Marekani yajuta kuwaua wanajeshi wa Syria

kiki255

New Member
Joined
Sep 18, 2016
Posts
3
Reaction score
2
Marekani imesema inasikitika juu ya shambulio lililoongozwa na ndege zake za kivita ambapo, bila kukusudia zililipua kambi za wanajeshi wa Syria.

Wakati huohuo Marekani imekosoa Urusi kwa kuitisha mkutano maalumu wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ikisema hatua hiyo ya Urusi kutaka kuwakosoa Marekani bila sababu maalumu.

Urusi inasema kuwa wanajeshi 60 wa Syria waliuawa katika shambulio hilo la Kaskazini Mashariki mwa Syria.

Makao Makuu ya Kijeshi yanasema kuwa ndege hizo zilidhania kuwa zilikuwa zikishambulia kambi za makundi ya Islamic State, ambazo Marekani ilisema zilikuwa zikitafuta kwa siku kadhaa.

Lakini Urusi inasema kuwa Marekani walikuwa na lengo la kuwasaidia wanachama wa Islamic State na kuongezea kuwa mapatano yake na Marekani kuhusiana na usitishaji wa mapigano umehatarishwa.
Hakuna habari za kuthibitisha idadi ya watu waliouawa.

Chanzo: BBC
 
May be they done it purposeful ili vita isiishe, because i think wanafaidika sana vita iki going on
 
Hakuna cha bahati mbaya wala nini sijui, walishambulia jeshi la Syria kwa kushtukiza wakiwa na lengo la kuwasaidia waasi, ndiyo maana baada ya mashambulizi ya ndege na Drone za Merikani na Uingereza waasi walianzisha a massive mashambulizi dhidi ya Jeshi la Syria, which means mashambulizi ya ndege yalikuwa coordinated na waasi na inadaiwa na Jeshi la Syria kwamba Daesh/waasi ndiyo walihusika kuongoza ndege wapi pa kushambulia - walipewa vifaa vya kuongozea na washirika wa NATO.
 
May be they done it purposeful ili vita isiishe, because i think wanafaidika sana vita iki going on

Wanacho tafuta hasa hasa ni kumuondoa madarakani Rais wa Syria na kusimika ma puppet watakao kubaliana na Merikani na Nchi ya Qatar kujenga bomba la gesi kupitia Syria, Uturuki kwenda Ulaya!!

Baada ya Asaad kuwakatalia US ujenzi wa bomba la gesi kupitia nchini mwake ndiyo wakabuni njama za kutaka kumpindua kwa kupitia waasi - yaani wazungu wako radhi kuanzisha uaasi/vita kuua watu innocent kwa kitu kidogo kama ujenzi wa bomba la gesi, hawataki Urusi iendelee kuuza gesi nchi za Ulaya!!
 
Uko sawa kabisa mkuu, lengo la Marekani ni kuidhoofisha Urusi kiuchumi, Kwa Sababu mauzo ya gesi yanaibusti Sana urusi kiuchumi Kwa hali, Urusi haitakubali maana tayari inaujua mchezo wa marekani na Vita Syria haitaisha.
Rejea neno la Mungu ktk utabiri wa nabii isaya, Ole wako Damascus maana mjini wako utakuwa magofu.
 
Mamboo ya east+west+middle +korea
Yaan israel+USA+RUSSIA+IRAN+NORTH KOREA+IRAQ+SYRIA- Ni kama mambo ya ngoswe,
 
Uzuri wamkubali kuwa wamestriie kwa bahat mabaya sio kama wale wanaoshambilia allepo na kuua watu kila cku picha znasambaa kwe mitandao but hutowackia hata cku moja wamekiri..wao wanasema tangu waanze mashambuliz ya anga hakuna raia waliomuua
 
Sasa mbona urusi inapopiga wale waasi wanaompinga Asadi hamkemei..! Maana obvious marekani anawasupport ukiacha ISIS

Mkuu Bigmind, kumbuka Syria ni nchi huru na Rais aliyepo madarakani anakubalika ni wananchi wengi nchini Syria, alichaguliwa kidemokrasia kwa kupigiwa kura, sasa Nchi za NATO zina mmlaka gani ya kutaka/shinikiza mapinduzi kwa nchi ambazo hawazipendi kutoka na na uchu wao wa kimaslahi binafsi.

