Marekani yamuonya tena Kagame

Marekani yamuonya tena Kagame

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

JUMAPILI, JANUARI 19, 2014 06:49 NA MWANDISHI WETU


WAKATI utata ukiwa umegubika juu ya kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Rwanda, Kanali Patrick Karegeya, taarifa kutoka Ikulu ya Marekani zinaitaja nchi hiyo kuhusika moja kwa moja na kifo hicho. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki, amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari, ukiwamo mtandao wa Yahoo pamoja na BSN, akisema kuwa Rwanda imehusika na kifo cha Karegeya.

Katika maelezo yake hayo, Psaki alisema kwamba kwa mujibu wa onyo alilolitoa Rais Paul Kagame hivi karibuni, kwenye ibada ya kuliombea taifa hilo, inadhihirisha undani wa kifo cha Karegeya.

"Tuna wasiwasi na mfululizo wa mauaji ya wanasiasa maarufu nchini Rwanda," alisema Psaki.

Kauli hiyo imekuja wakati tayari kumekuwapo na shutuma nyingi zinazomhusisha Rais Kagame na tukio la kifo cha Karegeya, kutokana na uhasama wa muda mrefu uliokuwepo baina yao.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa Rwanda na Marekani umekuwa ni wa mashaka, baada ya Rais Paul Kagame kuhusishwa na matukio mbalimbali ya kihalifu, yakiwamo mauaji ya wanasiasa wa upinzani pamoja na uchochezi wa vita katika eneo la Mashariki mwa Kongo.

Licha ya kukana kufadhili waasi wa M23, mwaka jana Rais Barack Obama alimuonya Kagame kuacha mara moja kuchochea mapigano Mashariki mwa Kongo.

Katika hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni katika ibada ya kuliombea taifa hilo, Rais Kagame alitoa onyo kali kwa watu wanaoisaliti nchi hiyo kwamba watakabiliwa na wakati mgumu popote watakapokuwa.

Rais Kagame aliwataka Wanyarwanda wote kuungana katika kusimamia misingi sahihi na msimamo wao kama taifa, bila kujali tetesi zinazotoka katika mataifa ya nje kuhusu wale waliotangaza kuisaliti Serikali yake.

Hata hivyo, hakutaja moja kwa moja kuhusu tuhuma zinazoikabili Serikali yake juu ya mauaji ya aliyewahi kuwa Mkuu wake wa Ujasusi, Karegeya, ambaye ameuawa Januari Mosi, mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo wa Rwanda, alitoa onyo kali kwa kusema kuwa wale wote wanaoigeuka nchi yao na kuchagua kuua raia wasio na hatia kwa sababu zao binafsi, wanastahili kushughulikiwa ipasavyo.

Akisisitiza maelezo hayo, Kagame alisema hatakuwa na huruma na watu ambao wanasahau namna Rwanda ilivyowatengeneza hadi kufika mahali walipo.

Rais Kagame, aliwataka viongozi wa Rwanda kutosumbuliwa kwa yanayowakuta ‘maadui wa taifa', kwa kuwa Mungu aliwapa nguvu ya kujenga na kukilinda kile walichokijenga, hivyo wale wanaosahau kwamba wana dhamana kwa Wanyarwanda na kuamua kutenda mambo mabaya dhidi ya taifa lao, ni wazi kwamba wamesahau kuwa hawataweza kuwa juu ya watu wao.

"Mliponiapisha kuwa kiongozi wenu mliniagiza kwamba wakati wote niilinde nchi hii, kwa maana ya kusimama kwa ajili ya watu wake," alisema.

Hotuba hiyo iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa watu ambapo wengi wao waliitafsiri kama ni ujumbe wa kilicho nyuma ya utata wa kifo cha Karegeya.

Kanali Patrick Karegeya (53), ambaye alikuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini kwa miaka kadhaa, baada ya kutofautiana na mkuu wake wa zamani, Rais Kagame, aliuawa na watu wasiojulikana ambapo mwili wake ulikutwa katika Hoteli ya Michelangelo Towers, nchini Afrika Kusini.

Ikumbukwe kuwa Kanali Karegeya aliongoza Idara ya Usalama ya Rwanda kwa muda mrefu na alikuwa ni mtu aliyeaminiwa kwa kiasi kikubwa na Rais Kagame.

