Marekani yalegeza vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei

Marekani yalegeza vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei

😀😀Donald Trump sio wa kuingia kwake kichwa kichwa, hili ni tusi kubwa sana kwa wachina. Alichofanya ni kama kunyang'anya bakuli la cha kula cha mbwa ili aone mbwa atavyolilia msosi then anamwaga chini chakula cha kwenye bakuli kwa masharti mapya mbwa amalize msosi wa sakafuni ndani ya sekunde 90.

Huyu mzee sio wa kuingia 18 zake, haya sasa China pindeni shingo muanze kula chakula cha sakafuni fasta kabla sekunde 90 hazijaisha
Ukumbuke kuwa Huawei anatumia tecnolojia ya 5G hadi serikali ya Uingereza imempa tenda ya kuweka minara ya 5G, hata huko USA kuna taasisi za serikali zilikuwa zimeipa tenda hiyo kampuni katika mawasiliano kwahiyo msidhani Huawei ni kampuni ya mchezo
 
Ukumbuke kuwa Huawei anatumia tecnolojia ya 5G hadi serikali ya Uingereza imempa tenda ya kuweka minara ya 5G, hata huko USA kuna taasisi za serikali zilikuwa zimeipa tenda hiyo kampuni katika mawasiliano kwahiyo msidhani Huawei ni kampuni ya mchezo
Kwahiyo marekani hana technology ya 5G?
 
Serikali ya Marekani yalegeza kwa muda vikwazo vya kibiashara ilivyoweka wiki iliyopita dhidi ya kampuni ya simu ya China Huawei, hatua inayolenga kupunguza hali ya kuvurugwa wateja wake.

Hatua hiyo hata hivyo imepuuziliwa mbali na muasisi wa kampuni hiyo anayesema kuwa Huawei ilikuwa imejiandaa kwa hatua ya Marekani.

Wizara ya Biashara ya Marekani itairuhusu kampuni ya Huawei kununua bidhaa zinazotengenezwa Marekani kwa siku nyingine 90 ili kudumisha mitandao iliyopo na kutoa programu tumishi mpya kwa simu za sasa za Huawei.

Kampuni hiyo kubwa kabisa duniani ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu bado imezuiwa kununua vifaa kutoka nchini Marekani vya kutengenezea bidhaa mpya bila idhini za leseni ambazo kuna uwezekano kuwa zitakataliwa.

Serikali ya Marekani ilisema iliweka vikwazo hivyo kwa sababu ya Huawei kujihusisha na shughuli zinazoenda kinyume na usalama wa taifa au maslahi ya sera za kigeni.


DW

anacho fanya USA sio makusudi,ni kutokana soko ambalo mbeleni linaweza kumfanya sio jipya katika kutetea kampuni zake za ndani,ni wazi kampuni nyingi za USA ziliisha anza kulalamika kwenye vikao vingi vya wazi si kwa kuonesha vikipinga china,kurudisha mifumo yao ya utengenezaji nyumbani mfano apple na n.k,hili kutetea maslahi yake hutengeneza mvutano kuwa huawei ina sehemu hatarishi kwa marekani wakati kalibia kampuni 33 zinazo tengeneza vifaa umeme vya ndani vipo malekani kama qualcomm,broadcom,chip network,intel.
unajua mfano sawa na umemkaribisha mtu kijiji kwenu halafu kila siku hana kuzidi wakati wewe unafanya hicho hicho tena anaongeza mara mbili yake unatarajia nini.
 
Wacha waanze kuminyana wao kwa wao wakati sisi tunaanza kupanda kiuchumi. Nina imani ipo siku tutawapita wote kama wamesimama
Si rahisi kihivyo kwa ya uchumi wetu na itatuchukua mda wa miaka mingi kuwazid uelewe mwaka 2017 china ilikuwa na zaidi ya viwanda laki tatu,ili tufanikiwe lazima tuwe na idadi kubwa ya viwanda vyetu
 
Tunasubiri kuona mshindi katika vita hii. Sidhani kama atakuwa Marekani.
 
Back
Top Bottom