Echolima1
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 9,000
- 7,618
Jeshi la Marekani "limekamilisha" awamu mpya ya mashambulizi nchini Iran, likipiga zaidi ya maeneo 80, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumanne usiku na US Central Command. Marekani pia imerejesha tena vikwazo dhidi ya mauzo ya mafuta ya Iran kama kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara karibu na Lango la Hormuz.
Huku mkataba wa kusitisha mapigano kati ya nchi hizo mbili ukiwa unazidi kulegalega, Iran mapema leo Jumatano imeonya kwamba itatoa "jibu la kishindo" kufuatia mashambulizi hayo ya Marekani. ambapo tayari mifumo ya ulinzi wa anga iliamshwa huko Bahrain na Kuwait.
Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimeripoti milipuko kwenye kisiwa cha Kharg, ambacho ni kitovu kikubwa cha mauzo ya mafuta ya Tehran, pamoja na miji ya bandari ya Bandar Abbas na Sirik, na kwenye Kisiwa cha Qeshm. Mashambulizi haya yametokea wakati huu ambao Iran inafanya mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wao.
Usalama katika Lango la Hormuz unatarajiwa kujadiliwa na Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na viongozi wengine wa NATO wanapokutana mjini Ankara, Uturuki.
----
Mawimbi ya ziada ya mashambulizi ya anga ya Marekani yalifanywa nchini Iran.
Marekani iliziarifu nchi za Ghuba kuhusu umuhimu wa kujiandaa kwa uwezekano wa Iran kuchukua hatua katika saa zijazo.