Marekani kuchimba madini kwenye mwezi

ismail hassan

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
685
1,612
Itakumbukwa kuwa mwaka 2015 Bunge la Congress la Marekani lilipitisha sheria ya kuipa serikali ya nchi hiyo mamlaka ya kutafiti na kutumia madini na nishati nyinginezo zilizopo kwenye mwezi, na pia kusafirisha vitu hivyo kuja duniani.

Sheria hiyo inaeleza kuwa taifa hilo haliwezi kukubali jumuia ya kimataifa kutumia kanuni za baadhi ya makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa duniani, kukwamisha nchi hiyo kutumia madini na nishati za kwenye mwezi.

Sheria hiyo inafafanua kuwa mpaka wakati huu hakuna makubaliano yoyote kati ya taifa hilo na jumuia ya kimataifa kuhusu mgawanyo wa mipaka katika kuhodhi maeneo ya ardhi ya mwezi, na hivyo basi hakuna kikwazo au kigezo chochote kinachoweza kukubaliwa na taifa hilo katika harakati zake kuhodhi ardhi ya mwezi.

Aidha, mwaka jana 2019 serikali ya Rais Donald Trump iliunda kikosi cha jeshi la anga za juu ndani ya jeshi kuu la Marekani, tayari kuhami himaya na maslahi ya taifa hilo kwenye ardhi ya mwezi.

Kadhalika, kufuatia kuwepo hiyo sheria ya taifa hilo kuhodhi ardhi ya mwezi, mapema mwaka huu 2020 kiongozi huyo alisaini amri inayosisitiza kuwa Marekani ina haki ya kutafuta na kutumia raslimali katika anga la juu, ikiwemo kwenye mwezi.

Amri hiyo ilionekana kupooza makali yake pale iliposema kuwa mpaka sasa Marekani inachukulia anga za juu kama sehemu isiyo na raslimali, na hivyo nchi hiyo haihitaji ruksa au kufikia makubaliano yoyote ya kimataifa ili kuanza shughuli zake huko angani.

Yamkini, kutafuta madini kwenye mwezi kutasaidia wanadamu kuwa na uwezo wa kusafiri hadi katika anga za mbali, ikiwemo kwenye sayari zingine kama vile Mars.

Hadi wakati huu huaminika kuwa upo uwezekano wa kujenga kituo kikubwa cha mafuta kwenye mwezi, ambacho chaweza kutumika kutoa nishati kwa roketi za kusafirisha binadamu kwenda anga za mbali zaidi.

Uchimbaji wa mafuta hayo utakwenda sanjari na ukusanyaji wa hewa na gesi, kama vile hidrojeni na oksijeni hukohuko angani.

Kumiliki kituo cha mafuta katika anga ya mbali kutawezesha roketi kusafiri kwenda mbali zaidi katika anga, bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa nishati ya mafuta au gesi.

Kwa upande wake, Profesa Benjamin Sovacool anasema dunia inaelekea katika kujikita kwenye vyanzo vya nishati mbadala, kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa ambapo inahitajika raslimali tosha.

“Kwa sasa tunaelekea kumaliza raslimali tulizonazo duniani,” anasema profesa huyo wa masuala ya nishati katika Chuo Kikuu cha Sussex, nchini Uingereza.

Mkuu huyo anasema kuwa kutafuta raslimali zaidi kwenye anga za juu kunaweza kusaidia kutengeneza bidhaa zingine, kama ambavyo sasa baadhi ya magari hutumia nishati ya umeme.

"Hatua hiyo pia itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira duniani," anasema.

“Upatikanaji wa raslimali kwenye mwezi, hususan kama zitapatikana katika eneo moja, kutasaidia sana, kwani kazi hiyo itakuwa rahisi,” anafafanua profesa huyo.

Wajuzi wa baadhi ya mambo wanasema kutafuta raslimali hizo hapa duniani, mathalani katika maeneo kama Congo, Barani Afrika, kunafanyika katika mazingira hatari na ya kuogofya.

Katika amri hiyo ya Rais Trump, ni wazi kuwa hakuna sheria ya kimataifa itakayotumika kukabili juhudi za nchi yake kufaidika na raslimali zilizopo kwenye anga za mbali.
 
Na kuna jiwe liko katikati ya sayari ya mars na Jupiter limetengenezwa kwa kiwango kikubwa cha solid gold, nichekel kidogo na platnum. Thahabu iliyopo pale kwa bei ya sasa ya dhahabu, ni nyingi kiasi kwamba ina thamani ya mara zaidi ya 100 ya uchumi wote wa dunia. Shida ni kwamba ikiweza kuchimbwa ikaletwa duniani, bei ya dhahabu itaanfuka kabisa na kuifanya isiwe na thamani kabisa. Huenda mandazi yakawa na thamani kuliko bei ya dhahabu.
 
Wamarekani wanatakakutuangushua spana na mapauro ya utosi kutoka mwezini sasa.


Wapumbavu hao, wanataka kujipa hati miliki ya ardhi ya mwezi bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa!!!, hawajui kwamba mwezi ni UNIVERSAL HEAVENLY BODY na lazima kuwe na makubaliano ya kidunia juu ya matumizi au shughuli yoyote inayoweza kuleta athari huko mwezni na hatimaye athari hiyo kutokea duniani.-- Muamerika ni shetani muharibifu ambaye kwa sasa yeye ndiye anayechangia pakubwa uharibifu wa tabia nchi hapa duniani na amejitoa kutoka Tokyo treaty inayohusiana na udhibiti wa uharibifu wa tabia nchi.
 
Wamarekani wanatakakutuangushua spana na mapauro ya utosi kutoka mwezini sasa.
Usihofu,hilo haliwezekani kwani vitu vya kurudi duniani lazima vifungwe mota ndio viruke kuja huku, Hapo katikati kuna mpaka kati ya dunia na mwezi ambao hautoki mpaka uwe na nguvu hizo.
Marekani ni makeke tu hawajawahi kwenda mwezini na hawawezi kwenda kwa ajili ya madini ambayo wala hawajayaona.
 
I doubt kama mining katika mwezi inawezekana, sio kwamba hakuna minerals lakini "je hizo mineral zinaweza kuwa economically viable for mining?"
Ni expensive kuchimba madini mwezini alafu uyalete duniani.

Waseme tu lengo lao ni kumiliki maeneo mwezini. Maana mwezi una advantage nyingi katika utafiti wa anga. Moja wapo ikiwa ni kutumia mwezi kama kituo cha safari za anga.
 
Back
Top Bottom