Hata hivyo, kiongozi huyo alijikuta akiingia katika uadui mkubwa hata kudaiwa kuwa Ofisa Usalama huyo alikuwa akiandaa mikakati ya kumpindua Rais Kagame.

Uadui huo haukuishia kwa Karegeya pekee, bali hata aliyekuwa Mkuu wa zamani wa Jeshi la nchi hiyo, Faustin Kayumba Nyamwasa na washirika wake, walikumbwa na hali hiyo, hivyo kuwalazimu kuikimbia nchi yao.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikilaumiwa kwa kuwaua baadhi ya wanasiasa mashuhuri nchini humo, kama John Sengati, aliyeuawa nchini Rwanda, Kanali Theoneste Lizinde na Waziri wa zamani wa Rwanda, Seth Sendashonga waliouawa nchini Kenya.

Wengine ni Kanali Shabani Rutayisire, Gratien Munyarubuga, Dk. Assiel Kabera na Andre Kagwa Rwisereka ambao waliuawa nchini Rwanda.

Pia Regina Uwamaliya na Juvenal Uwilingiyimana nao waliuawa nchini Ubeligiji, huku Charles Ingabire akiuawa mjini Kampala na Pasteur Musabe aliyeuawa Cameroon.

Mpaka sasa kumekuwa na taarifa tofauti kuhusu kukamatwa kwa watu wanaoshukiwa kuhusika na kifo hicho, huku baadhi ya vyanzo vikimtaja mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa Rwanda, Apollo Gafaranga, ambaye alidaiwa kujenga urafiki wa karibu na marehemu Karegeya.

Oktoba mwaka jana, aliyekuwa mlinzi mkuu wa Rais Paul Kagame, Luteni Joel Mutabazi, alitekwa na kikosi cha Jeshi la Uganda na kukabidhiwa kwa Serikali ya Rwanda.

Luteni Mutabazi alikimbilia nchini Uganda Oktoba 2011, baada ya kufanikiwa kutoroka jela yenye ulinzi mkali wa kijeshi, iliyo katika mji wa Kami, nje kidogo ya mji wa Kigali, akituhumiwa kwa kuhusishwa na kutoroka kwa mkuu huyo wa majeshi na kukimbilia Afrika Kusini.

Mlinzi huyo pia anashutumiwa na Serikali ya Rwanda kwa kutoa siri kwa Kikosi Maalumu cha Umoja wa Mataifa chini ya Majeshi ya Umoja wa Kulinda Amani nchini Kongo, (MONUSCO) na kuwezesha kuchakazwa na kushindwa kwa kikosi cha waasi wa M23.


010812.jpg
 
Ipo siku huyu blood sucker damu yake nayo italambwa na wanyama wa mwituni...
 
Tanzania hatupashwi kuwa na ushirikiano na huyu Kagame ambaye ni muuaji mkubwa wa binadamu wenzake. Ushirikiano wetu na huyu mtu kwa sasa lazima uchukuliwe kwa tahadhari kubwa. I will hate this Man (Monkey) forever.
 
huyu jamaa atakuja kufa kifo kibaya sana!

Mkuu PK ni kitu kidogo sana, tatizo ni kuwa wanyarwanda watabai katiaka hali gani baada ya yeye kuondoka. Jamaa anapanda mbegu mbaya sana. Tatizo ni kuwa watu hawataki kukubali ukweli huu. Tanzania kuna hard evidence nyingi sana za mambo anayofanya PK, yakijawekwa hadhari itakuwa mshikemshike, lakini issue kubwa kwa sasa ni future ya wanyarwanda hasa pale watakapoanza kudeal na post PK time. Kuna watu wanaonekana kuwa PK will live forever, kitu ambacho ni cha ajabu sana.
 
