Mzee Chifu,
Hawa wazungu wote kwenye ofisi za ubalozi zao bongo wana maafisa wa ujasusi, kuanzia CIA, KGB, FBI, M16, Mount Royal-Canada, siku hizi mpaka NYPD wana majasusi wao hapa bongo,
wakati wa uchaguzi wetu wa rais, na wabunge kazi yao hawa jaamaa ilikuwa kuangalia kwa makini interest zao hapa bongo, na hasa dini za viongozi, kwani interest kubwa yao hapa sasa hivi ni Mujahadina, na Al-Queda, kwamba hawatapata safe haven,
kwa hiyo hawa majajsusi, tayari walishapeleka habari za rais mpya hata kabla hajachaguliwa kule Dodoma, ndani ya CCM, ndio maana mabalozi wa UK na US walikuwa hawaishi majumbani kwa JK na JM, kile kipindi kila wiki, tena walikuwa wakiwafuata mpaka Dodoma na Bagamoyo/Chalinze,
kwa hiyo habari za JK zilikuwa kule State Department siku nyingi, hata kabla mzee hajaenda kujitambulisha, na rais wa US na West kwa ujumla tayari walikuwa na habari zake zote, in details,
Now lets look at kujitambulisha, unaendaje kujitambulisha kwa rais ambaye tayari ulishaarifiwa kuwa hana nafasi ya kukuona? Bush aliambiwa hana nafasi, Kule German hivyo hivyo aliambiwa hana nafasi, mzee Blair ndio kabisaa hana nafasi, lakini rais wetu akaenda anyway! kujitambulisha kwa mawaziri na kina Chenney, what a shame! Kina Mwai Kibaki na Kagame wanakwenda kwa safari za kibinafsi lakini wanapokelewa na Bush mwenyewe kule Rose Garden na mpaka Oval Office, lakini wa kwetu aliyekuja rasmi kujitambulisha wanaishia kule Watergate Office kwa kina Chenney, aibu!
Yaani hata huyu mama wa ujerumani naye amekataa kuwa yuko bussy, so far rais wetu amepokelewa na mzee Chirac tu na tunajua siri yake anataka kuchukua miradi yote inayomilikiwa na US hapa bongo, maana US imechukua miradi yake yote kule Sierra Leone, na Senegal, na Congo-Zaire, kwa kuwatumia kina Kagame na M7,
Mzee JK, na Mtandao hizi sifa zitawaua, tulitegemea kuwa rais mpya atasimamisha safari za viongozi wetu wote wa taifa kwa angalau miaka miwili tu ili kuweka mambo sawa hapa nyumbani, kumbe ni yale yale ya Mkapa, ya kutaka ujiko nje huku nyumbani kumeoza, mnakimbilia kuvaa suti kwenda kwa wazungu ambao they are so bussy kiasi kwamba hawana nafasi ya kuwaona marais mnaowakilisha wananchi karibu 40 Millioni!
Ni lini mtasikia aibu kama waafrika na kutulia kwenu kama wazee wa Swazi na Botswana, ambao hawaendi huko kila leo lakini nchi zao ni bomba na kila siku tunakimbilia huko bondeni? Aibu acheni hizo!