Marando: Tunamtaka Rais mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marando: Tunamtaka Rais mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gambatoto, May 31, 2011.

 1. g

  gambatoto Senior Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKILI Mabere Marando anayemtetea Profesa Costa Mahalu aliyekuwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, amesema ataiomba mahakama imlazimishe Rais Jakaya Kikwete kufika mahakamani kumtetea mteja mteja wake iwapo hatakubali kwenda kutoa ushahidi baada ya kuombwa kufanya hivyo kwa barua.Marando ametoa kauli hiyo wakati Profesa Mahalu na mwenzake Grace Martin wakianza kujitetea leo.

  Mbali na utetezi wao binafsi, wanatarajia pia kuwa na mashahidi kadhaa wa kuwatetea akiwamo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa pamoja na Rais Kikwete.Tayari Rais Mkapa amewasilisha mahakamani hapo hati yake ya kiapo akimtetea Profesa Mahalu na mwenzake kuhusiana na tuhuma zinazowakabili huku akibainisha kuwa yuko tayari kufika mahakamani iwapo italazimu.

  Lakini hadi jana, Rais Kikwete alikuwa hajajibu barua aliyoandikiwa na Wakili Marando kwa niaba ya wateja wake wakimwomba akubali wa kufika mahakamani kuwatetea au kuwasilisha kiapo chake ambacho kitatumika kama ushahidi wa utetezi dhidi yao.

  Marando alisema jana kuwa Rais Kikwete alikuwa hajajibu barua hiyo, lakini akasema ikiwa Profesa Mahalu atamaliza kujitetea pamoja na mashahidi wengine kabla Rais Kikwete hajakubali, wataiomba mahakama imkumbushe.

  “Kama atakaidi hata baada ya mahakama kumwandikia, basi tutaomba kesi hiyo iahirishwe hadi mwaka 2016 (wakati atakapokuwa amemaliza muda wake wa urais) ili imlazimishe kuja kutoa ushahidi huo,” alisema Marando.

  Mei 3, mwaka huu Wakili Marando alimwandikia barua Rais Kikwete yenye kumbukumbu namba MM/PCRM/2011/1 kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, akibainisha kuwa ni miongoni mwa mashahidi muhimu ambao wateja wao wamewaagiza wamwite.

  Barua hiyo inabainisha kuwa umuhimu wa Rais Kikwete katika ushahidi huo wa utetezi unatokana na ukweli kwamba nyumba hiyo ya Ubalozi wa Italia ilinunuliwa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na kwamba alikuwa na taarifa zote kuhusu mchakato wa ununuzi wake.

  Mchakato huo, kwa mujibu wa barua hiyo ni pamoja na nguvu ya kisheria aliyopewa mteja wao ambayo ilisainiwa na Rais Kikwete wakati huo akiwa Waziri Septemba 24, 2004 pamoja na hotuba yake aliyoitoa Bungeni Agosti 3, 2004 akithibitisha kuwa ununuzi wa jengo hilo haukuwa na mushkeli wowote.

  Pia barua hiyo inaweka wazi kuwa kuna barua nyingi tu ambazo Profesa Mahalu alimwandikia Kikwete akiwa waziri, pamoja na katibu mkuu wa wizara hiyo, ambazo anapaswa kuzitambua mahakamani wakati wa utetezi.

  “Kwa hiyo tunaomba kwa unyenyekevu kabisa, uweke barua yetu hii mbele ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania; aisome na akueleze utujibu kama hana pingamizi kuja kueleza ukweli mahakamani. Kama muda wake hauruhusu, kulingana na ratiba zake za kitaifa, tunaomba aturuhusu tumwandalie kiapo (affidavit) kitakachoeleza yaliyotekea ili tukiwasilishe mahakamani badala ya kumwita yeye mahakamani”, inasisitiza barua hiyo na kuongeza kuwa hakuna kifungu cha Katiba kinachozuia Rais kuitwa kutoa ushahidi mahakamani.

