Marehemu Mwl.Irenge hakulipwa mafao yake: Aibu ya Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marehemu Mwl.Irenge hakulipwa mafao yake: Aibu ya Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Elli, Aug 2, 2012.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Juzi kwenye mazishi ya marehemu Mzee James Irenge ambaye alikuwa mwalimu wa baba wa taifa Julias Kambarage Nyerere katika shule ya Msingi Mwisenge ambaye alifariki akiwa na umri zaidi ya miaka 120 niliona na kusikia kitu cha aibu sana, ushuhuda wa ajabu, huu ulitamkwa na kiongozi wa familia hio ambaye niliskia kwa maskio na macho yangu kuuona anchokisema kuwa hadi Mzee Irenge anafariki dunia bado alikua akiidai serikali mafao yake ya Ualimu ikiwamo nauli ya kusafirishiwa mizigo yake.

  Hili lilizungumzwa mbele ya kiongozi wa kitaifa na tangu juzi nimekua nikifuatilia kuona labda kutakua na hatua yoyote itakayokuwa imechukuliwa na viongozi wa kitaifa lakini suala hili limekuwa kimya na hakuna alieoneka kujiguswa na statement ile. hali ile niliitafsiri kuwa ni aibu kubwa kwa taifa ambalo limekuwa likijivunia kutunza watu exceptional kama hawa!!!


  Wasi wasi wangu ni kuwa; kama hili limefanyika kwa mtu kama huyu, vipi hal;i ya walimu hawa wa "kawaida" wasio na title yoyote? Ni lini kazi na utu wetu vitaheshimiwa? Source ya Taarifa Hii ilikua ni ITV taarifa ya habari
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Bado Irene ssra aje kutupiga mabovu baada ya kufikisha miaka 55!
   
 3. K

  Konya JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  that true,ilikuwa ni aibu kama sina kumbukumbu nzuri mengine yalikuwa ni madai ya toka miaka ya sabini na cha kushangaza hii issue haijapewa uzito unaostahili kabisa
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Hakuna hata media moja ukiacha JF ambayo iliripoti, as if jamaa alikua akiripoti majungu flani hivi
   
 5. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,474
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Kwa miaka 120 inamaana alistaafu kabla ya uhuru, hata mwanafunzi wake(baba wa taifa) alimsahau kweli? au kuna kitu kimekosewa hapo.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,072
  Likes Received: 6,536
  Trophy Points: 280
  kweli waalimu hawawekwi sawa kwenye madai yao.
  but watalipwa kuanzia 2015.
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Huo ndio ukweli, na aliyesema hayo ni mwanae mbele ya waziri mkuu
   
 8. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,474
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180


  Sasa hapo wa kulaumu ni nani, huyu mtu alistaafu hata kabla mwanafunzi wake hajaingia Ikulu.Je katika uhai wake aliwahi kudai madai yake? huo mda ni mrefu sana ni vigumu kujua hata faili lilipo.
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Mpwa, swali lako la kwanza sidhani kama lina mantiki yoyote, vivyo hivyo na swali la pili
   
 10. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kubwa kwa taifa hili na ni laana ambayo bila shaka itakumbuka viongozi wote walio poka haki ya marehemu. Walimu wote watakuwa wamelaaniwa na hata wakidai stahili zao mbalimbali watapuuzwa tu. Kapuuzwa mwalimu wa Nyerere itakuja kuwa wasote vumbi?!!!
   
 11. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,474
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180

  Mkuu huyu mtu amestaafu miaka karibu kumi nyuma ya uhuru. Hapa wa kulaumiwa ni nani hasa.
   
 12. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Ile taarifa ya habari hata mimi siku ile iliniacha hoi.

  Alistaafu miaka ya sabini lakini hadi anafariki hakupewa mafao yake.

  Sasa SSRA wanataka malipo yafanyike baada ya kustaafu, je, mareehemu huyu mbona alistaafu lakini hakupewa hadi familiya wakamuomba Waziri Mkuu Pinda awasaidie ili iwasaidie usafiri.

  Sasa kama huyu Mungu alimjaalia kuishi miaka 120, je akina sisi tutaishi miaka mingapi???

  Je, Waziri mkuu atakuja kwenye mazish yangu ili watoto wangu wamuombe awasiadie wapate mafao yangu??


  Kweli Serikali ya CCm haitutendei haki kabisa.  MIZAMBWA
  INAIUMA SANA!!!
   
 13. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  For god's sake guys dont politisize this. Mwalim nyerere was born in 1922 and went to school probably when he was 10 so that makes him being in primary school up to may be 1942 . and this teacher was probably employed during colonial time prior to vita ya pili. and if he taught for 30 years he must have retired in late 50's hence retirement benefit probably paid by the colonial govt and if he was employed by missionaries;;;;; Kuna wazee wengi hawakulipwa pensheni zao up to vifo vyao. My grandfather retired from railways in 1951 his benefits ceased after uhuru, pia kuna wazee walipigana vita ya 2 ambao wapo hai hadi leo na hawalipwi pensheni. Huyu mzee probably kutokana heshima ya kumsomesha mwalimu ndiyo maana alikuwa anapewa hiyo favour.
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Hio ndio issue ya msingi
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Ni mwanafunzi yupi unayemuongelea???

  Mwalimu Irenge alikuwa ni MWalimu aliyemfundisha Mwl. julius Nyerere. Miaka ya Sabini Nyerere ndiye alikuwa Rais wa Tanzania.

  Na pia hawa wote walikuw na uhusiano mzuri kwani hata kabla ya Kifo cha baba wa Taifa, Mwl. Irenge alifika kumjulia khali kule Butiama mara kwa mara.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,474
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Sina tatizo na hilo, ila najaribu kujiuliza huyu mtu amefariki akiwa na miaka 120. Kwa utaratibu wa kustaafu wa kufikisha miaka sitini inamaana alistaafu miaka sitini nyuma kipindi ambacho tulikua hatujapata hata uhuru. Katika hali kama hiyo binafsi nashindwa kuelewa hata tatizo lilipoanzia.
   
 17. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280

  Siku ile ya mazishi ya MWl. Irenge kwenye Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku iliwekwa hewani, na waziri mkuu Pinda aliwakilisha Serikali, mtoto wa marehemu alitoa ombi la kuwa baba yao alistaafu miaka ya sabini lakini bado alikuwa hajapewa pensheni yake hadi leo. Hivyo familiya inamuomba waziri mkuu awasaidie wapate pensheni ya mzee ili iwasaidie usafiri.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!!
   
Loading...