NATO wanapiga mabom majeshi ya Syria bila sababu, hakuna aliyewapa kibali cha kushambulia nchi huru, Umoja wa Mataifa ndiyo wenye mamlaka ya kuidhinisha mashambulizi kama kuna sababu za msingi kufanya hivyo - cha ajabu NATO haikupewa kibali na Umoja wa Mataifa kuishambulia Syria, NATO walitumia jeuri yao ya nguvu za kijeshi na kifedha wanajiamulia kuua watu wasio na hatia nchini Syria!!

Urusi wao ni tofauti kidogo, wanafuata sheria za Kimataifa, jeshi lake la anga linatumika kushambulia waasi baada ya kuombwa na Serikali ya Syria kutoa msaada kijeshi, Syria ilifikia hatua ya kuomba msaada kutoka Urusi baada ya kuzidiwa nguvu na waasi wanao saidiwa na nchi zinazo hunda NATO.

Urusi imejitolea kuwangamiza magaidi wanao sumbua Ulimwenguni, hakuna Taifa ambalo linaweza kujidai kwamba haliwezi kushambuliwa na waasi, hata Merikani nayo juzi juzi hapa imeshambuliwa na waasi na sina shaka wapo waasi wengi nchini humo wanao ishi kama sleeper cells, siyo kwamba wanahibuka tu from nowhere - tatizo wenzetu hawa (USA) jeuri yao haiwafunzi kitu, badala ya kushirikiana na Warusi katika harakati za kuangamiza magaidi ambao ni tishio hata kwa Taifa lao, wao wanaedelea kufanya hujuma ili Warusi washindwe katika harakati yao ya kusambaratisha magaidi.

US hawana hata aibu wanaedelea kushirikiana na magaidi kama Daesh/ISIS nk wanawapa silaha, fedha na mafunzo baadae waasi hao hao wanawageuzia kibao Wamerikani kwa kutumia silaha walizo pewa na USA kushambulia Wamerikani, nchi za Ulaya, Urusi na Uchina - yaani watawala wa Merikani unaweza kufikiri ni kichwa cha mwenda wazimu, hawatafakali mambo kiundani kabla hawajatenda - adventures zao zote walizo wahi kutekeleza, hakuna hata moja waliwahi kufanikiwa au kurudisha amani ya kudumu, kila walipo kwenda vurugu,ukosefu wa amani na vilio ufuata nyuma!

Chukulia mifano ya:Afghanistani huu ni mwaka wa kumi na tano je nchi hiyo ina amani gani, Libya, Iraq huu mwaka wa ngapi - juzi nimesikia US atapeleka ndege Monsul kusaidia Jeshi la Iraq kupigana na ISIS, yaani waasi wanaopewa msaada na the US huko Syria ndiyo anataka tena kupigana nao nchini Iraq!!!
 
Uzuri wamkubali kuwa wamestriie kwa bahat mabaya sio kama wale wanaoshambilia allepo na kuua watu kila cku picha znasambaa kwe mitandao but hutowackia hata cku moja wamekiri..wao wanasema tangu waanze mashambuliz ya anga hakuna raia waliomuua
U..S.A bwana hahah
 
Wanacho tafuta hasa hasa ni kumuondoa madarakani Rais wa Syria na kusimika ma puppet watakao kubaliana na Merikani na Nchi ya Qatar kujenga bomba la gesi kupitia Syria, Uturuki kwenda Ulaya!!

Baada ya Asaad kuwakatalia US ujenzi wa bomba la gesi kupitia nchini mwake ndiyo wakabuni njama za kutaka kumpindua kwa kupitia waasi - yaani wazungu wako radhi kuanzisha uaasi/vita kuua watu innocent kwa kitu kidogo kama ujenzi wa bomba la gesi, hawataki Urusi iendelee kuuza gesi nchi za Ulaya!!
Umenikumbusha kuhusu Rwandan genocide!
Anzisha uasi, wahanga wawe innocent civilians ili upate njia ya kuingia Congo DR ili ukapore madini!
 
Ukifatilia mambo utakuta walio mfundisha PK mbinu hizo na William Clinton na John Blair - ni marafiki wake wa karibu mpaka leo, Bill Clinton kwa mfano alinunua nyumba huko Rwanda, kwa nini!!

Hillary Clinton akishida kinyanganyiro cha Urais nchini mwao, basi vurugu ndani ya DRC zitalipuka upya na uporaji wa mali asili utarudi pale pale. Au utamsikia mama huyo akisema Congo ni nchi kubwa mno ingawanywe kama Sudan ili Kivu iende Rwanda na kasikasini Uganda, atajaribu kupiga debe hilo kutokana na shinikizo la PK don't you underrate PK ana mbinu nyingi sana - Clintons wana mawazo ya ajabu sana, wanataka ni Syria inagawanywe - akishinda Urais Dunia itavurugika sana.
 