  Katika kiapo chake alichokiwasilisha mahakamani, Mkapa anamtetea Mahalu na akidai kuwa amefanya naye kazi kwa muda mrefu na anamjua kuwa ni mtu mwaminifu, mtiifu na mchakapakazi. Mkapa alieleza katika hati yake hiyo kuwa mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wa uongozi wake na kwamba alikuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na ununuzi huo na kwamba ulifanyika kwa mujibu wa sheria.

  Alifafanua kuwa mpango wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa ni utekelezaji wa sera ya serikali wa kuwa na majengo yake ya kudumu katika kila ubalozi kwa kununua au kujenga ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za upangaji. Aliongeza kuwa serikali yake ilimpa Profesa Mahalu mamlaka yote kupitia nguvu ya kisheria ya kusimamia na kutekeleza mchakato wa ununuzi wa jengo.

  Mkapa alisisitiza kuwa kupitia utaratibu wa serikali, alikuwa akijua kuwa taarifa ya uthamini wa jengo hilo iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi ilikuwa ni Dola za Marekani 3.0 milioni wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilikadiriwa Euro 5.5 milioni: “Kupitia utaratibu wa serikali nilifahamu kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa gharama ya Dola za Marekani 3.0milioni sawa na Euro 3,098,741.40,” alisema Mkapa.

  Pia Mkapa alisisitiza kuwa alikuwa na bado anatambua taarifa ya serikali bungeni ya Agosti 3, 2004 iliyoeleza na kuthibitisha kuwa taratibu zote za ununuzi wa jengo hilo zilifuatwa kwa mujibu wa maelekezo ya serikali na kwamba dalali alilipwa kikamilifu.

  “Kwa kipindi chote ambacho nimefanya kazi na Balozi Mahalu katika nafasi mbalimbali za utumishi wa serikali ameonyesha tabia thabiti na za dhati, uaminifu, utiifu, uchapakazi na ubora," alisema Mkapa.

  Alisema kuwa sifa hizo zilimfanya atunukiwe na Rais wa Italia, Tuzo ya Heshima ya Juu wakati wa kuadhimisha Siku ya Taifa hilo, muda mrefu baada ya kuwa ameondoka nchini humo.

  Profesa Mahalu na mwenzake, Martin aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo wanakabiliwa na mashtaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60. Wanadaiwa kusababisha hasara hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo la ubalozi huo, wakati wa utumishi wao.

  Kutokana na mashtaka hayo, leo wanadiplomasia hao wanaanza kujitetea baada ya mahakama hiyo kuwaona kuwa wana kesi ya kujibu.Mahalu na Martin wanadaiwa kula njama na kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti na katika maeneo tofauti huko Italia, likiwamo la kumpotosha mwajiri wao katika hati ya matumizi.

  Miongoni mwa mashtaka hayo ni kwamba Septemba 23, 2002 huko Rome, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walisaini vocha yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa bei ya ununuzi wa jengo la ubalozi ni Euro 3,098,741.58, maelezo ambayo yalikuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.

  Source: Mwananchi
  Marando: Tunamtaka Rais mahakamani
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Marando mbele ya mahakama ya maoni ya watu ana credibility kweli ikija kwenye upambanaji dhidi ya ufisadi?

  Wadau mnaonaje? Mimi kwangu hana.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ooh noo.. akikataa kuitikia haipaswi kuahirishwa kesi bali itolewe amri ya mahakama na Polisi waende kumkamata na kumleta mahakamani. Akikataa Bunge linamuondoa kwani anakuwa amevunja Katiba kitu ambacho ni "impeachable offense".
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  You wish...
   
 5. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mh Mzee wa kijiji

  Labda hiyo itatokea kwenye miaka ya 2090, ambapo hayamkini kati yetu kizazi hiki tutakuwa tumeisha itika kwa mola wetu.
  lakini kwa kipindi hiki cha kina ustadhi Chande Jaji Mkuu na maustadhi wengi kwenye kona mbalimbali za nchi hii tusilitegemee hilo,
  kwani mategemeo yangu nisingekuwa nategemea kuwa Saidi Mwema na crews wake wangekuwa bado madarakani.
  Hivyo basi kwa Tanzania yetu hii hatujawa na viongozi waadilifu,ambao wanaelewa kwamba cheo ni dhamana na wako tayari
  kuachia ngazi ili kuilinda hadhi yao.
   
