Hivi hata Marekani haijui nani yuko nyuma ya migogoro ya Zanzibar na yupi wa kumuona? Kuonana na Naibu katibu mkuu wa ccm , Abdalla Juma,Kada ambae yeye mwenyewe hajitambui ambae hawashi hazimi, haongezi wala hapunguzi ni sawa na kudanganya toto. Tatizo sio CCM Zanzibar, tatizo ni mtawala Tanganyika. Kumbuka aliekuwa Naibu katibu mkuu wa ccm Ali Vuai amepoteza nafasi yake kwa kukiri tu, kuwa Maalim Seif ameshinda na apewe Serikali. Kauli hiyo ilimponza na Mtawala Tanganyika ikamsubiri akanyage ardhi ya Dodoma,machinjioni ya wana CCM Zanzibar na kumalizwa.
Kama kweli Bwana GREGORY SIMPKIMS,ofisa wa Masuala ya sera za kijamii na kisiasa au Serikali ya Trump ina utashi wa kutatua migogoro hii ya kila uchaguzi Zanzibar, basi angeonana na Rais JPM na wazo la kuitisha kura ya maoni kama wazanzibari wangependa kuendelea kubaki kwenye ukoloni wa Tanganyika au kujitenga nayo.