Marekani, gari lapata ajali na kuruka kuingia ndani ya ghorofa.

Marekani, gari lapata ajali na kuruka kuingia ndani ya ghorofa.

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,292
Gari moja lililokuwa linaendeshwa kwa kasi katika jimbo la California hapo jana liliruka na kuingia ndani ya ghorofa ya juu kwenye jumba moja baada ya kugonga uzio wa kutenganisha barabara.

Sehemu moja ya gari ilibaki ikining'inia nje ya jengo hilo huku watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo wakinusurika na majeraha madogo.

Polisi wameambia wanahabari kwamba dereva wa gari hilo anadaiwa kutumia dawa na alikuwa ametembelea hospitali moja.

Ajali hiyo pia ilisababisha kuzuka kwa moto mdogo ambayo wazimamoto walifanikiwa kuuzima.

Kisa hicho kilitokea Santa Ana, maili 35 (56km) kusini mwa Los Angeles.
FB_IMG_1516085494178.jpg

FB_IMG_1516085487414.jpg
 
Barabara za juu si nzuri. Bora TANESCO Ubungo linavyovunjwa. Semi ingeweza kuingia Pale
 
Back
Top Bottom