Marekani yakana kuhusika na mapinduzi Uturuki

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
6,892
2,000
Kerry.jpg

Marekani imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameutaka utawala nchini Uturuki kuheshimu sheria wakati wa uchunguzi wao kuhusu mapinduzi hayo.
Kerry amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika mapinduzi hayo inasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa NATO.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika mapinduzi hayo inasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa NATO.

Mapema kupitia kwa hotuba yake, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitoa wito kwa rais Obama kumrejesha nchini humo kiongozi wa kidini raia wa Uturukli anayeishi nchini humo Fethullah Gulen ambaye analaumiwa kwa kupanga mapinduzi hayo.
Bwana Gulen anayakana hayo.

Marekani inasema kuwa Uturuki ni lazima ithibitishwa hayo kabla ya uamuzi wa kumrejesha Gulen kufanyika.

Mapema nchini Uturuki maelfu ya watu walijitokeza wakiimba na kupeperusha bendera ya taifa katika barabara za mji wa Istanbul na Ankara kumuunga mkono rais Erdogan.
Bustani nyingi mjini Istanbul zilijaa watu waliokuwa wakiimba wakisema kuwa ardhi yao na demokrasia haviwezi kuchukuliwa na jeshi.

Bustani nyingi mjini Istanbul zilijaa watu waliokuwa wakiimba wakisema kuwa ardhi yao na demokrasia haviwezi kuchukuliwa na jeshi.

Serikali imetawaka wafuasi wake kusalia katika bustani kuu usiku kucha. Mashirika kadha ya ndege yalirejea safari zao kwenda Istanbul Jumamosi jioni.

CHANZO: BBC
 
Fundi chupi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
344
250
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
Uturuki baby
USA grandfather
 
bampa 2 bampa

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
236
500
Hizo helkopta 42 ambazo hazionekani na zilikuwa kwenye kambi ambayo ndio kuna wanajeshi wamarekan huoni kwamba kunakitu au unafikiri watakubali tu haraka
 
Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,431
2,000
Wanahusukia.. huyo sheikh Fethullah anafanya nini huko marekani kama siokuleta udakuz
 
nyiudanyuki

Member
Jul 17, 2016
7
45
cku hizi kila conspiracy basi marekan yuko behind......mbn turkey ina historia ya mapinduzi mengi tu hapo kabla
Me nadhani kutokana na tabia yake ya urealist ambayo ni nchi nyingi zenye uwezo zina tabia kama hizo. Ila marekani ni too much. He is greedy, uncouth in nature, selfish and vita kwake ndio suruhisho la kupata interests zake. Lisemwalo lipooo kwanini ulaumiwe wewe katika kila kituuu???
 
mair erasto

JF-Expert Member
Jul 13, 2016
413
500
hao waturuki kwanini wasiseme aliye husika hapo ni mrusi? kwasababu mrusi ndio walikua na ugomvi naye. kwasababu uturuki alilipua ndege ya urusi na
putin alisema ile gharama ya ndege watakuja kuilipia kwamna yoyote ile unaweza ukute hizo ndio gharama zake. za kumchokoza mbabe.

lakini hapo kwa mmarekani unaweza ukute wanamuonea kwasababu alikua hana ugomvi naye.
 
nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
6,062
2,000
Me nadhani kutokana na tabia yake ya urealist ambayo ni nchi nyingi zenye uwezo zina tabia kama hizo. Ila marekani ni too much. He is greedy, uncouth in nature, selfish and vita kwake ndio suruhisho la kupata interests zake. Lisemwalo lipooo kwanini ulaumiwe wewe katika kila kituuu???
yeah cjakataa kuwa iko hvyo but uwepo wa marekan usiwafanye watu wawe wavivu wa kufikiri coz nowdays imekuwa ikitokea kitu chochote ambacho watu hawakielewelew watakwambia itakuwa US tu hiyo
 
DesertStorm

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
2,048
2,000
hao waturuki kwanini wasiseme aliye husika hapo ni mrusi? kwasababu mrusi ndio walikua na ugomvi naye. kwasababu uturuki alilipua ndege ya urusi na
putin alisema ile gharama ya ndege watakuja kuilipia kwamna yoyote ile unaweza ukute hizo ndio gharama zake. za kumchokoza mbabe.

lakini hapo kwa mmarekani unaweza ukute wanamuonea kwasababu alikua hana ugomvi naye.

Wabongo mnajua ku-make maneno sio mchezo! Uturuki alishamlipa tayari puttin, Puttin ameshazipokea hizo pesa na ameshamsamehe tayari!

Hivyo US kilaza anahusika %100 Percent utake usitake, na usipende kuropoka kama hao wenzako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom