Marekani yatangaza vikwazo vya biashara dhidi ya China

Marekani yatangaza vikwazo vya biashara dhidi ya China

Yako Atta

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2016
Posts
288
Reaction score
468
Nchi ya China Ijumaa hii imeionya Marekani kuwa haiogopi vita vya kibiashara wakati huu ikitishia kutoza kodi ya zaidi ya dola bilioni 3 kwa bidhaa kutoka nchini Marekani katika kile kinachoonekana kujibu tangazo la rais Donald Trump kutoza kodi dhidi ya bidhaa kutoka China.

Utawala wa Beijing umetoa orodha ya bidhaa ambazo zitalengwa na kuongezewa ushuru wa hadi kufikia asilimia 25 kuanzia kwenye matunda hadi kwa nyama ya nguruwe licha ya kuwa imeshindwa kuchukua hatua zaidi na kuonesha nia ya kuwa na mazungumzo.

Hatua za hivi karibuni zimeshuhudia masoko ya hisa yakiporomoka wakati huu Marekani, ambayo inaituhumu Uchina kwa wizi wa haki miliki pamoja na hatua nyingine ambazo sio za haki dhidi ya makampuni yake, huenda ikachochea vita ya kibiashara.

"China haitaki kupigana vita ya kibiashara, lakini haiogopi kabisa vita hiyo," imesema taarifa ya wizara ya biashara ya China.

Mapema rais Donald Trump alitia saini amri ambayo itaweka ukomo kwa uwekezaji wa makampuni ya Uchina nchini humo.

"Tuna tatizo kubwa la wizi wa haki miliki linaloendelea kwa sasa," amesema rais Trump wakati akitia saini agizo hilo ambalo litajumuisha bidhaa ambazo zitatozwa ushuru wa hadi kufikia asilimia 25.

Hatua ya Trump haijachukua mara moja hatua za kuweka ushuru mpya, lakini ndani ya majuma mawili waziri wa biashara wa Marekani anatarajiwa kutangaza bidhaa zilizolengwa kwenye amri hiyo ya rais Trump.

Wakati huu rais Trump akionekana kutafuta ugomvi na mataifa yenye nguvu, utawala wa Beijing umeonya kuwa vita vya kibiashara havitamnufaisha yeyote na haitakaa kimya kuona Marekani ikitoa adhabu kwa biashara zake.

Waziri wa viwanda Wilbur Ross alisema Alhamisi ya wiki hii kuwa hatua za kulinda haki zake miliki ililenga kuifanya China ije kwenye meza ya mazungumzo na kujadiliana kutafuta njia za kudhibiti wizi huo.

Source: RFI Swahili
Mwandishi: Emmanuel Richard Makundi
 
Trump akiwa kwenye kampeni alisema ataishusha dhamani makusudi hela ya china

Sasa naona china kajaa kwenye 18 za mzee sijui china nae atakaza msuli, Soko kubwa la magumashi la bidhaa za china lipo Africa
 
Marekani hii vita haiwezi
Marekani wako 340m people, China wako zaidi ya 2b people. Imangine bidhaa yako ikikataliwa China impact yake inakuwaje? yaani ni sawa na kusema Kilombero hawataki kufanya biashara na DSM
 
Back
Top Bottom