As long as he's doing a lot of good for his country, I really don't care about huo ukabila. Ninyi msiokuwa na ukabila mko wapi?
```
Hakuna kitu kizuri katika maisha ya binadamu kama kuishi kwa amani na kutonyanyasika katika nchi,tena na mgeni!go to hell cocroach!
 
Mkuu PK ni kitu kidogo sana, tatizo ni kuwa wanyarwanda watabai katiaka hali gani baada ya yeye kuondoka. Jamaa anapanda mbegu mbaya sana. Tatizo ni kuwa watu hawataki kukubali ukweli huu. Tanzania kuna hard evidence nyingi sana za mambo anayofanya PK, yakijawekwa hadhari itakuwa mshikemshike, lakini issue kubwa kwa sasa ni future ya wanyarwanda hasa pale watakapoanza kudeal na post PK time. Kuna watu wanaonekana kuwa PK will live forever, kitu ambacho ni cha ajabu sana.
Mkuu maisha ya wanyaruanda yapo mikononi mwa Mungu!huyu PK aende kuzimu na Rwanda itabaki salama!
 
Mkuu maisha ya wanyaruanda yapo mikononi mwa Mungu!huyu PK aende kuzimu na Rwanda itabaki salama!

If you listen to the rhetoric from Rwanda you wonder whether some people's brains down there have "ceased" to work. I applaud PK's work, but looking ahead to post PK era, i see very dark cloud. Looks like there is nothing like post PK Rwanda.
 
If you listen to the rhetoric from Rwanda you wonder whether some people's brains down there have "ceased" to work. I applaud PK's work, but looking ahead to post PK era, i see very dark cloud. Looks like there is nothing like post PK Rwanda.

I think post PK-Rwanda will be just fine
 
kwa marekani tu amegusa pabaya hajui kuwa hili taifa ni mzee wa kaya wa dunia si dhani kama atavuka miezi mitatu kabla hajashambuliwa na vikosi vya marekani vyenye ndege zisizokuwa na rubani nakuhukumiwa adhabu ya kifo kulingana na aliyoyafanya duniani.Asifikili kunanchi itadhubutu kutoa msaada.
 
wamarekani nao huwa hawaeleweki, subiri aje rais mwingine kutoka republican unaweza kuona rangi nyingine!
 
Huyu jamaa ni mkabila wa nguvu sana!wahutu hawana furaha kabisa ndani ya nchi yao!

Uliwahi kuishi Rwanda au unatoa Mawazo yako kwa kufikirika lkn huna uhakika na ulichokiandika mkuu.
Rwanda hakuna ukabila kwa sasa . na ukitaka ukimbizwe Rwanda nenda huko uanze kuuliza eti wewe kabila gani.
Hata baada tu ya vita, miaka miwili baada ya vita nilikuwa Rwanda . hivyo naongea kwa uhakika.
Nilikuwa Nyamirambo, baadae kachikilo(handiwork hivyo) ,na mwisho niliishi Butale matyazo avenue.usije ukazungumza ukabila kule.
 
I think post PK-Rwanda will be just fine

Thinking is one thing, and what may come is quite the other. Siku zote unachopanda ndio utakachovuna. Watu hawawezi kuendelea kuwa wajinga siku zote. If you terrorize people it is very possible that they may take action, and that does not mean just fine.
 
Ni kweli rwanda hawatamki wewe ni kabila gani ila ni wabaguzi kwa vitendo na si kwa kuulizana wewe kabila hili nililishuhudia mwenyewe kwan mimi ni mtu kutoka kaskazin mwa Tz na watu wa kule wapo wanafanana na wasomali hivyo nilipofika kule walijua mimi m2c hapo ndipo nilishuhudia utofauti wa mimi na mwenzangu niliekuwa naye yeye hawakumfurahia kama mm hata katika huduma.hivyo basi ukabila upo rwanda kwa asilimia kubwa
 
Thinking is one thing, and what may come is quite the other. Siku zote unachopanda ndio utakachovuna. Watu hawawezi kuendelea kuwa wajinga siku zote. If you terrorize people it is very possible that they may take action, and that does not mean just fine.

Huyu Paul Kagame jamani ni hatari sana!, uhatari wake sio tu kwa hao Wanyarwanda ndugu zake anao waua bali pia ni hatari kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati. Ambaye haamini naomba achue muda ajifunze juu huu ndugu aanze na historia yake, mikakati yake, washirika wake, bila kusahau malengo yake(yao). Hata sisi wabongo hatupo salama ikiwa mikakati yake tusipo ingilia kati kuiharibu kwa gharama yoyote!. Nilicho jifunza zaidi juu ya Kagame na washirika wake popote walipo duniani wana uwezo wa kuiaminisha Dunia, kitu cha uongo kikawa kweli na kitu cha ukweli kikawa uongo na hatari zaidi, kila eneo muhimu kitaifa na kimataifa kuna watu wake(wao) wanao julikana na wasiojulikana kwa lugha nyepesi na weza sema hivyo!.
 
Back
Top Bottom