Marekani anaweza kuziwekea nchi zote duniani vikwazo?

Marekani anaweza kuziwekea nchi zote duniani vikwazo?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,050
Reaction score
12,968
Nimewaza tu.

Urusi pale walipo isingekua vikwazo vya Marekani ingekua iko mbali sana ila miaka na miaka Moscow imekua ikiishi kwa vikwazo.

Juzi Rais Putin ametangaza silaha mpya ya supersonic ila akasema wanategemea mfulululizo wa vikwazo kutoka Washington na wamejiandaa, watakabiliana navyo.

Marekani kamuwekea vikwazo Iran kwa zaidi ya miaka 40, isingekuwa vikwazo vya Marekani sasa Iran ingekuwa mbali sana ila miaka na miaka wanachezea vikwazo juu ya vikwazo. Sasa hali ni mbaya zaidi Iran.

Marekani kaiwekea vikwazo Korea kaskazini kwa miaka zaidi ya 70, vikwazo vimeinyong'onyesha sana Korea kaskazini.

Hali ni mbaya, juzi Kim Jong Un amesema raia wake wanapitia magumu sana sababu ya vikwazo vya Marekani.

Marekani kawekea jeshi la China vikwazo, katishia kuiwekea vikwazo vikubwa China vinginevyo ije kwenye majadiliano na China kakubali matakwa ya Marekani, wako kwenye majadiliano. Kawekea makampuni mengi ya china na mengine yamekufa kabisa kina ZTE.

Marekani alitishia kuiwekea Umoja wa Ulaya vikwazo, alitishia kuiwekea Mexico na Korea vikwazo vinginevyo wakubali kurekebisha mkataba wao wa kibiashara na kweli Mexico na Canada wakakubali, hakuna namna.

Huko America ya Kusini nchi zote zimelazimika kukubaliana na matakwa ya Marekani kukwepa vikwazo.

Kwa sasa Italy uchumi wake unapumulia mashine baada ya Marekani kuweka vikwazo kadhaa kwenye mauzo yake ya nje.

Barani Afrika Mugabe tu ndie alipigwa vikwazo, tunajua maisha ya Wazimbabwe.

Je, Marekani anaweza kuziwekea nchi zote duniani vikwazo na bado asidhurike?
 
Kwa level ya Uchumi walio nao.. zaidi Dola Trillion 12 ..na jinsi Dunia Tulivyo ungana na kutegemeana..pia matumizi ya Dollar kwenye international trade.. Kinaifanya Marekani kuiwekea inchi yoyote vikwaZO.. Mpaka sasa hamna ichi inayiweZa kuichallange USA
 
Africa hatuwezi kuungana tukaiwekea vikwazo Marekani? Maana nchi nyingine zinaogopa kuiwekea vikwazo.
 
Wanasaidia nchi maskini nyingi. Misaada inayogusa maisha ya watu kama ARV hivi.
Rais wa Bank ya dunia anateuliwa na Rais wa Marekani.
Mashirika ya UN bajeti yake kubwa inatoka US.
Sasa wakisema usifanye biashara na huyu, huna ubavu wa kukataa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchumi wa Jimbo la California peke yake ni mkubwa kuliko nchi yote ya ufaransa// uchumi wa Texas ni mkubwa kuliko Saudi Arabia na mafuta yake yote uchumi wa USA ni mkubwa Sana mwaka 2012 bank moja tu iliyumba ilikuwa inaitwa Lehman and Brothers uchumi wote wa dunia ulidondoka na hiyo ni bank moja tuuuuuu
 
Hivi uchumi wa Afrika nzima unaweza kulingana na uchumi wa Yew York?
 
Hii ni ngumu kwasababu uchumi wetu tunamtegemea Marekani kuanzia madawa, Silaha mpaka bajeti ya nchi. KIngine ni mnunuaji mkubwa wa bidhaa zetu kwahiyo haiwezekani.
Africa hatuwezi kuungana tukaiwekea vikwazo Marekani? Maana nchi nyingine zinaogopa kuiwekea vikwazo.
 
Gambino,

Ndio anaweza kumuwekea yeyote vikwazo kwa sababu anamiliki mtandao wa kutuma hela popote.