Mkuu Bigmind, kumbuka Syria ni nchi huru na Rais aliyepo madarakani anakubalika ni wananchi wengi nchini Syria, alichaguliwa kidemokrasia kwa kupigiwa kura, sasa Nchi za NATO zina mmlaka gani ya kutaka/shinikiza mapinduzi kwa nchi ambazo hawazipendi kutoka na na uchu wao wa kimaslahi binafsi.

NATO wanapiga mabom majeshi ya Syria bila sababu, hakuna aliyewapa kibali cha kushambulia nchi huru, Umoja wa Mataifa ndiyo wenye mamlaka ya kuidhinisha mashambulizi kama kuna sababu za msingi kufanya hivyo - cha ajabu NATO haikupewa kibali na Umoja wa Mataifa kuishambulia Syria, NATO walitumia jeuri yao ya nguvu za kijeshi na kifedha wanajiamulia kuua watu wasio na hatia nchini Syria!!

Urusi wao ni tofauti kidogo, wanafuata sheria za Kimataifa, jeshi lake la anga linatumika kushambulia waasi baada ya kuombwa na Serikali ya Syria kutoa msaada kijeshi, Syria ilifikia hatua ya kuomba msaada kutoka Urusi baada ya kuzidiwa nguvu na waasi wanao saidiwa na nchi zinazo hunda NATO.

Urusi imejitolea kuwangamiza magaidi wanao sumbua Ulimwenguni, hakuna Taifa ambalo linaweza kujidai kwamba haliwezi kushambuliwa na waasi, hata Merikani nayo juzi juzi hapa imeshambuliwa na waasi na sina shaka wapo waasi wengi nchini humo wanao ishi kama sleeper cells, siyo kwamba wanahibuka tu from nowhere - tatizo wenzetu hawa (USA) jeuri yao haiwafunzi kitu, badala ya kushirikiana na Warusi katika harakati za kuangamiza magaidi ambao ni tishio hata kwa Taifa lao, wao wanaedelea kufanya hujuma ili Warusi washindwe katika harakati yao ya kusambaratisha magaidi.

US hawana hata aibu wanaedelea kushirikiana na magaidi kama Daesh/ISIS nk wanawapa silaha, fedha na mafunzo baadae waasi hao hao wanawageuzia kibao Wamerikani kwa kutumia silaha walizo pewa na USA kushambulia Wamerikani, nchi za Ulaya, Urusi na Uchina - yaani watawala wa Merikani unaweza kufikiri ni kichwa cha mwenda wazimu, hawatafakali mambo kiundani kabla hawajatenda - adventures zao zote walizo wahi kutekeleza, hakuna hata moja waliwahi kufanikiwa au kurudisha amani ya kudumu, kila walipo kwenda vurugu,ukosefu wa amani na vilio ufuata nyuma!

Chukulia mifano ya:Afghanistani huu ni mwaka wa kumi na tano je nchi hiyo ina amani gani, Libya, Iraq huu mwaka wa ngapi - juzi nimesikia US atapeleka ndege Monsul kusaidia Jeshi la Iraq kupigana na ISIS, yaani waasi wanaopewa msaada na the US huko Syria ndiyo anataka tena kupigana nao nchini Iraq!!!

ImageUploadedByJamiiForums1474416671.289519.jpg
 
Uzuri wamkubali kuwa wamestriie kwa bahat mabaya sio kama wale wanaoshambilia allepo na kuua watu kila cku picha znasambaa kwe mitandao but hutowackia hata cku moja wamekiri..wao wanasema tangu waanze mashambuliz ya anga hakuna raia waliomuua
nenda kashambulie kambi za kijeshi za wamarekani afu utoke na msemo kuwa ilikuwa bahati mbaya uone kitakacho fuatia.
 
Last week US aliua Syrian Troops waliokuwa kambini, halafu US wakasema "Bahati mbaya"... Sasa kwa kuwakomesha, Putin nae Kaua hao U.N. Convoy halafu kasema "Hatuusiki"

Equation balanced and kwa hiyo Sasa hivi wako evenly.
 
Mpaka leo sijui sababu gani inayowafanya Wamerakani na Warusi kuendelea kuwepo Syria.
Kwani wakiondoka kuna madhala gani?
Kwani ni lazima kwa kila Taifa kufuata utawala wa kidemokrasia?
Vipi kuhusu urithi wa dunia wa mji/jiji la Damascus?
Au ndio tunavyoita kutimia kwa /kutimiliza maandiko katika vitabu vitakatifu?
 
Back
Top Bottom