Xavier Africa
Senior Member
- Oct 4, 2017
- 180
- 386
Binafsi nilikwenda USA mwaka 2013 wakati nimemaliza A level kwa mwaliko wa rafiki yangu mmishenari daktari.
Nilikutana nae vipi huyu daktari? Stori inaanzia hapa..
Ilikuwa likizo shuleni na mimi sikutaka kurudi home nilikomaa shule ili nijisomee vizuri.
Sasa nikawa asubuhi naamka napiga zoezi la kukimbia maeneo ya shule (shule ipo jirani na hotel moja ya hivi wazungu wanapenda sana kufikia).
Basi kuna siku nimeamka asubuhi nakimbia nikakutana na huyu babu (75 years) naye anapasha, nikajipendekeza kwa kumsalimia na kukimbia nae huku naongea ongea broken.
Tumekimbia tukamaliza mbio nikarudi nae huku tunatembea ananiuliza uliza maswali nikamwambia mimi Mwanafunzi pale akaniuliza jina nikamtajia haaa akashangaa tumefanana majina akafurahi sana yule mzee, akaniambia jioni atakuja nimngojee uwanja wa mpira.
Basi jioni ikafika nikawa zangu wanjani nikaona hii migari ya watalii inakuja nilivyo tazama nikamuona yeye ndo anaendesha nikamfata tukapiga story huku ananiuliza kuhusu familia yangu akatoa kitambulisho chake akanionesha jina lake nithibitishe kama kweli tumefanana majina.
Baada ya story kuisha akasema kesho juoni atakuja twende hotelini kwao.
ITAENDELEA
INAENDELEA
Basi kesho yake ikafika akaja ila safari hii alikuja na dereva wake mswahili tukapiga story then tukaenda motel yao
ebwana eeh kuingia ndani wamejazana wazungu tupu mweusi nilikuwa mimi yule dereva na wahudumu tu afu wale jamaa ni warefu mimi kajiona ka mende hivi mfupi hatari
ndo kwa mara ya kwanza nikala pizza ila ya kijerumani mana wagen wengi pale walikuwa wajerumani huyu Daktari nae ni mjerumani anaeishi U.S.A
basi mle lugha ilikuwa ni kijerumani sana kingereza huyu mzee na dereva ndo tuliokuwa tunaongea nikanywa na kula night wakanirudisha shule
basi ikawa ni mtindo huo yule mzee akanitambulisha kwa familia yake kama rafiki yangu ana vijana wakubwa tu mpaka tulivyofungua shule nikawa nimepata connection na wazungu wanafunzi wenzangu wakawa wananiuliza nimefahamiana nao vipi hawa jamaa nawazungusha tu bra bra nawaambia mimi siyo mwenzenu mjue hahaha
likizo yao iliisha wakasepa daktari akaniachia mawasiliano nikawa nachat nae kwa email na facebook tu
nilipomaliza shule akaniuliza unataka kuwa nani nikamjibu (japo sijawa nilietaka kuwa)
akanieleza lifani lake analopenda niwe kamwambia kwa masomo niliyosomea siwezi kuwa
nikamwambia mzee nishamaliza shule namimi nataka niwatembelee kwenu Dr Hans hakuwa na hiyana akanikaribisha akanipa ratiba ya lini atakuwa home
nikaanza kufatilia passport japo wasumbufu hao migration nikaipata
nikaenda kufatilia visa ubalozi wa U.S.A nikapewa visa ila baada ya kuwapa barua ya mwaliko wa miezi 3
hela ya ndege kimbembe nilijua hela ndogo kumbe ni mtaji wa boxer kabisa na chenji inabaki
mzee alinitumia hela kupitia western union nikafanya shoping ya nguo kidogo na begi mana anajua kwetu hali ni ngumu kutokana na nilivyo mueleza
nikakata tiketi ya ndege ya shirika moja tukapaa usiku wa saa saba tukatua NAIROBI
baada ya hapo tukaruka hadi instanbul pale nikashuka nikaunga ndege hadi U.S.A ndege ili take off majira ya jioni kama kumi kasoro hivi nilianza kuona maajabu kuanzia pale airport kumejengeka ni hatari ni kubwa na inavutia
mzee alikuja kunipokea na mke wake hata gari walilokuja nalo sikuwahi ona huku
basi tukatoka airport kuelekea mtaani umbali ulikuwa mrefu kidogo tukiwa njiani ushamba ni mzigo sana mimi macho yalikuwa yanashangaa nje tu magorofa ni mengi ni marefu barabara zao zinapendeza hewa ni safi ajabu hakukuwa na baridi wala joto
tukaanza kuingia nje ya mji nyumba zipo smart zinarangi miti imepandwa vizuri mzee akasema mbona huongei unashangaa tu
nikamwambia Dr Hans hivi kama US kupo hivi mbinguni kutafananaje sasa wakabaki wanacheka tu wakasema mbinguni hakuna mfano wake
nikatania kawaambia mimi bora nibaki huku tu hii ndo mbingu yangu
tukafika kwao nyumba za kawaida ramani flani sizielewi ila nmejifunza kila nchi ina mtindo wa nyumba zake kule mijengo mingi ya makazi imefanana
tokea nifike maji umeme havijawahi katika
kadi inatumika sana kuliko cash
kwenye bus unatoa kadi unaingizwa kwa mashine
makanisa mengi yamebaki tupu wale jamaa hawasali kivilee japo wao ndo wametuletea dini
madhehebu mengi yapo kwa race ni marachache kukuta mweusi ndani ya makanisa ya wazungu
japo sikuangalia shughuri za kiuchumi zikoje
ila majumba ya cinema yapo makubwa mlimani city utaiona kama kibanda umiza
watu hawana habari na mtu yani wapo bize
nilikuwa nikitembezwa city center yani mtu akiniona anasema huyu ni wakuja macho ni juu tu magorofa ni marefu ni hatari
NIMESHINDWA KUELEZEA IPASAVYO
ILA POINTI YANGU
ULE MJI NI MZURI NA WA LUXURY MFANO WAKE HAKUNA
HAKUNA
Mende nzi sijui kuku mbuzi anakatisha road ng'ombe sijawah ona kwa miezi 3
na wazungu wanajijua kuingia peponi hawawezi wameamua kutengeneza pepo zao hapa
sisi waafrika tujitahidi kufika peponi maana tunapoishi panahuzunisha sana
ndo maana trump anajua US ni pepo ya dunia kila mmoja ana admire kufika kule so ukileta fyokofyoko anakupiga ban tu
mimi nilitamani nisirudi huku sema hapakuwa na namna tu ilibidi nirudi but nampango masters nikachukulie kule