1.
Murangira
Senior Member
--------------------------------------------------------------------------------
Historia na kumbukumbu zinaonyesha kwamba wewe Es umekuwa na beef na Mbowe muda wote wa maisha yako. Je unataka leo niamini kwamba umeanza tena kuendeleza fitina ambazo zinaonekana hata kule CCM?
Mimi nimetoa hoja, lakini kama kawaida wewe unataka personal badala ya kujibu hoja, here I come,
Freeman, ni rafiki yangu wa karibu toka tukiwa watoto, alipopata ajali kwenye ile miaka ya 80s pale Salender Bridge, mimi nilikuwa ninacheza Disco RSVP, nilipoambiwa tu niliacha starehe zangu, na kuwa mtu wa kwanza kufika pale na ku-secure gari na mali zake pale kwenye scene ya ajali, na kuhakikisha kuwa usafiri wa kumepeleka Hospitali umepatikana, na mali zake zote pale zimefikishwa nyumbani kwake Sea View, ndipo nikaenda Hospitali Muhimbili, na washikaji wengine walioujiunga nasi mpaka asubuhi.
Mara ya mwisho alipoalikwa na Rais Bush, kuhudhuria mkutano wa Republican Party, kule NY mimi nilikuwa kule kwa shuguli zangu binafsi, na nilikuwa nilishirikiana naye throught out mpaka mwisho wa shughuli zake, baba yake mzazi alikuwa ni rafiki yangu zaidi na nilikuwa nikikaa naye sana kupiga story pale Sea View, familia yangu na ya Freeman, ni very intact, nimehudhuria vilivo vingi sana vya familia yake, na yeye pia na familia yake wamehudhuria sana ya kwetu, please hili la personal beef ba Freeman ninaomba uliondoe mawazoni mwako kuwa hata yeye na familia yake wakikusikia watakucheka sana!, maana to this day we are very close kifamilia!
2.
Maana Malecela bila ya aibu na utu na hata bila ya kujali kwamba ni mzazi ila kwa kulinda tumbo lake na kwa uchache wao alitoa maneno makali dhidi ya Zitto na kuhitimisha kwamba atimuliwe Bungeni.Sasa yule mzee na labda uwezo wake wa Kisiasa sasa umefoikia kikomo kwa utetezi wake jambo kama lile .
(a). Malecela, sijui anahusiana nini na hoja yangu,
However, Malecela ni mzee mwenye umri wa miaka 72, unless wewe kwenu hakuna wazee, maana wangekuwepo usingekuwa na tatizo la kuelewa kuwa wazee huwa hawaongezeki uwezo wa kisiasa wakifikia umri huo, ila huwa wanaongezeka busara zaidi kwenye any professional waliko,
(b). Hoja ya kumfukuza Zitto, bungeni alikuwa-created na Luwaassa, ambaye moja ya shughuli zake bungeni ni kusimamia shuguli za serikali ndani ya bungeni, ilishinikizwa na Mundhiri, na kupigiwa kura na wabunge wote walikokuwepo, Malecela alichangia kama mbunge, na makamu wa mwenyekiti wa CCM, na alichangia maoni yake kutokana na ishu ta hand, wabunge wengi walipiga kura ya kumsimamisha bunge kwa kufuata sheria za bunge, huo ulikuwa ni uamuzi wake binafsi kama una tatizo nao mtumie ujumbe au muandikie barua, na uwaaidikie wabunge waote waliohusika kumfukuza Zitto bungeni, hakufukuzwa kwa kura moja ya Malecela,
(c). Malecela, hakupiga kura wala kutoa maoni yake kwa ajili ya tumbo, hapana, maana yeye kama waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais mstaafu, kisheria ya taifa letu taifa linampatia nyumba mbili, moja Dodoma, nyingine Dar, walinzi wa personal na nyumbani, chakula, wafanyakazi wa ndani, magari mawili mapya kila mwaka, safari mbili za nje ya nchi kwa matibabu kila mwaka, ujumbe wa kudumu cc na NEC, mpaka atakapoitwa kwa muumba wake.
And this works for Kawawa, Seif Hamadi, Salim, Warioba, Sumaye, Mwinyi, Mkapa, Bilali, na Salmin.
Now guy, Malecela hahitaji kufanya kazi yoyote at this point and time kupata hayo mafao juu, hayo mafao yapo pale pale afanye kazi au asifanye, awe mwansiasa au asiwe, ajiunge na upinzani au asijiunge, mafao yatakuwa pale pale, kwa hiyo hoja ya tumbo uliyoisema ni mufilisi mkuu! sasa anaishi kwa mafao, haishi kwa mshahara wala posho!
3.
Huoni kwamba hii ni advantage hata Malecela anaweza kuinga mkono kama kweli Mbowe , Mrema na Marando ni mali yao kwa kuwa wanaisaidia CCM .Je wewe huna furaha kwamba Chama chako kina msaada toka kwa hawa tu ?
Furaha yangu ni pale tu, viongozi wetu wa upinzani na CCM, wanapofanya kazi ya kulisaidia taifa, lakini siwezi kuwa na furaha ya kuwa na kina the Marando likes kwenye siasa yetu, ninawaheshimu Zitto, na Dr. Slaa kwa sababu uwezo wao bungeni sijui kama unaweza kufikiwa na Freeman na Marando walipokuwa humo humo bungeni, ninaomba uniambie Freeman na Marando, walifanya nini walipokuwa bungeni?
Lakini ninamuheshimu Freman, kwa kuipa, meno makali Chadema, na kuweza kuwapatia Zitto na Slaa, platform ya kulisaidia taifa letu, lakini misaada ya kina the Marando likes kwa CCM, au kina Tambwe na Akwilombe, au Guninita? No thank you hawa hawana msaada wowote ila wanajali matumbo yaka ulivyosema, lakini hawana faia kwa taifa langu!
4.
Maana maandiko yako yanaonyesha hasira kubwa kwa hawa watu 3 .Je unaweza kuelezea ni kipi cha mno?
Mwananchi yoyote mwenye akili timamu atakayesoma huu ujumbe wako na wangu, sina sababu ya kuwa na wasi wasi kwake kuelewa mwenye hasira kati yangu na wewe ni nani, hilo wala halinisumbui maana ninaiamini sana hii forum kwenye hilo la kuchagua mchele na pumba!
5.
Umesema hawa jamaa si wapinzani means ni CCM wenzio , je unaweza kuthibitisha madai yako maana labda mnashiriki wote katika vikao vya kuuza Nchi au ni bla bla zako za kima mara za ku derail ukweli ?
Je na wewe unaweza kuthibitisha madai yako kuwa hawa kina Marando, ni upinzani?
6.
Heshima kwako nisaidie majibu
Heshima ikurudie mara mbili mkuu, na tuendelee kukta ishu na kumkoma nyani giladi mpaka milima ya Sinai!