Marekani inahusikaje na na Ugaidi sehemu mbalimbali duniani

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,349
Kwa wale wanaoamini ugaidi sehemu yoyote duniani huwa umeanzishwa na Marekani, Je sababu hasa za msingi za Marekani kufanya hivyo huwa ni zipi?

Marekani inanufaikaje na makundi mbalimbali ya ugaidi duniani yanayoua, kuteka meli na raia wake kwa ajili ya ransom?

Ni wakati gani hasa Marekani huwa inaamua kuanzisha kundi la ugaidi kama nyenzo na njia pekee ya kuwezesha maslahi yake?

Kwa nini America ya Kaskazini, Kusini/Latin America, Ulaya na nchi nyingi za mashariki ya mbali hakuna makundi ya ugaidi??
 
Sema swali lako pia umeliweka 'kipotoshaji' sana; kuwa Ugaidi sehemu yoyote duniani umeanzishwa na Marekani.

Yapo baadhi ya maeneo ambayo yanakuwa yana maslahi kwake, kwa njia moja ama nyingine, husupport vikundi vinavyoisumbua 'serikali isiyo rafiki' kwake.

Mfano vikundi dhidi ya Serikali ya Iran.

Latin America hakuna ugaidi? Wale FARC kule Columbia. Urusi yenyewe miaka ya 2000 amesumbuliwa na ugaidi wa Chechn.

Ukisoma katikati ya mistari, post yako inautazama ugaidi kuwa ule wa kiislam. Kwa mujibu wa FBI, Ndani ya Marekani kuna vikundi vya kigaidi vya itikadi kali vya mrengo wa kulia vingi kuliko vya kiislam; far right, Alt rights n.k. Wale wanaoshambulia gay clubs hawana tofauti na ISIS. So, tanua zaidi mtazamo na mjadala.
 
Kwa wale wanaoamini ugaidi sehemu yoyote duniani huwa umeanzishwa na Marekani, Je sababu hasa za msingi za Marekani kufanya hivyo huwa ni zipi?

Marekani inanufaikaje na makundi mbalimbali ya ugaidi duniani yanayoua, kuteka meli na raia wake kwa ajili ya ransom?

Ni wakati gani hasa Marekani huwa inaamua kuanzisha kundi la ugaidi kama nyenzo na njia pekee ya kuwezesha maslahi yake?

Kwa nini America ya Kaskazini, Kusini/Latin America, Ulaya na nchi nyingi za mashariki ya mbali hakuna makundi ya ugaidi??
Marekani ni taifa la shetani. Linafadhili ushoga, ugaidi, vita, mauaji nk ili tu auze silaha na kupora rasilimali
 
Boko Haram n a ISIS wanapatia wapi silaha na fedha?
Wapo matajiri wana fedha na wanahusudu itikadi za ugaidi. Unafikiria magaidi waliolipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998 walipata wapi mabomu??
 
Mbona makundi mengi ya kihuni yana ufadhil kutoka nchi kama Iran, inasemekana hata Gadaffi alikuwa na hii kitu pia.

Hii dunia au masilaha mazito yangekuwa yanamilikiwa na nchi za ile jamii ya watu wenye itikadi fulani, dunia isingekalika hii kila eneo.
 
Mimi nitajibu kwa mtazamo tofauti kidogo kwanza dhana ya ugaidi ni pana sana tofauti na vile watu wengi wanavyoisi kuwa imekaa kidini hasa kiuslamu kutetea jihadi au kuupigania uislamu ila siyo kweli ila imeenezwa sana sababu ya matukio mengi kufanyika kwenye nchi za kiislamu.

