Marekani yapeleka wanajeshi Gabon ikihofia machafuko Congo

Marekani yapeleka wanajeshi Gabon ikihofia machafuko Congo

Hilo linafahamika kaka,tatizo sasa hawashtuki na kukubali kujifunza wakabadilika,wanakubali kuchochewa na kuchocheka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tulishatawaliwa mpaka kifikra so kujikomboa kwenye makucha ya mzungu siyo leo wewe huoni tunakataa majina yetu ya kiafrika na kuitwa yao eti ndiyo mazuri
 
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake imewapeleka wanajeshi 80 mjini Libreville, Gabon kuwalinda raia wa Marekani na ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika barua aliyowasilisha Bungeni jana, Trump alisema wanajeshi Zaidi huenda wakapelekwa katika eneo hilo kutokana na uwezekano wa kuzuka maandamano yenye ghasia.

Barua ya Trump imesema wanajeshi hao: “watabaki katika eneo hilo hadi hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utakapokuwa imara na uwepo wao usihitajike tena.”

Mwishoni mwa wiki Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani ilitoa wito kwa Tume ya Uchaguzi – CENI kuhakikisha kuwa kura zinahesabiwa kwa umakini na kutishia kuwawekea vikwazo watakaohujumu mchakato huo au kutishia Amani na utulivu wa nchi hiyo.

Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ziliiongezea mbinyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zikiitaka iheshimu matakwa ya wapiga kura wakati muda wa mwisho wa kutoa matokeo ukikaribia.

Kuna ongezeko la matarajio kuwa wasimamizi wa uchaguzi watachelewesha matokeo ya mwanzo yanayotarajiwa Jumapili – hatua inayoweza kuongeza hofu katika nchi hiyo isiyokuwa na utulivu.

“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko katika wakati wa kihistoria kuelekea mpito wa kidemokrasia,” umesema Umoja wa Ulaya.

Umetoa wito kwa maofisa kuhakikisha mat okeo yananayosubiriwa yatatimiza matakwa ya wapiga kura.

Ombi sawa na hilo limetolewa na Umoja wa Afrika – AU baada ya kupewa tathmini kutoka kwa mkuu wa timu ya uangalizi wa uchaguzi yenye wanachama 80.

“Ni muhimu kuheshimu matokeo ya uchaguzi,” amesema mkuu wa AU Faki Mahamat kwenye Twitter.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana katika kikao cha faragha kuujadili uchaguzi huo, lakini baada ya masaa mawili ya mkutano likashindwa kukubaliana kuhusu taarifa kwa vyombo vya habari.

Wanadiplomasia wamesema nchi kadhaa yakiwemo mataifa ya Kiafrika yalisema hatua ya aina hiyo itakuwa ya mapema mno.

MPEKUZI
 
Wamesema wanalinda raia wake. Si kuingilia uchaguzi.
Mbona povu lingi ndugu?
Halaf hili si jambo geni, panapotokea machafuko katika nchi fulani, raia wa nchi nyingine huwa wanarudishwa nyumbani. Au nchi husika hutuma vikosi kulinda wananchi wao. Muda mwingine husimamia zoez la kuwaondoa.
Marekani imepeleka Wanajeshi 80 nchini Cabon kwa kile kinachodaiwa ni kulinda Ubalozi na Raia wake nchi Congo DRC kwa madai ya uwezekano wa kutokea Ghasia.
Upuuzi huu wa Marekani kuhubiri Deomkrasia wakati yenyewe ndiyo ya kwanza kuingilia mambo ya nchi zingine ni wa kulaani kwa nguvu zote na Waafrika.

Heko kwa Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walioketi kwa kujadili Uchaguzi wa Congo DRC kwa kukataa kuunga mkono upuuzi huo wa Marekani.

Marekani Yapeleka Wanajeshi Gabon ili Kukabiliana na Machafuko yoyote yanayoweza Kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). | MPEKUZI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nauliza tu,hivi laana ya mtu mweusi inaweza kumpata mtu mweupe?(Mzungu)
 
Na yatakaa huko hadi 2020 kuja Tanzania kulinda raia wa Marekani.
 
