Sasa ni kujifunga mkanda tu,maana tulizoeleshwa kuishi kibepari.
Kuishi kijamaa na kutumia vya kwetu ndio dawa ya bepari ingawa
hali hii itawaumiza sana wajamaa waliozoeshwa kuishi kibepari.
Kwa nchi huru kama Tanzania kuwekewa vikwazo na wazungu, huo
uhuru tunaouimba kila siku ni danganya toto.
Kuiwekea vikwazo nchi kama Tanzania ni sawa na kuziwekea
nchi majirani zipatazo nane.
Ninachokiona hapa ni uchokozi tu wa wazungu kwa nchi yetu
ili wasikie Mh.Rais Dr.JPM anasemaje/ana maoni gani? a.k.a
kupima upepo wa Amiri Jeshi Mkuu.
Hizi ni dalili za mwisho kabisa za kuparaganyika kwa mifumo yote inayoutegemeza mwili wako ili kuuwezesha kuwa na urari sawa wa kimwili na kiakiri.
Mmarekani hajakurupuka kufikia maamuzi ya kuinyima Tanzania misaada,maamuzi yake ni zao la kiburi cha watawala wetu waliojiapisha kubaki madarakani kwa ghalama yoyote hata kwa kuutoa uhai wa Watanzania.
CCM na serikali yake haipaswi kukimbia kivuli chake,leo hii tunadharirishwa ulimwenguni kwa kuwekwa kwenye kundi la mataifa yasiyofaa kwa sababu tu ya kiumbe kiitwacho shein,eti hicho ni mwiko kwake kuwa nje ya Ikulu.Kwamba ni bora Taifa zima liadhibiwe kuliko mahafidhina na manyang'au ya ccm kupoteza mamlaka za kuikalia Zanzibar kimabavu.
Baada ya MCC kushusha rungu lake,mmeibuka watetezi wengi mkilaani uamuzi wa MCC huku mkijitia upofu na kiburi cha kifisadi kujisahaulisha sababu zilizopelekea Taifa linyimwe huo msaada.
Kwani ni nani kati ya wapumbavu wote waliopo huko serikalini asiyejuwa kuwa ccm imepora haki ya wazanzibar kujichagulia viongozi wanaowataka?Ifike mahali tuache itikadi na tuungane kupinga jeuri za wanasiasa.Bila hofu eti zezeta moja linathubutu kutamka kuwa eti bora tule nyasi kuliko Kupokea misaada yenye masharti?Yaani mbaki madarakani kwa ghalama za Watanzania kula nyasi?
Tuwe wakweli,waliotufikisha hapa ni mainterahamwe wa ccm walioamua kujivika umungumtu na kujimilikisha Taifa letu.
Mliamua kuuminya Uhuru wa habari kwa kisingizio cha makosa ya Mtandao,kama mliona kosa la kimtandao kwa waliokuwa wanafanya Kazi ya kukusanya matokeo ya UKAWA,kwa nini hamkuliona kosa hilo kwa vijana wa IT Masaki waliokuwa wanafanya Kazi ileile iliyokuwa inafanywa na vijana wa ngome wa UKAWA?
Double standard za vyombo vya usalama ndiyo vilivyotufikisha hapa tulipo.Tusimlaumu Mmarekani kwa mapungufu yetu wenyewe,ni maamuzi ya kijinga na kipumbavu kabisa yaliyofanywa na wapumbavu wanaoongoza serikali ndiyo yaliyotufikisha hapa.
Waliopewa dhamana walipigiwa kelele watumie mamlaka waliyonayo kikatiba kuzuia uvunjaji wa demokrasia Zanzibar,lakini kwa kiburi chao na upumbavu wao,walisema kwa dharau kuwa hawaingilii ya Zanzibar,bali wapo tayari kumsambaratisha yeyote atakayeleta fyokofyoko zinazoweza kuathiri chama chao.
Tusipige kelele na kuelekeza chuki zetu kwa Mmarekani,tuangalie wapi tulipojikwaa na si pale tulipoangukia.Kigingi kilichotukwaa na kutusababishia anguko la kunyimwa msaada na Wamarekani ni ccm.Ndiyo,ni ccm kupitia kada wake Jeicher ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.
NB:Maneno "ujinga,upumbavu na ulofa" nimeyaazima toka kwa Mh.B.W.Mkapa.Rais mstaafu wa JMT.