridhishwa na hali ya kisiasa iliyopo nchini, na kwamba imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala hayo.

“Nchi ya Marekani wameridhishwa na hali ya kisiasa inavyoendelea nchini, hivyo wanaona ni muhimu kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye mambo hayo,” amesema Zuhura.

Ujenzi wa bandari hiyo ulizinduliwa 2015 na Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete, lakini Juni 2019, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Hayati John Magufuli, ulisitisha utekelzaji wa mradi huo uliokuwa chini ya mradi wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo.

Mradi huo ulikuwa ukifadhiliwa na Serikali ya China, ulisitishwa na Rais Magufuli kwa maelezo kwamba mkataba wake ulikuwa wa hovyo.

Hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, umefufua majadiliano kuhusu ujenzi wa mradi huo na wawekezaji
Hapa kuhusu hali ya kisiasa tumepigwa. Siku zote mabepari ukiwapa mradi au ukiwaonyesha deal zuri lazima watakaa na wewe hata kama ni dikteta. Hali ya kisiasa inapimwa na wananchi wenyewe na sio wataka minofu nje. Wakionyeshwa ishara ya deal wanakupigia makofi. Tumeona nchi za West Africa ziiongozwa na ma dikteta lakini hakuna Mmarekani au Europian yeyote anayepiga kelele zaidi za kusema hali ya kisiasa safi.
 
Back
Top Bottom