 6. n

  nitasemaukweli Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well tutaona dance ya katiba ya ccm. Mtuhumiwa anataka atetewe na Mkapa na aliekuwa waziri wa mambo ya nje, kikwete. Ufisadi kama kawaida na kilichobaki ccm ni kupelekana mahakamani kama video vile. Sasa ngoma yenu na mzigo wenu si tunaangalia kama mnataka kuwachezea watanzania ngoma ipi ya kumfanya huyu mwizi wa mamilioni ya Watanzania walk free again.

  ccm dance mahakamani kwao, tunajua aendi mtu jela ni kama show to....Katiba mpya ndio fundisho kwenu nyie
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hii itakuwa kali, serikali inapeleka mtu mahakamani then mkuu wa serikali hiyo hiyo anatakiwa akamtetee. What a shame!
   
 8. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,084
  Likes Received: 1,121
  Trophy Points: 280
  "If wishes were horses even beggars would ride"
   
 9. The sage

  The sage Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Rais kwa kukaidi kwake, kwangu mimi naona kuna mawili: ama ni dharau kwa mahakama ambacho ni chombo muhimu katika taifa letu au uhuru wa mahakama haupo.
   
 10. DJ CHOKA FREDY

  DJ CHOKA FREDY Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ni kifungu gani cha sheria au ndani ya katiba yetu kinachomzuia rais kuacha kutoa ushahidi hata kama watu walifuja pesa kipindi yeye hajawa rais,,,,aende bhana akatoe huo ushahidi mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake yeye si ndiye alikuwa waziri enzi hizo na kila kitu kilikuwa chini yake, sisi bado tunarukaruka hapa tunamsubili :dance::dance::dance::dance::dance:
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umesahau hii?
  Waziri: Dowans ni haki yao lazima walipwe
  Rais: Mimi ni mmojawapo wa wanaopinga Dowans wasilipwe
   
 12. DJ CHOKA FREDY

  DJ CHOKA FREDY Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa nani hapo anamshitaki mwezake au ndo watz tunadanganywa kama watoto????:smow::smow::smow:
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Tutajionea mengi
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  You will never imagine when things wil turn up soo abruptly bro tena hatuta fika 2015 ndipo mtajua kuwa kizazi kilichopo tayari kimeanza badirika na hao watakao kuwa ni wagumu kubadilika my friend watakuwa wakimbizi nadani ya nchi yao, sidhani kama twaitaji kufika 2090 hii hali itabadilika now now watanzania hamto amini kabisa,   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  aje mahakamani...na tunamsubiri sana huku mahakamani....maana maelezo yake ni muhimu
   
 16. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Issue inakuwa ni pale yeye alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani, aliwahi kutetea manunuzi hayo bungeni kwamba hayakuwa na mushkheri, leo hii ni serikali yake ndiyo imemshitaki kwa wizi ambao yeye alishawahi kumkania. Je itakuwaje leo akienda mahakamani akasimamia kile alichokizungumza bungeni kwamba jamaa si mwizi wakati yeye huyo huyo kupitia serikali yake ndio wanaodai ni mwizi! Si atakuwa anajipinga mwenyewe!
   
 17. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JK akimtetea Mahalu inakula kwake, akimzamisha inakula kwake ...

  Ila ninataka kuamini kwamba kuna kitu kulitokea wakati Profesa akiwa balozi na Jk akiwa waziri na matokeo yake ndo tunayaona sasa.

  Kaazi kweli kweli
   
 18. k

  kiloni JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aende akacheze usanii tumemzoea; Jakaya Kikwete the most unpopular president of the century. SHAME!! TZ!! SHAME VOTERS SHAME SHAME!!!
   
 19. semango

  semango JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kazi kweli kweli
   
 20. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... style hii inajulikana kama ... CALLING THEIR BLUFF
   
Loading...