Marekani yaionya Syria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani yaionya Syria

Discussion in 'International Forum' started by sulphadoxine, Jun 24, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Marekani imeeleza wasiwasi wake juu ya taarifa kuwa Syria inapeleka vikosi vyake katika mpaka wao na Uturuki, na kuonya kuwa huenda kukawa na mapigano zaidi.
  Waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton amesema hatua hio ya majeshi ya Syria "inatia wasiwasi".
  Anasema hali hii huenda ikasababisha kukithiri kwa mapigano kati yao na Uturuki na kuwaweka wakimbizi katika mazingira magumu zaidi.
  Imeripotiwa kuwa vifaru vya kijeshi vya Syria vimeonekana vikiingia katika kijiji cha Khirbet al-Jouz,kulazimisha wakaazi kukimbia hadi nchi ya Uturuki.
  Zaidi ya watu 1,300 wameuawa tangu kuanza wa makabiliano dhidi waandamanaji wanaopinga utawala wa Syria mwezi Machi.
  Maelfu ya waandamanaji wamekamatwa, wanaharakati wa upinzani wanasema.
  Miji mingine ya Syria - ikiwemo Homs na Hama - imetangaza mgomo baada ya makabiliano na maafisa wa usalama pamoja na wanaomuunga mkono Rais Bashar al-Assad mapema wiki hii.
  [h=2]'Ukatili'[/h][​IMG] Wakimbizi wa Uturuki wakisubiri kuingia nchini Syria


  " Kama ni kweli, basi hatua hio itafanya hali ya wakimbizi nchini Syria kuwa mbaya zaidi," Clinton alisema Alhamisi jioni.
  " Hadi pale vikosi vya Syria vitakapositisha mashambulio na ukatili ambayo sio tu yanawaumiza raia wake wenyewe bali hata kuzidisha mapigano katika mpaka, basi tutaona machafuko yakiongezeka katika eneo hilo."
  Clinton pia alisisitiza wito wa serikali ya Marekani kwamba Rais Assad atekeleze mabadiliko aliyoahidi au ajiuzulu.
   
Loading...