Wamesema wanalinda raia wake. Si kuingilia uchaguzi.
Mbona povu lingi ndugu?
Halaf hili si jambo geni, panapotokea machafuko katika nchi fulani, raia wa nchi nyingine huwa wanarudishwa nyumbani. Au nchi husika hutuma vikosi kulinda wananchi wao. Muda mwingine husimamia zoez la kuwaondoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Marekani ndiyo kawaida yao wanapoona kuna utajiri katika nchi fulani kujifanya kulinda raia wake kumbe lengo Leo ni utajiri huo
 
Mkuu hiyo ni kawaida ya USA hasa pale inapotokea hali ya wasiwasi kwenye chaguzi zetu za Africa.. DRC kuna raia wa USA hivyo kunapotokea sintofahamu ni jukumu la USA kuangalia uwezekano wa kuokoa raia wake ndio maana hawako DRC ila wako Gabon..

Kama kuna uwezekano hata Tanzania tukae tayari kwenda kuokoa raia wetu hali ikiwa mbaya..
 
Marekani imepeleka Wanajeshi 80 nchini Cabon kwa kile kinachodaiwa ni kulinda Ubalozi na Raia wake nchi Congo DRC kwa madai ya uwezekano wa kutokea Ghasia. Hicho ni kisingizio tu cha kutafuta Sababu ya Kuiingilia Congo DRC yenye utajiri mkubwa wa Madini ili iweze kufyonza Madini hayo.
Upuuzi huu wa Marekani kuhubiri Deomkrasia wakati yenyewe ndiyo ya kwanza kuingilia mambo ya nchi zingine ni wa kulaani kwa nguvu zote na Waafrika.

Heko kwa Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walioketi kujadili Uchaguzi wa Congo DRC kwa kukataa kuunga mkono upuuzi huo wa Marekani.

Marekani Yapeleka Wanajeshi Gabon ili Kukabiliana na Machafuko yoyote yanayoweza Kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). | MPEKUZI
Intaprinyuwaa kajifunze kingereza.

marekani inaenda kulinda raiya wake waliopo Congo.
 
Mkuu hiyo ni kawaida ya USA hasa pale inapotokea hali ya wasiwasi kwenye chaguzi zetu za Africa.. DRC kuna raia wa USA hivyo kunapotokea sintofahamu ni jukumu la USA kuangalia uwezekano wa kuokoa raia wake ndio maana hawako DRC ila wako Gabon..

Kama kuna uwezekano hata Tanzania tukae tayari kwenda kuokoa raia wetu hali ikiwa mbaya..
Duniani kote kunapotokea wasiwasi katika nchi ningine kinachofanyika ni kuondoa raia wake na siyo kupeleka jeshi, usitake kutudanganya
 
Lengo la mwandishi ni zuri kimtazamo WA nje lkn utakuta majitu humu yanataka nchi yetu ifanyiwe hivyo kwa manufaa ya wahuni
Nadhani wewe umenielewa vizuri sana, Hawa sijawahi kusikia Tanzania tunapelekea jeshi letu katika nchi ambazo kuna raia wetu na hali ya kiusalama siyo nzuri huko. mbaya kabisa Marekani wana tabia ya kuepeleka jeshi kwenye nchi zenye utajiri wa asili
 
Siwatetei. Ila hawajapeleka jeshi kubwa kama walivyofanya kwa nchi nyingine.
Ila safar hii wameenda kulinda raia wao. I guess ni ubalozini.
Marekani ndiyo kawaida yao wanapoona kuna utajiri katika nchi fulani kujifanya kulinda raia wake kumbe lengo Leo ni utajiri huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila nchi ina utaratibu wake. America wanajali sana wananchi wao kiasi kwamba hata kama akifariki.. mwili lazima urudishwe nyumban kwa gharama zozote zile.
Kwetu sis huwa raia wetu tunawaleta ubalozin then inatumwa ndege kuwarudisha nyumbani.
Sion baya lolote hapo..

Back
Top Bottom