Marekani yautaka mradi wa Bandari Bagamoyo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
618
SERIKALI ya Marekani imeahidi kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, kama Tanzania itakubali kupokea msaada huo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 12 Mei 2022, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus, akielezea mafanikio ya ziara ya kikazo iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, nchini Marekani, Aprili mwaka huu.

“Kwa upande wa ujenzi wa Bagamoyo, Serikali ya Marekani wao wamesema iko tayari kutoa utaalamu wa ushauri kuhusu ujenzi huo wa Bandari ya Bagamoyo endapo Seriklai ya Tanzania itahitaji,” amesema Zuhura.

Katika nyingine, Zuhura amesema, Marekani imeridhishwa na hali ya kisiasa iliyopo nchini, na kwamba imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala hayo.

“Nchi ya Marekani wameridhishwa na hali ya kisiasa inavyoendelea nchini, hivyo wanaona ni muhimu kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye mambo hayo,” amesema Zuhura.

Ujenzi wa bandari hiyo ulizinduliwa 2015 na Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete, lakini Juni 2019, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Hayati John Magufuli, ulisitisha utekelzaji wa mradi huo uliokuwa chini ya mradi wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo.

Mradi huo ulikuwa ukifadhiliwa na Serikali ya China, ulisitishwa na Rais Magufuli kwa maelezo kwamba mkataba wake ulikuwa wa hovyo.

Hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, umefufua majadiliano kuhusu ujenzi wa mradi huo na wawekezaji
 
Niliwahi kusema humu kwamba Marekani kamwe haitokubali China ichukue bandari ya Bagamoyo na kuweka manowari na meli zake za kivita. China ikipata bandari ya Bagamoyo, itahatarisha maslahi ya Marekani kwenye bahari ya hindi na ndani ya bara la Afrika. Kitu ambacho Marekani itakipiga vita mpaka mwisho.
 
Kwa usalama wa nchi yoyote maskini, haitakiwi kuwagonganisha kimaslahi Mataifa Mawili au zaidi makubwa. Kinachoikuta Ukraine ni hiyo.

Nchi ijitahidi kwa vyovyote vile kutowagonganisha mataifa haya mawili makubwa katika mradi mkubwa kama huo.
Kwanza haitakaa itengamae mradi kama huo.
 
Back
Top Bottom