Pamoja na dola ya marekani kuwa ndo sarafu ya dunia kwenye manunuzi lakini bila Marekani kumiliki mfumo wa kutuma hela wasingeweza kujua ni nani na nani wanatumia fedha fulani.

Mtandao huu uitwao SWIFT CODE. Uwezo wa kuweka vikwazo kwa yeyote atakayekiuka masharti yake unatokana na yeye kuwa na access na huo mtandao.

Benki nyingi na taasisi nyingine za fedha zinapewa masharti kwamba usifanye biashara na fulani na ukifanya nae ujue tayari unazuiwa kutumia soko la Marekani pamoja na benki za Kimarekani.

Hakuna anayeitaka hiyo hasara maana tayari utaenda nje ya biashara baada ya muda mfupi kwa sababu hutapata access ya fedha zako kutoka popote.
 
Hivi uchumi wa Afrika nzima unaweza kulingana na uchumi wa Yew York?
Ujue kwamba New York ndio financial center ya dunia Manhattan street Ni rich huo ni mtaa tuu sasa jiji zima la new york Ni even richer than the rest of Europe combined.

Put together
Uk
German
France
Italy

Hizo ndio babe za ulaya na hazifui dafu kwa new york
 
Kwa level ya Uchumi walio nao.. zaidi Dola Trillion 12 ..na jinsi Dunia Tulivyo ungana na kutegemeana..pia matumizi ya Dollar kwenye international trade.. Kinaifanya Marekani kuiwekea inchi yoyote vikwaZO.. Mpaka sasa hamna ichi inayiweZa kuichallange USA
Dollar hata dunia nzima iache kuitumia abaki yeye, Canada, Israel na U.K ataendelea kuwa juu.
Kinachomfanya aendee kuwa juu nu uwezo wa jeshi lake na namna lilivyo sambaa hapa Afrika mashariki tu tunao
 
Nchi nyingi za ulaya zinaongozwa na uchumi wa michezoya kamali,pesa nyingi iko kwenye mzunguko huo,na ndio sector inayoongoza sana kwa mapato mengi, wenzetu wanaishi kwa ujanja wa akili sisi tunaishi kwa nguvu pasipo kutumia akili,

The level if thinking makes us differ from them, viongozi wa kiafrica kama Mugabe walioweza kufikia thinking capacity za wazungu, mzungu akikujua una taka kuharibu maslahi yake anakumaliza maana fikilia yeye hana ardhi, hana madini, law material zote ana import, ukilinganisha na nchi mfano yetu, wametumia njia nyingi sana, wanaishi wakiwaza maisha ya kizazi chao si chetu, misaada anayotoa mzungu nyuma ina msumari wake, ila kwa mtu asiyejua anaona wana roho safi ila ukweli unafahamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Africa hatuwezi kuungana tukaiwekea vikwazo Marekani? Maana nchi nyingine zinaogopa kuiwekea vikwazo.
Hiyo URUSI tu ni kubwa kubwa kuliko
download (1).jpeg
bara zima la Africa.....Brazil peke yake ni nusu ya bara la Africa.
 
Anaweza kuweka vikwazo popote duniani kwa kuwa ni superpower Wa dunia,mambo yote yanaanzia marekani,uchumi,siasa,jeshi vyote kashikilia yeye fikiria dola ya marekani tu..inatumika nchi zote duniani INA maana biashara zote za kimataifa lazima zifanyike kwa dola,sasa ukiwekewa vikwazo usiuze biashara zako kimataifa..huwezi toboa kabisa,bado nguvu ya kijeshi hakuna nchi itaishinda marekani kiubunifu Wa silaha na teknolojia mpya za kivita,bado ushawishi Wa kisiasa kwa nchi nyingi duniani...marekani inachukuliwa kama mfano Wa kuigwa kidemokrasia.
 
Gambino, Kama ulimaanisha nchi zote Duniani kwa wakati mmoja haiwezekani, kwa maana hata yeye hataweza kununua au kuuza kwa nchi nyingine, ila kamakila moja kwa wakati wake inawezekana kwa maana kila nchi duniani inaushirikiano na Marekani ama wa moja kwa moja au kupitia taifa jingine.
 
Back
Top Bottom