Swali kwanini marekani analaumiwa sana kwenye swala hili LA ugaidi kwa mtazamo wangu finyu marekani alizindua ukoloni mpya kwenye kivuli cha ugaidi, sema wengi hawalisemei ili alizivamia nchi hasa za kiislamu zenye rasilimali azitakazo na kuzikalia kimabavu tukianzia iraki, wote tunajua alitafuta kisingizio na kuikalia kimabavu na kuchota mafuta atakavyo, sirya amekalia hadi Leo maeneo yake yenye utajiri wa mafuta na kuyauza bila kuingiliwa na yeyote, Afghanistan aliikalia na kutoa kandarasi kwa makampuni yake kuchimba madini bila kuulizwa na yeyote, mexico ambaye ni jirani yake marekani anafaidika na biashara ya madawa nyuma ya kivuli cha CIA, Libya serikali ilipinduliwa wote tunajua nini kinaendeleaa pale saivi kwaiyo siyo kuwa wanasingiziwa hapana
 
Hujaelezea au kutoa hata mfano mmoja ni kwa jinsi gani Marekani anaanzisha makundi ya kigaidi katika hizi nchi ulizozitaja.
 
Hii dunia au masilaha mazito yangekuwa yanamilikiwa na nchi za ile jamii ya watu wenye itikadi fulani, dunia isingekalika hii kila eneo.
Ile jamii ingesababisha vita za dunia, fikiria hiyo jamii ingekuwa na hayo masilaha si ingeziangusha katika miji mizuri kama Hiroshima na Nagasaki? Ingesababisha vita baridi na mamilioni wangekufa, ingevamia nchi za watu kupora rasilimali kama mafuta kwa kisingizio cha kusambaza "haki za binadamu" na "ustaarabu" ambao wao wenyewe hawatouzingatia juu ya watu watakaowavamia. Ila kwa kuwa nguvu ziko kwenye mikono salama, dunia ina amani kabisa kila sehemu. Husikii vita Ukraine, Mexico wala DRC. Wala hakujatokea uonevu, ukoloni wala uvamizi.
 
Umejibu vema kabisa!
 
Hiroshima na Nagasaki ni matokeo ya ugomvi ulioanzia Ulaya kati ya kambi ya Hitler vs Ulaya naUSSR, US alienda kuwasaidia tu kuimaliza hiyo vita.

Chanzo vita Ukraine tangu mwaka 2014 in Urusi na hata sasa yeye ndiye amevamia jirani yake, US wanasaidia watu wanaoonewa.
 
Wapo matajiri wana fedha na wanahusudu itikadi za ugaidi. Unafikiria magaidi waliolipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998 walipata wapi mabomu??
Unayajua mabomu yaliyotumika!?..madude yamechongwa humuhumu tu!..halafu mmoja alikua mfanyakazi ubalozi wa marekani Kenya,baada ya pale marekani akazipenya nchi zilizokumbwa na hiyo kadhia kuliko mwanzo na baada ya 9/11 marekani alizipenya takriban nchi zote duniani,ni aidha uwe nae au uwe na magaidi
 
Chanzo vita Ukraine tangu mwaka 2014 in Urusi na hata sasa yeye ndiye amevamia
Umeleta mada huku tayari ukiwa na majibu. Kosa ni kulazimisha hicho unachokiamini wewe ndiyo sahihi zaidi!!!!!!!!!!!!!!

Kwa kusoma kwangu kote vitabu mbalimbali (mpaka sasa) nimekuja kugundua kuwa dunia inaendeshwa kwa siri kubwa na kikundi kidogo cha watu. Hicho unachokifahamu wametaka wao, na wataamua kipi wewe ukifahamu na kipi usifahamu.

Mimi na wewe (najua utabisha)hatuufahamu ukweli ni upi na uongo ni upi!!!!!!!!! Kinachofanyika ni kuunganisha nukta yaani kutumia fikra tunduizi ingawaje nayo ni kubahatisha!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mfano mdogo: Wenye Tanzania yao wanafahamu baada ya rais Samia nani anayefuata na atakayefuatia!!!!!Sisi tutakachofanya ni kutabiri na kubahatisha!!!!!!!!!!! wenyewe wamekwisha panga na kuamua!!!!!!!!!!! Hiyo ni Tanzania, je huko duniani????????
 
Umechanganya mambo mengi yasiyohusiana hata na huu uzi pamoja.
 
Back
Top Bottom