Marekani vs Zambia

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Habari zenu wana Jamii,kuna habari nimezisikia lkn cna uhakika nazo naomba majibu yenu kwa wanaojua.
Inasemekana kwamba USA walikuwa wanunuzi wazuri sana wa shaba kutoka Zambia kiasi ambacho mpaka Raisi wa nchi hiyo kipndi hiko alikuwa ni K.Kaunda kuwaambia raia wake watakula kuku mpaka basi.
USA nao wanazalisha shaba lkn sio kwa wingi kama ilivyokuwa inatoka Zambia,sasa USA wakawa wananunua na kuhifadhi kwao walipoona sasa wana shaba nyingi wakaamua kuuzima mkataba na Zambia na kushusha bei ya shaba hiyo hiyo kiasi ambacho Zambia akawa hawezi pata faida.
Zambia walipoona kwamba hawana uwezo wa kuendeleza migodi hiyo na kufilisika kabisa,USA akatoa shaba zake alizoweka chimbo na kuzipandisha bei sababu wao peke yao ndio waliokuwa nazo,je?kuna ukweli wowote ktk hilo.
Pia tumeona ni jinsi gani hawa jamaa (USA)wasivyo marafiki wa kweli kwa kumuweka Uchi Mh wa Takukuru(Hoseah),kuivamia Afghanstan,Iraq,Vietnam,kuisambaratisha USSR na sasa wanataka kuwamaliza North Korea na Iran,sikulazimishi uipende/uichukie USA,ni nini hasa lengo la USA ktk Dunia hii?
Je?kila adui/rafiki wa USA ni lazima awe adui/rafiki wa TZ.
Naomba mniweke sawa katika haya
 
Back
Top Bottom